Facts 13 kuhusu Lowassa na Uchaguzi 2015

Facts 13 kuhusu Lowassa na Uchaguzi 2015

OgwaluMapesa

JF-Expert Member
Joined
May 24, 2008
Posts
10,942
Reaction score
437
1. Lowassa, ndiye mgombea mtarajiwa pekee mwenye wapenzi na mashabiki wengi kwa sasa....

2. Lowassa, ndiye mgombea mtarajiwa pekee mwenye wasifu na historia kubwa na iliyotukuka katika utendaji wake ndani ya Chama Cha Mapinduzi na Serikali kwa ujumla..

3. Lowassa, ndiye mgombea mtarajiwa pekee ambaye mpaka sasa kashawishiwa na makundi mengi sana ya kijamii, eg. Wakulima, wafanyabiashara, bodaboda, wafugaji, Mamalishe, wachimbaji wadogo wa madini, wanafunzi, wachungaji n.k

4. Lowassa, ndiye mgombea mtarajiwa pekee mwenye ushawishi na nguvu ndani ya Chama Cha Mapinduzi na jamii kwa ujumla (rejea tafiti na takwimu mbalimbali)

5. Lowassa, ndiye mgombea mtarajiwa pekee aliyeonyesha uzalendo wake kwa kupigania Nchi yake katika vita vya Kagera 1978/1979. Kwa Nchi nyingi duniani kupigana vita ni sifa muhimu na ziada kwa mtu anayewania uongozi. Kushiriki kupigana vita huchukuliwa kuwa ni kiwango cha juu kabisa cha uzalendo...

6. Lowassa, ndiye mgombea mtarajiwa pekee mwenye maono yaliyowazi katika kuwakomboa wananchi kwa kuonyesha vipaumbele vya Taifa eg. Elimu, Elimu, Elimu, Afya, Kilimo, Kuondoa umasikini, kukuza uchumi n.k

7. Lowassa, ndiye mgombea mtarajiwa pekee aliye maarufu na ambaye wananchi wana matumaini naye kwa sasa. Hii inatokana na utendaji kazi wake na uwezo wake mkubwa wa kusimamia jambo eg. Shule za kata, mradi wa maji ziwa Victoria, Chuo cha UDOM, maamuzi ya City Water, viwanja vya Mnazi Mmoja na plot No. 125~157 Mikocheni n.k

8. Lowassa, ndiye mgombea mtarajiwa pekee mwenye maamuzi magumu na sahihi kwa manufaa ya wananchi na Taifa kwa ujumla...

9. Lowassa, ndiye mgombea mtarajiwa pekee atakayeweza kusimamia, kurudisha na kuleta nidhamu kwa viongozi na watendaji wa serikali na mashirika ya Umma...

10. Lowassa, ndiye mgombea mtarajiwa pekee mwenye nguvu wa ushawishi wa hoja kwa wananchi na katika vikao mbalimbali vya maamuzi (rejea kikao cha maamuzi kuhusu matumizi ya maji Ziwa Victoria nchini Misri, rejea kikao cha kupitisha maamuzi ya ujenzi wa UDOM n.k)....

11. Lowassa, ndiye mgombea mtarajiwa pekee aliyejiandaa kisaikolojia kuingia Ikulu (rejea uchambuzi wa Prof. Kitila Mkumbo)....

12. Lowassa ndiye mgombea mtarajiwa pekee mwenye sifa za ziada kama...
i. Mchapakazi kwa bidii
ii. Msikivu
iii. Mbunifu
iv. Muadilifu
v. Mpenda watu/wananchi
vi. Mvumilivu & Mstahimivu

13. Lowassa, ndiye mgombea mtarajiwa pekee mwenye dhamira na nia ya dhati kuondoa umasikini uliokithiri (Absolute Poverty)....

Mytake: kwa hizi facts zote, ni wazi Lowassa kwa sasa tunakuitaji kuliko kipindi chochote kile katika historia ya Nchi hii...
 
Lowassa anatosha huwezi mlinganisha na msanii Membe au Sitta eti mwanamume kushindana mpaka mwenzako akatwe jina ubebwe na meza huuu Ni upuuzi sana wa akina mzee fulani wa ccm
 
Mkuu ocampo four utaficha uso wako wakati Lowassa atakapoangukia pua. Tanzania ya sasa haiwezi kuongozwa na adui wa maendeleo kwa ufisadi. Lowassa hana sifa hata za kuendelea kuwa Mbunge kwakuwa madoa yake ya ufisadi hayafichiki.
 
Last edited by a moderator:
Mangula pia mnafiki kutwa vikao vya siri na Jack Gotham ndo maadili hayo? Mangula na nape mnatumika kulipa fadhila lakini nawaambieni wana CCM hatudanganyiki na jidanganyeni eti mmewahi kukata watu na chama hakijayumba nawaomba sana mjaribu haka kamchezo kenu ambacho mnakapangia mikakati ya gizani eti kuwasuprise wanaccm Naapa pigo mtakalo pata mtaandikwa kwenye vitabu vya historia ya ccm
 
Nilikuwa sijaangalia ni jukwaa lipi hili.....aaagh kumbe ni mahusiano,mapenzi na urafiki ccm
 
14.Lowassa ndio fisadi pekee kutoka ccm ambae amepata heshima ya kutajwa na baba wa taifa kwamba asipewe uongozi wa nchi hii milele na milele.

Ndo maana hii nchi inalaaniwa kuamini Nyerere ananafasi ya Mungu nyerere kitu gani ameiacha nchi hoi taabani acha usengele
 
Lowasa ndio waziri mkuu pekee aliyefukuzwa kazi kwa ajili ya wizi na mikataba mibovu

lowasa ndio mgombea pekee anayeshawishi watu kwa pesa eti kwenda kumuomba agombee

lowasa ndio mgombea pekee aliyekataliwa na mwl j.k nyerere

Tanzania ndo nchi pekee inaishi kwa kutegemea wafu
 
Lowasa afya yake sio timamu na anaweza asiwe na afya timamu wakati ukifika, pia Lowasa ni mtu wa visasi, nani achague Robbot

Lowasaa ni mkristo safi anayeamini katika kusamehe 7 mara 70..... Swala la afya siyo kweli Edward yuko fiti asilimia 100, na infact hilo ni swala ambalo mamlaka nayo analo Mungu.....
 
Back
Top Bottom