music mimi
JF-Expert Member
- Jun 16, 2013
- 441
- 758
Tukubali tukatae Mbosso ni msanii mkali kabisa wa kizazi cha sasa cha bongofleva.
Ana aina yake ya uhandishi, anauimbaji wa tofauti wa pwani, ana weza kutengeneza idea nzuri ya nyimbo.
Naweza sema angepata fair airtime kama ya wasanii wengine kwenye local media zote kwa sasa ndio angekuwa msanii namba moja bongo.
Lazima tukubali ndio msanii wa wcb aliyeathiriwa zaidi na beef za media kwa label yake.
Lazima watu wa wcb wakubali kuna kitu kikubwa wanapoteza kwa kuendeleza ugomvi na awa wakongwe wa burudani na wanaoathirika ni wasanii wao ambao bado wanategemea local media (mavoko, mbosso &lavalava.)
Washabiki wa muziki wa bongo wana utamaduni wa kuaminishwa ndio waamini ilo ni jambo lisiloitaji ubishani. Kuna watu wanaamini XXL ndio wapitishaji wa ipi ni nyimbo nzuri na uwezi wabadilisha , kuna watu ambao ni wengi ikiwemo watangazaji wanaamini sana endorsement ya B 12 kwenye wimbo au Gardner G Habash kwao wimbo au msanii akipitishwa na awa watu ni heat.
Najua wenye team mtanishambulia lakini naamini WCB bado wanaitaji kuona namna ya kumaliza tofauti na media sababu sioni media kubwa kama IPP au Clouds zikiomba suluhu na wasafi.
Bado nasisitiza kungekuwa na fair kwenye airtime basi sasa hivi tungeanza kusahau ushindani wa Kiba na Diamond ambao hauna nguvu tena. Sasa hivi tungekuwa tunazungumza Mbosso na Aslay na ingekuwa ni burudani nzuri sana sababu ya vipaji vya awa wawili.
CC chige Chinga One data LAKI si pesa Daudi Mchambuzi
Last edited: