sky soldier
JF-Expert Member
- Mar 30, 2020
- 5,408
- 19,033
Ni kweli kwamba huwa kuna mameneja wanazingua lakini pia tusisahau kuna wasanii nao huwa wanazungua
Lazima tuelewa vizuri mazingira ya wasanii, management na soko kwa jumla.
Wasanii wengi wanapoianza kazi ya miziki wanakuwa hawajiwezi kwa lolote, Hivyo hulazimika kutafuta management itakayoweza kufanikisha kutimiza ndoto zao kwa kulipia gharama.
Msanii na Meneja hujikuta wakiingia mikataba nafuu kwasababu ya ualisia wa biashara yenyewe ya muziki siku zote huwa ya kubahatisha.
Ndio maana mameneja wengi huwa wanasifiwa kwa kumtoa msanii mmoja tu kati ya wengi alionao.
Kazi ya management hiyo kwanza ni kuhakikisha msanii anatunga nyimbo nzuri zitakazoenda kulitingisha soko, Baada ya hapo kulipia gharama za kurekodi audio na video, ikiwa ni pamoja na mavazi kuanzia unyayoni mpaka utosini.
Baada ya hapo kulipia promo kwenye radio na TV station zote ili nyimbo zipigwe kila kukicha, kisha linakuja swala la kum'brand msanii ili kumuongezea thamani angalau naye uonekane ni mtu fulani kati ya watu.
Katika hili ndipo pesa zinapoteketea kwani management ina wajibu wa kuhakikisha msanii anavaa vizuri kuanzia viatu hadi kofia, management pia uhakikisha msanii lazima akae kwenye nyumba nzuri inayoendana na hadhi ya kisanii, gharama za saluni na mahitaji muhimu ya nyumbani zikiwemo samani za nyumba nzima na chakula cha kila siku pamoja na usafiri.
Fahamu kuwa wakati haya yote yanafanyika, ni pesa ya meneja ndio inayoteketea. Promo inapokubali kwenye media, ndipo wanaanza kujitokeza watu wa pembeni na kuanza kumshika masikio msanii, Hapo ndipo maneno ya "unaibiwa wewe yaani nyimbo zimehit bado huna kitu?" Baadhi ya wasanii wengi huwa ni mambumbumbu kwani huwa wanakubali kujaa upepo kirahisi bila kujali gharama ilyotumika imerudi au bado.
Hii husababisha msuguano mkubwa kati ya meneja na msanii. Kwani hasara huwa ni kubwa kuliko faida.
Suala la hili lilikuwa fundisho kwa mameneja kadhaa huko nyuma ndio maana ujinga huo umefanyiwa marekebisho kwenye Lebo ya WBC, ukitaka kusepa lazima uzitapike kachumbari zote ulizokula !!.
Kuna muda wasanii ndio wanazingua !! Tatizo sio mameneja bali akili ya baadhi ya wasanii ni kama ya wadangaji, Hawana uchungu gharama waliyowekezewa, wanajiangalia wao tu.