Fact Check: Picha zinazosambaa, sio maiti za bahari ya Pemba wakati wa Kampeni

Fact Checkers

Member
Nov 29, 2010
5
45
Salaam Wakuu,

Kwenye Mitandao ya Kijamii (hasa Twitter), kuna habari (picha) zinasambaa kwamba ni Miili ya watu iliyotupwa Baharini huko Pemba Wakati wa Uchaguzi Mkuu Tanzania 2020.

20201224_112510.jpg
20201224_112512.jpg
20201224_112515.jpg
Screenshot_20201224-112845.png

Picha zinaambatana na maneno kwamba, "Jeshi na Polisi wanatupa maiti baharini muda huu

Wanafukuza wavuvi ufukweni maiti zinatolewa kwenye roli ya jeshi zinatiwa kwenye boti ya JWTZ zinakwenda kutupwa baharini".

Baada ya kufuatilia kwa kina, tumekuta picha hizo sio za Tanzania. Na hii ni baada ya kuona Video nzima ambayo ilitumika kuscreenshot hizo picha zinazodaiwa ni miili ilitupwa baharini na vyombo vya Usalama vya Tanzania.

Picha zinazosambaa ni za Mama mwenye miaka 33 ambaye aliokolewa baada ya gari lake kutumbukia baharini Mombasa.

Winnie Achieng' aliripotiwa kufariki katika hospitali ya Coast General ambapo alikuwa amekimbizwa na wasamaria wema.

Achieng' alikuwa pamoja na mwanawe Gift Otieno wakati wa tukio hilo lakini mwanawe alifaulu kuogelea hadi nchi kavu.

Kulingana na ripoti ya polisi, Achieng' alikuwa akijaribu kupita gari lingine kwenye eneo la Makupa kabla ya kutumbukia majini.

"Ilifanyika wakati dereva alikuwa akijaribu kupita pikipiki iliyokuwa mbele yake lakini gari lake likagonga mawe na kupoteza mwelekeo na kutumbukia baharini," ripoti ya polisi ilisema.

Gift, mwenye miaka 12, alifanikiwa kuruka lakini Achieng alipatikana akiwa amezirai baada ya kunywa maji mengi.

"Gari hilo lilikuwa kwenye kasi. Nililiona likielekea kwenye Kisiwa cha Mombasa na kisha ghafla nikaliona limetumbukia baharini. Nilikimbia kuwaokoa waliokuwepo," Omar Chigamba aliambia gazeti la Nation.

Hivyo si kweli kwamba picha hizo ni za Maiti wa Pemba.

Pia soma > Mama afariki, mwanaye anusurika baada ya gari kutumbukia baharini


Hapa Chini ni Video inayoonesha tukio hilo la Kenya Mombasa ambapo hizo picha zimechukuliwa na kudai ni Pemba Tanzania.

 

denooJ

JF-Expert Member
Mar 31, 2020
3,861
2,000
Usitufanye watoto kutuletea picha za tukio la huyo mama aliezama baharini Kenya halafu unaambatanisha na maneno yako ili ujaribu kuficha ukweli wa kile kilichotokea huko Pemba wakati wa kampeni za uchaguzi wa mwaka huu.

Hili sio jukwaa la watoto.
 

Imeloa

JF-Expert Member
Jan 28, 2013
7,144
2,000
Hoja ni nini sasa, ina maana kuna anayepinga kuwa hakuna watu waliouliwa Pemba.

Kwenye huu utawala watu waliokwisha uliwa wanafika 1,000 kabisa halafu bado Magufuli anadai hawezi kutia sahihi mfungwa anyongwe. Unafiki gani huu.
 

tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
38,342
2,000
Huwa nawashangaa mno Watanzania ambao hupenda Kuchafua Taswira yetu ya Amani na Utu Kimataifa. Kuna Watu Uzushi utawagharimu sana.

Ww ni mshirika wa uovu hapa nchini, ndio maana unalazimisha kuficha uovu kwa kisingizio cha kulinda taswira ya nchi. Ni hivi, taswira ya nchi hii tayari ni chafu, sasa sijui unataka iwe chafu mara ngapi.
 

kolola

JF-Expert Member
Apr 26, 2020
1,684
2,000
Weka hizo video hadharani ili tuzione.

Maiti zilizookotwa kwenye viroba ufukweni mwa bahari 2016 Mwigulu Nchemba alidai ni miili ya Wasomali na alipotakiwa aweke ushahidi hadharani ili tujue kahitimisha vipi kwamba ni miili ya wasomali alishindwa kufanya hivyo.
Ulivyo mpuuzi watu wanazungumzia 2020 wewe unababwaja na matukio ya 2016
 

mkorinto

JF-Expert Member
Jun 11, 2014
20,379
2,000
ndio siasa maandazi za tz zilipofikia kwa sasa.

inafikia hatua hujui nani tapeli nguli,kati ya ccm na wanaojiita wapinzani.
 

USSR

JF-Expert Member
Jul 15, 2015
5,193
2,000
Askofu unateseka sana na roho yako mbaya .umeumbuliwa tulia tu
Weka hizo video hadharani ili tuzione.

Maiti zilizookotwa kwenye viroba ufukweni mwa bahari 2016 Mwigulu Nchemba alidai ni miili ya Wasomali na alipotakiwa aweke ushahidi hadharani ili tujue kahitimisha vipi kwamba ni miili ya wasomali alishindwa kufanya hivyo.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom