Serikali inatembela unabii wa Jomo Kenyata, kwamba Nyerere anaongoza Maiti

SOVIET UNION

JF-Expert Member
Sep 2, 2017
455
1,283
Naamini kabisa Watawala wanatembelea maneno ya Jomo Kenyata kwamba kule Tanzania Nyerere anatawala Maiti.

Jomo Kenyata alikuwa sahihi sana na aliona mbali au alishaona kabisa kwamba kule Tanzania Nyerere anaongoza Maiti.

Yanayo endelea kwa sasa ni prove tosha ya Jomo Kenyata, angalia watawala wanafanya wanacho taka au wanavyo jisikia na hakuna kitu raia tunafanya, Leo hii bei ya sukari haishiki na Wakina Bashe wanakuja na majibu simple sana kwa sababu wanajua wanatawala maiti.

Angalia Migao ya umeme,tunaenda mwaka wa pili sasa na huu mgao na haiwakoseshi usinguzi watawala kwa sababu wanajua wanatawala Maiti. Nchi hii kinacho wapa nguvu wawatala ni aina ya watawaliwa waliopo.

Sio Polisi, wala Jeshi, wala Usalama wa Taifa unao wapa Watawala nguvu bali ni aina ya Raia wanao tawaliwa ndio hao sana wanao wapa nguvu kubwa sana. Kuna watu wanazania labda Serikali inategemea Jeshi la polisi hapana, inajua fika inatawa aina ipi ya watu.

Wasingekuwa wanatawala Maiti kauli kama za Kipindi kile Mwigulu kwamba Hamieni Burundi kama hamtaki Tozo zisingeweza tolewa, Ile statment haiwezi tolewa kwenye Taifa jingine ambalo raia wake wako hai make huo moto hakuna atakaye weza kuuzima.

Watawala wamejaa dharau na viburi kwa sababu wanajua wanatawala aina ipi ya watu.

Kwa sababu ya kutawala Maiti ndio maana wao wanawekeza sana kwenye anasa za kutisha ilihali hao naiti wanashinda njaa, hawan ajira.

Jomo Kenyata alisema yeye anatawala Wagonjwa au watu walio mahututi na wanaweza amka wakati wowote ule na ikawa balaa na ndio kinacho tokea leo hii Kenya.

Kenya angalia Walimu wao kila Mwaka sana Migomo ya kudai nyongeza za mishara, Tanzania haiwezi tokea hakuna Mwalima wa Kugoma labda wagomeee whatsapp.

Hawa watawala wanajua fika wanaongoza aina ipi ya watu na hakuna kitu kinawapa presure wala kuwakosesha usingizi.
 
Ni kweli kabisa angalia maigizo ya Makonda, maigizo ya aina ile huwesi yapata kokote kule kwenye hii sayari,kwa kifupi hawa CCM wanacheza na akili za watu ambao asilimia kubwa ni kama maiti na hapo ndio Serikali imewekeza sana kwenye maigizo kuhadaaa watu. Makonda ana pigia simu Waziri kuhadaaa wajinga ionekane kuna utawala unao wajibika kwa wananchi.
 
Back
Top Bottom