Fact Checkers
Member
- Nov 29, 2010
- 5
- 22
Salaam Wakuu,
Kwenye Mitandao ya Kijamii (hasa Twitter), kuna habari (picha) zinasambaa kwamba ni Miili ya watu iliyotupwa Baharini huko Pemba Wakati wa Uchaguzi Mkuu Tanzania 2020.
Picha zinaambatana na maneno kwamba, "Jeshi na Polisi wanatupa maiti baharini muda huu
Wanafukuza wavuvi ufukweni maiti zinatolewa kwenye roli ya jeshi zinatiwa kwenye boti ya JWTZ zinakwenda kutupwa baharini".
Baada ya kufuatilia kwa kina, tumekuta picha hizo sio za Tanzania. Na hii ni baada ya kuona Video nzima ambayo ilitumika kuscreenshot hizo picha zinazodaiwa ni miili ilitupwa baharini na vyombo vya Usalama vya Tanzania.
Picha zinazosambaa ni za Mama mwenye miaka 33 ambaye aliokolewa baada ya gari lake kutumbukia baharini Mombasa.
Winnie Achieng' aliripotiwa kufariki katika hospitali ya Coast General ambapo alikuwa amekimbizwa na wasamaria wema.
Achieng' alikuwa pamoja na mwanawe Gift Otieno wakati wa tukio hilo lakini mwanawe alifaulu kuogelea hadi nchi kavu.
Kulingana na ripoti ya polisi, Achieng' alikuwa akijaribu kupita gari lingine kwenye eneo la Makupa kabla ya kutumbukia majini.
"Ilifanyika wakati dereva alikuwa akijaribu kupita pikipiki iliyokuwa mbele yake lakini gari lake likagonga mawe na kupoteza mwelekeo na kutumbukia baharini," ripoti ya polisi ilisema.
Gift, mwenye miaka 12, alifanikiwa kuruka lakini Achieng alipatikana akiwa amezirai baada ya kunywa maji mengi.
"Gari hilo lilikuwa kwenye kasi. Nililiona likielekea kwenye Kisiwa cha Mombasa na kisha ghafla nikaliona limetumbukia baharini. Nilikimbia kuwaokoa waliokuwepo," Omar Chigamba aliambia gazeti la Nation.
Hivyo si kweli kwamba picha hizo ni za Maiti wa Pemba.
Pia soma > Mama afariki, mwanaye anusurika baada ya gari kutumbukia baharini
Hapa Chini ni Video inayoonesha tukio hilo la Kenya Mombasa ambapo hizo picha zimechukuliwa na kudai ni Pemba Tanzania.