Face Masks (Barakoa) ziwe lazima kwa watu wote

carlross

Member
Sep 28, 2013
26
45
Nchini singapore ni kosa mtu kutoka bila kuvaa barakoa/ mask ! endapo hili litakiukwa mtu atalipishwa faini ya $300 na akirudia atalipishwa $1,000

Czech republic na slovakia ni nchi nyingine ambazo zimepitisha sheria ya kila mtu lazima avae barakoa ili kupambana na ugomnjwa huu wa COVID19.

Inafurahisha zaidi ambapo kwenye nchi ya czech republic kulikuwa na kampeni ya kitaifa na uhamasishaji wa watu wa kuvaa barakoa ambazo zimetengenezwa nyumbani, watu walihimizana wakatengeneza na wakagawa bure mask ili kucontrol uenezaji wa ugonjwa hii.

Czech republic ni kati ya nchi zilizopunguza kwa kiasi kikubwa ueneaji wa covid19 kwa wananchi wake na ni nchi iliyotumia njia zote wengine waliokuwa wanatumia kukiwa na mabadiliko kweye sehemu ya sheria za barakoa tu,
wanafunzi na vijana wameungana na kuteneneza barakoa nyumbani zenye asilimia 100% cotton , na kuna sehemu maalumu za kucollect hizo mask kupitia website Damerousky.cz, na manispaa mbalimbali pia hugawa mask kwenye vulnerable groups za nchi hiyo.

KUMBUKA: HIZI NI JITIHADA ZA WANANCHI KUHAKIKISHA KILA MTU ANAVAA BARAKOA/ MASK!

TANZANIA:
viongozi wetu wapitishe sheria ya Barakoa/Mask kuvaa ni LAZIMA na sio ombi! then tuanze kampeni ya nchi nzima ya kutengeneza barakoa ! wenigne wakijitolea pia kuwasaidia watu wenye kipato cha chini barakoa! polisi wahakikishe watu wanavaa barakoa/ Mask

Hakikisha na wewe unavaa barakoa kila saa kila dakika, maisha yamebadilkika Huu ni utamaduni mpya na haina budi
kuufwata,

masks4all.jpg
 

Ncha Kali

JF-Expert Member
Sep 19, 2019
4,371
2,000
Halafu kwa TZ hiyo kitu ipo Dasilamu tu, mikoani wala hatuna habari.... hivyo basi sheria zenu zijikite huko huko lisiwe suala la kitaifa.
 

carlross

Member
Sep 28, 2013
26
45
Halafu kwa TZ hiyo kitu ipo Dasilamu tu, mikoani wala hatuna habari.... hivyo basi sheria zenu zijikite huko huko lisiwe suala la kitaifa.
lipo sema hujui tu, hili ni swala la kitaifa lakini tuanze kwa spidi hapa dar es salaam,
 

JAYJAY

JF-Expert Member
Oct 31, 2008
3,892
2,000
Hao viongozi wanatumia bajeti ya ofisi kupata barakoa. Ukitaka iwe sheria na kila mwananchi apewe kwa bajeti hiyo hiyo sio kuwatwisha watu mizigo ambayo nyie wenyewe viongozi hamuwezi kuibeba.
 

carlross

Member
Sep 28, 2013
26
45
Hao viongozi wanatumia bajeti ya ofisi kupata barakoa. Ukitaka iwe sheria na kila mwananchi apewe kwa bajeti hiyo hiyo sio kuwatwisha watu mizigo ambayo nyie wenyewe viongozi hamuwezi kuibeba.
Hahahahahahha Barakoa za bure bure tena zile za masaa manne manne ,surgical masks sio?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom