Ezekiel Maige: Kamati teule ilikuwa na kinyongo na Mimi

Noti mpya tz

JF-Expert Member
Mar 23, 2011
974
244
Mbunge wa msalala Yuko Star Tv hivi sasa katika kipindi cha medani za siasa pamoja na mambo mengine amesema yeye alipokuwa waziri wa maliasili na utalii hakukuwahi kusafirishwa mnyama yeyote hai kwenda nchi za nje, hata sungura hakusafirishwa.

Issue ya twiga alikuta tayari ilishafanywa ila Kamati teule kwa ungomvi wa Mtu na Mtu individually wakaamua kumsingizia yeye ili aondolewe kwenye nafasi yake kwa chuki.

Binafsi naona Kama anamlaumu Mh. Lembeli ambaye Kamati yake imekuwa mwiba kwa mawaziri, kila inaposoma ripoti yake imekuwa ikiondoka na mawaziri. Refer Juzi kwenye op. tokomeza.

Update.
Mh. Maige amesema anapenda rais ajaye awe jasiri Kama Ezekike Maige ambaye alidhubutu Kutenda yaliyoshindikana wizarani, yeye Hana kundi katika wale wanaotajwa kugombea urais mwaka ni.
Anasema rais ajaye Kama Ataona yeye Maige anafaa Kuwatumikia watanzania Yuko tayari Kuwa waziri tena.

Update;
mh. Maige anasema kesi iliyoko mahakamani inahusu Maafisa wanyama pori aliifungua yeye ila waziri aliefuata akawa anajitangaza Kuwa ni yeye, kusema watanzania wamhukumu kwa utendaji wake na uzalendo wake kwa taifa.
Kalaumu waandishi wa habari kwa kuendesha kampeni za uongo/kupotosha ukweli wa mambo.
 
Aisee jamaa alisahau nn pale wizarani? Hata kama watu wanaulilia uwaziri ila huyu jamaa amezidi..
Jaman wadau wenye acces wamsaidie kupata anachokililia bure akafa kwa mawazo
 
Aisee jamaa alisahau nn pale wizarani? Hata kama watu wanaulilia uwaziri ila huyu jamaa amezidi..
Jaman wadau wenye acces wamsaidie kupata anachokililia bure akafa kwa mawazo
Afe tu kwani nini???!!!!
Ana nini ambacho unique kikikosekana wizara itayumba???!!

Kuna watu hawana shukurani kabisa,hivi huyo ana calober ya uwaziri wa wizara hiyo????!!!
 
Kama Waziri,alifanya juhudi gani Twiga wetu kurejeshwa? Aende zake kule

Tupatupa wa Lumumba

Swali hili anayetakiwa kujibu ni Membe maana wapo Uarabuni.
Mimi nadhani jukumu la kulinda wanyama wetu tuwakabidhi WWF(world wildlife fund) maana Wizara imeshindwa hata juzi wameua Faru tena mbugani Serengeti alaf yule bishoo Nyalandu anauza sura tu.
 
Eti hajaamua kugombea tena ubunge 2015. Eti akiombwa na wana msalala ndo ataenda kugombea! Kumbe akina zitto wapo wengi. Muda utakapofika atakuwa wa kwanza kukimbilia fomu hafu akipigwa chini na magamba kwenye kura za maoni utasikia atakavyoanza kujambajamba kama anavyofanya kupigwa chini uwaziri
 
Huyu jamaa hajakubali tu.

Mkuu bei ya mafuta,umeme,simu,authority,prestige yote sasa nehiii!!!!!
Saa hizi traffic wanamsimamisha "mzee naomba kukukagua"na anatii enzi zile haikuwepo hii tyre kwa kilomita Yokohama, Dunlop, Michelin! !!!!!!

Misafari ya nje na simu za washika dau pia quishney!!!

Kihoro mchezo nini
 
Uwaziri mtamu aisee, safari kila kukicha, bahasha za A3 size zimejaa noti zinagongana tu mlangoni. Wanyama wote hao kwanini suiwe bilionea ni haki yake kumwaga chozi kwakuwa wakiteuliwa huwa tunawaandika eti waziri........... ameula, kwali wanaula?

Aisee jamaa alisahau nn pale wizarani? Hata kama watu wanaulilia uwaziri ila huyu jamaa amezidi..
Jaman wadau wenye acces wamsaidie kupata anachokililia bure akafa kwa mawazo
 
Mwambieni maige aridhike na ubunge wake,alichaguliwa na wanamslala kuwa mbunge,uwaziri aliteuliwa tu kwa utashi wa mh.rais,isiwe nongwa kuukosa,kila siku lawama,lawama,na kujivuna alifanya hiki na kile,haitamsaidia kitu,atimize wajibu wa wapiga kura wake ili uchaguzi wa mwakani arudi bungeni,ni ujinga tu kudhani alionewa,kila siku kulialia tu,maana alishajiona eti naye anatosha kuwa rais wetu,tulishakusahau maige jamani,amini kwamba wewe sii waziri na jk hana sababu ya kukurudisha ndani ya baraza,tumezichoka lawama zako bhana,kama vipi nenda mahakamani ukaudai uwaziri wako,na zaidi ya yote,huna cha kujilinganisha na kagasheki ,sema tu uwaziri uliupata kama zari la mentali.
 
Msaka tonge kapokonywa mdomoni tonge akiwa hajalimaliza sasa anawayawaya hapa kazi ipo kauwaziri katamu aisee asikuambie mtu.
 
Ila kachana nimependa,sasa kama bado ana hope za kurudi tena kwenye uwaziri afanye mazoezi maana ile big tummy yaweza pasuka.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Back
Top Bottom