Ezekiel 18:21


Yesu wangu nampenda sana, usimchafue kiasi hicho.Unamlinganisha Yesu Kristo na sangoma!Kama ni mkiristo unapashwa kutubu mara moja.
 

Naam tena MUNGU azidi kusema kwenye ZABURI 16:10 - 11
...Maana hatakuachia kuzimu nafsi yangu,
Wala hatamtoa mtakatifu wake aonje uharibifu.+

11...Utanijurisha njia ya uzima;
Mbele za uso wako ziko furaha tele;
Na katika mkono wako wa kuume
Mna mema ya milele
 

hii mada nzima imejaa udini tu! Wana jf wa madhehebu mengine inakuwaje sasa?
 

.
Prophet, wewe je hutakufa?
Maana kama ni habari za maisha baada ya haya mimi nami naamini ila haipaswi ku-politise(kufanya neno la Mungu siasa).
 
<br />
<br />MBONA TUNAAMBIWA UKIMFANYIA DHAMBI ROHO MTAKATIFU HUSAMEHEWI?
 
Je Nyoka wa Musa wa wana wa Israel ilikuwa nini?
Je Yesu alipompaka kipofu tope na akaona ilikuwa nini?
Biblia ni kitabu kigumu kama ilivyo na imani.

Kitu cha msingi mimi nadhani ni kuacha tu MUNGU aitwe MUNGU.

Huyo nyoka aliishia wapi? Je, hukuona jinsi watu walivyogeuka na kuelekea ibada ya mungu nyoka mpaka ikabidi aangamizwe? Tukitazama tena kuhusu miujiza ya Yesu Kristo katika agano jipya ilikusudiwa kumdhihirisha kwamba ni Mungu. Na pia tukitazama matokeo ya miujiza hiyo (matunda) hata huyo aliyepakwa tope alikiri kuwa Yesu ni Mwana wa Mungu. Kwa maana nyingine miujiza yooooooooooooooooooote aliyofanya Yesu (hata na wanafunzi wake) ilimtukuza Mungu na watu waliacha njia zao mbaya na kumgeukia Mungu wa kweli.

Enter Loliondo. Je, kuna mabadiliko gani ya kiroho baada ya watu kupokea kikombe cha maajabu? Je, watu wanamrudia Mungu na kuacha njia zao mbaya? Maana kila anayezungumza anaonyesha tu jinsi gani babu anavyotisha.

Kuna swali moja la muhimu ambalo najiuliza. Huyu babu anadai ametokewa na Mungu. Je ni katika nafsi ipi alijidhihirisha? Mbona simsikii babu akitaja kuhusu YESU KRISTU ambaye ndiye aliyeukomboa ulimwengu na Yeye pekee ndiye njia ya uzima? Kama nimekosea nisameheni lakini ni kweli kabisa sijasikia chochote kuhusu Yesu Kristo hapo Loliondo.

Tena kuna mwingine ametokewa na Bikira maria na kwamba naye ameonyeshwa mti unaotibu magonjwa sugu ukiwemo ukimwi. Sasa hapo hapatatosha. Mimi nafikiri tupime kila jambo kwa maandiko. Maandiko yanasema mtawatambua kwa matunda yao (Mathayo 7:16)
 
.
Prophet, wewe je hutakufa?
Maana kama ni habari za maisha baada ya haya mimi nami naamini ila haipaswi ku-politise(kufanya neno la Mungu siasa).

nitakufa.

ila ninaamini kutokwenda kwa Babu kutaniongezea siku za kuishi. Amen!
 


hii siyo sehemu ya mahubiri..............
 
2. Lowassa anajiwinda kwa gharama yoyote kutaka kugombea urais upande wa CCM, lakini dhambi alizotenda tunazifahamu na yeye anazijua, ndiyo maana alijiuzulu kwa sababu ya dhambi hizohizo, na wala hajawahi kusimama na kuwaomba radhi watanzania, na sasa anataka kugombea urais. Hajatenda yaliyo halali na haki. Huyu Lowassa hataishi milele, atakufa.[/QUOTE]

Mhubiri 10:16,17
"Ole wako, nchi, akiwa mfalme wako ni kijana, Na wakuu wako hula asubuhi! Heri kwako, nchi, mfalme wako akiwa mtoto wa watu, Na wakuu wako hula wakati ufaao, Ili makusudi wapate nguvu, wala si kwa ajili ya ulevi.
 
Kijana usipotoshe watu kwa andiko moja la Biblia bila kujua tafsiri yake. Biblia utaielewa tu kama utakuwa unasoma na kutambua maana ya maneno yanayoandikwa, nadhani hujui tafsiri ya kifo katika Biblia......kifo kinachozungumziwa katika Biblia na ambacho tukimtii Mungu tutakiepuka ni kile kinachotenganisha maisha ya milele.

Yesu Kristo mwenyewe alikufa, hakuna binadamu yoyote ambae ataepuka kifo, hiyo ni laana ambayo imeshapita tangu hapo dhambi ya Eden. Cha kuepuka hapa ni hukumu baada ya kifo, kwamba wale wataoitii sheria yake basi watapona na kuishi maisha ya milele lkn wale wasioitii basi watatimiza adhabu ya kifo.

Tambua kuwa Mungu hashuki mwenyewe bali hutumia wewe na binadamu wengine kusaidia watu wake, hivi kama watu wanaokwenda Loliondo wanapata nafuu kwa magonjwa yao na wanaenda kwa kuamini Mungu wewe kinachokuwasha ni nini????? Usichezee Biblia na tafsiri zake kama hujui kitu unachoelewa.
 

We unayejiita nabii, u nani wewe uwezaye kumhukumu mtu? Huwezi jua pengine alishatubu. Kwa hiyo mie nadhani mwenye uwezo wa kumhukumu mtu mwenye dhambi ni Mungu,
 

...........lakini mtu mbaya akighairi na kuacha dhambi zake zote alizozitenda, na kushika amri zangu zote na kutenda yaliyo halali na haki, hakika ataishi, hatakufa.

Niongeze Biblia inasema "....ya kale yamepita, tazama!yamekuwa mapya"(2Wakorintho 5:17).

(Mathayo 5:45- 47).

........Ili mpate kuwa wana wa Baba yenu aliye mbinguni; yeye huwaangazia jua lake waovu na wema, huwanyeshea mvua wenye haki na wasio haki.
 
EZEKIEL 18:21 ''''...lakini mtu mbaya akighairi na kuacha dhambi zake zote alizozitenda, na kushika amri zangu zote na kutenda yaliyo halali na haki, hakika ataishi, hatakufa.

unaweza kuanzia mstari wa EZEKIEL 18:20-


tusitumie vitabu vya mungu kusafisha watu nasema patachimbika nyi subirin tu agombee hlf tuone labda nife
 
Hapo kwenye blue: hivi na hao watakao mchagua kuwa rais watakuwa na akili kweli...?

Hatachaguliwa na wananchi bali kamati ya uchaguzi itachakachua na kumuingiza madarakani kwa asilimia zaidi 90 ya kura zote, upo hapo??
Inaweza kuwa mbaya zaidi ya uchakachuzi wa JK 2010.

Sijui na hili tutalifumbia macho au ndio tutakuwa kama ivory coast?

Nina hamu sana ya uchaguzi mkuu 2015, Mungu tusaidie taifa lako teule na changa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…