Exposure unaipata sehemu yoyote ile as long un smartphone na bando

Masikio Masikio

JF-Expert Member
Apr 12, 2023
1,840
3,378
Bado kuna watu wanaamini ili uwe na exposure lazima uende abroad kwa dunia ya science na technologia unahitaji tu simu yako ya smartphone na bando utajifunza jambo ambalo unalitaka

Sikatazi watu kwenda abroad kama umepata nafasi ni vizuri ila kama hujapata wekeza mda wako kwenye kuperuzi mambo ya msingi utajifunza mambo mengi sana

Kuna watu kupitia tutorial wamejifunza mambo mengi sana

Kama unakiu ya kujifunza jambo flani hutatafuta visingizio kwamba hulijui kwa sababu hujaenda nje kwenye dunia ya science na technologia, ni mambo machache sana ambayo yanakulazimu uende abroad kuyasoma
 
Lingine ni kua usilinganishe real experience na browsing ya smartphone,
Hao ambao wanaenda kupata real experience mbona wakirudi hakuna cha maana wanachofanya

Nenda vyuon wengi wa waadhiri wamesoma phd abroad lakin wakirudi wanakua machawa wa wanasiasa na wanakua hawana tofauti na mtu ambaye hata nje hajawahi kwenda
 
Son, ili uwe na exposure unatakiwa utembee in person,..... huku mitandaoni utapata references tu ya uliyoyaona kwa macho, sikia kwa masikio, feel kwa ngozi, smell kwa pua na taste kwa ulimi.

Dunia ina harufu tofauti, shombo la Dar haliwezi fanana na la Mombasa....hali kadhalika Hali ya hewa ya NYC
 
Nimeongelea watu ambao hawana uwezo ebu soma uzi na uelewe
Alafu mimi naongelea exposure ya kujifunza na sio kwenda kushangaa magorofa
 
Nikuhakikishie kabisa kwamba kwenda nchi fulani ni tofauti kabisa na kusikia habari zake kwa watu au mitandaoni kuna mambo mengi sana huwezi kuyafahamu
Hamna chochote ni yale yale kama mshamba hata uende wapi unabaki vile vile .
.Wachina wanaiba teknolojia kwa kutumiwa picha ya kitu au sample ,then wanafanya manuva fasta.

Bongo ukienda nje huwezi kuwa na exposure kwa ndio kwanza unaanza kushangaa magari.

Kuna madogo walikuwa wanasome shule fulani ya kulipia wanaenda mpaka nje jamaa wangu ni mwanae hapa ofisi ,walienda Marekani wakazungushwa sehemu mbali mbali mpaka kweny viwanda vikubwa ,sehemu nyingine kweny migahawa mda wa kula na kurdi hotelini mda wa kupumzika.

Mwisho wa siku dogo anaulizw na baba ake alivyojifunza huko Marekani anataja mahotel mara vyakula ila amesahau walienda kusoma kuhusu manufacturing industries kama topic...
 
Hio ndo point na lengo la uzi naongelea exposure ya kujifunza kitu na sio kwenda kushangaa mazingira au magorofa au kuja kuturingishia mapicha
 
Son, ili uwe na exposure unatakiwa utembee in person,..... huku mitandaoni utapata references tu ya uliyoyaona kwa macho, sikia kwa masikio, feel kwa ngozi, smell kwa pua na taste kwa ulimi.

Dunia ina harufu tofauti, shombo la Dar haliwezi fanana na la Mombasa....hali kadhalika Hali ya hewa ya NYC
tatizo linaanzia hapa, 'exposure' ina maana nyingi

kama ni kujua vitu mbalimbali kama teknolojia, biashara unaweza kupitia mitandao

kama ni ile ya 'nimeishi USA, ujerumani, ufaransa, nimefanya kazi na wazungu' ile ya kujidai, basi lazima usafiri
 
Mimi siongelei ya kujidai bali ile ya kujifunza vitu
 
Back
Top Bottom