Export business - From Tanzania to the world

Jero_pesa

Member
Dec 28, 2020
14
17
Heshima kwa wapambanaji wote!

Itoshe kusema itifaki imezingatiwa, na kwa heshima kubwa, napanda jukwaani nikilenga kujadili hili jambo la Export business!

Kwanza, hapana shaka kwamba Tanzania & East Africa na Africa kwa ujumla ni sehemu ambazo zimepata upendeleo sana katika raslimali ardhi na hali ya hewa inayoruhusu uoteshaji na ukuzaji wa mazao mbalimbali.

Turejelee pia kwamba, tafiti zinaonesha ya kwamba, kwa raslimali ardhi ya Afrika, inatosheleza kulisha dunia nzima kwa muda wa mwaka mmoja endapo zimetumika ipaswavyo; -
Tusiende mbali sana, tafiti pia zinaonesha kwamba, Tanzania inauwezo wa kulisha Africa mashariki na kati kwa mwaka mmoja pasipo mtu kulala njaa.

Hebu turejelee kwa hali halisi,
Tanzania inaImport almost kila kitu;-
1. Tunaagiza ngano,
2. Tunaagiza mafuta ya kula (mawese)
3. Tunaagiza shayiri (raw materials for bear)
And the list goes on.

WaTanzania tunakwama wapi? Vijana tuko wapi? Tunasubiri ghalika lishuke ndo tujue kwamba kuna fursa kama hizi?

Anyway..... Ngoja tuendelee na mada,

Katika kipaombele kikubwa kinachopewa uzito na uhitaji wa hali ya juu kwa nchi za ulaya, urusi na marekani ni upatikanaji wa organic products (bidhaa /mazao yasiyotumia kemikali) yaani health products!!

Je, ni kwamba sisi watanzania hatuwezi zalisha na kuwauzia hawa watu? Nini kinatukwamisha, je ni uvivu? Je ni kukosa mitaji? Je ni taratibu na sera za serikali?

Najua kuna wajuzi na watalaam wa mambo haya kwa hali ya juu sana hapa JF. Naomba niwasilishe thread kwa kukaribisha mjadala na kuibua mawazo juu ya Export business, especially katika mazao ya kilimo na mifugo.

Salute!
 
Katika kipaombele kikubwa kinachopewa uzito na uhitaji wa hali ya juu kwa nchi za ulaya, urusi na marekani ni upatikanaji wa organic products (bidhaa /mazao yasiyotumia kemikali) yaani health products!!
Hapa inaonesha Ushajua need ya huko Duniani, Russia nk
Je, ni kwamba sisi watanzania hatuwezi zalisha na kuwauzia hawa watu? Nini kinatukwamisha, je ni uvivu? Je ni kukosa mitaji? Je ni taratibu na sera za serikali?

Kinatochotukwamisha ni kushinda tunajadili vitu bila kuvifanyia kazi, Hao Watu unaotaka wakujibu unahisi wanafanya hivo vitu?

Kwanini wewe usiwe sehemu ya Mfano kwa kufanya Maamuzi ya Kuanza leo, kisha kesho uje ushauri wengine kutokana na Uzoefu utakaoupata?

Najua kuna wajuzi na watalaam wa mambo haya kwa hali ya juu sana hapa JF. Naomba niwasilishe thread kwa kukaribisha mjadala na kuibua mawazo juu ya Export business, especially katika mazao ya kilimo na mifugo

Hapa pia unaonesha kabisa Ushajua Kuna uhitaji wa hizi bidhaa ila unatafuta mtu atayekupa go ahead ya kufanya mambo yako

Hilo ndilo linatukwamisha
 
Hapa inaonesha Ushajua need ya huko Duniani, Russia nk

Kinatochotukwamisha ni kushinda tunajadili vitu bila kuvifanyia kazi, Hao Watu unaotaka wakujibu unahisi wanafanya hivo vitu?

Kwanini wewe usiwe sehemu ya Mfano kwa kufanya Maamuzi ya Kuanza leo, kisha kesho uje ushauri wengine kutokana na Uzoefu utakaoupata?

Hapa pia unaonesha kabisa Ushajua Kuna uhitaji wa hizi bidhaa ila unatafuta mtu atayekupa go ahead ya kufanya mambo yako

Hilo ndilo linatukwamisha
Safi sana mkuu, nina kila sababu ya kukushukuru sana kwa jibu lako makini.

Lakini kwa mstakabali wa uzi, sipo na nia ya kuDisclose taarifa za mtu binafsi, either taarifa zangu ama mtu yeyote kwamba anaExport hizi bidhaa.

Hata hivyo, lengo kuu ni kuleta mjadala wa suala hili katika jamii ya kiTanzania ambayo bado hatuna mwamko kuhusu fursa zilizo nje ya milango yetu, ambapo nina imani kabisa ni jambo ambalo litaweza kufumbua macho watu wengi zaidi nchini.
 
Hapa inaonesha Ushajua need ya huko Duniani, Russia nk

Kinatochotukwamisha ni kushinda tunajadili vitu bila kuvifanyia kazi, Hao Watu unaotaka wakujibu unahisi wanafanya hivo vitu?

Kwanini wewe usiwe sehemu ya Mfano kwa kufanya Maamuzi ya Kuanza leo, kisha kesho uje ushauri wengine kutokana na Uzoefu utakaoupata?

Hapa pia unaonesha kabisa Ushajua Kuna uhitaji wa hizi bidhaa ila unatafuta mtu atayekupa go ahead ya kufanya mambo yako

Hilo ndilo linatukwamisha
Safi sana mkuu, nina kila sababu ya kukushukuru sana kwa jibu lako makini.

Lakini kwa mstakabali wa uzi, sipo na nia yabkuDisclose taarifa za mtu binafsi, either taarifa zangu ama mtu yeyote kwamba anaExport hizi bidhaa.

Hata hivyo, lengo kuu ni kuleta mjadala wa suala hili katika jamii ya kiTanzania ambayo bado hatuna mwamko kuhusu fursa zilizo nje ya milango yetu, ambapo nina imani kabisa lotaweza kufumbua macho watu wengi zaidi nchini.
Ngoja waje kutoa muongozo...

Cc: mahondaw
Naam, waite na wengine mkuu.
 
Back
Top Bottom