Exclusive: Uhuni wa CCM uchaguzi Serikali za Mitaa huu hapa

Elli Mshana

Verified Member
Mar 17, 2008
40,134
2,000
MKAKATI WA MSIMAMIZI MSAIDIZI KUMHUJUMU MGOMBEA WA CHADEMA KITONGOJI CHA STOONI ULIANZISHWA MAPEMA.

Mkakati wa Msimamizi Msaidizi wa Kijiji Cha Nyangoto Kata ya Matongo kuhusu uchaguzi kwenye kituo cha stooni ulianzishwa mapema.

Kitongoji cha stooni kilichokuwa kinagombewa na mgombea wa Chadema ndug. ALEX CHACHA BEGA na mgombea wa CCM ndug. SAIMON AUGUSTINO MAGURI ulianzia tarehe 8/10/2019 ambapo mgombea wa Chadema yeye kwa kusimamia kwake binafsi alisimamia zoezi la uandikishaji lililoanza tarehe 8/10/2019 mwenyewe akiwa kama wakala kwa siku zote alibaki kwenye kituo. Mgombea wa chama cha mapindizi ndugu SAIMON AUGUSTINO MAGURI alisimamiwa na mtoto wake STANLEY SAIMON, kilichofatia ni hichi mgombea wa Chadema alikuwa anajitambua na anafahamu utaratibu, alijiandikisha kama kawaida kwenye kituo chake kumbe msimamizi msaidizi ambaye amefahamika kwa jina moja Mwl. HENRY alikuwa na mkakati wa badae ambao mgombea wa Chadema hakuujua kwamba kazi ya wasimamizi ni pamoja na kuhujumu uchaguzi.

Wakakubaliana kuwa huyu hatagombea tutamwandikisha jina tena kwa mara nyingine.
Baada ya muda mgombea wa Chadema kuenguliwa pamoja na sababu nyingine kuwa ameshindwa kutambua anapoishi na kwamba amejiandikisha zaidi ya kituo kioja. Yeye alipinga kuwa hakujiandikisha mara mbili kwa sababu alikuwa ni wakala na alijiandikisha kwenye kituo kile kile cha uwakala wake lakini imejulikana kwa ushahidi baada ya aliyekuwa akiandikisha kwenye kituo cha stooni kuagizwa na msimamizi msaidizi kuomba malipo yake baada ya kufanikisha zoezi la kumhujumu mgombea wa Chadema na ushahidi upo. Je? serikali iliweka watu mapema ili waharibu uchaguzi?.

Lakini Mungu hamtupi mja wake leo tarehe 12/11/2019 ALEX CHACHA BEGA amepokea simu kutoka kwa aliyekuwa mwandikishaji wa daftari la mpiga kura kitongoji cha stooni mwenyewe namba za simu 0743xxx169. Simu ilitakiwa kwenda kwa aliyekuwa wakala wa CCM kipindi cha uandikishaji kitongoji cha stooni ambaye ni mtoto wa mgombea wa kitongoji cha hicho ndug. SAIMON AUGUSTINO MAGURI kwatiketi ya CCM akiwa anadai malipo kwa niamba ya msimamizi msaidizi.

Dah Audio zimegoma ku-upload
 

Kawe Alumni

JF-Expert Member
Mar 20, 2019
8,700
2,000
Wapinzani hawakutumia busara kujitoa Wamekosea sana

Wafikirie kabla ya kufanya maamuzi ya pupa
 

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
2,479
2,000
Mwl Joyce alikua muandikisha Kitongoji cha Stooni Nyamongo, alimpigia wakala wa uandikishaji simu kimakosa akifiri amempigia wa CCM, alikua anaomba rushwa kwa wakala ambae baadae ndio alikua awe mgombea wa Kitongoji mwalimu Joyce alikuwa anasema ametumwa na msimamizi wa uchaguzi anaeitwa Henry eti kwa sababu wamefanikiwa kumuondoa mgombea wa CHADEMA kwa kumuandikisha mara mbili.
 

Attachments

 • File size
  2.7 MB
  Views
  1
 • File size
  900.6 KB
  Views
  1

mwananyaso

JF-Expert Member
Feb 19, 2017
2,116
2,000
Mavi
Mwl Joyce alikua muandikisha Kitongoji cha Stooni Nyamongo, alimpigia wakala wa uandikishaji simu kimakosa akifiri amempigia wa CCM, alikua anaomba rushwa kwa wakala ambae baadae ndio alikua awe mgombea wa Kitongoji mwalimu Joyce alikuwa anasema ametumwa na msimamizi wa uchaguzi anaeitwa Henry eti kwa sababu wamefanikiwa kumuondoa mgombea wa CHADEMA kwa kumuandikisha mara mbili.
 

Boniphace Kichonge

JF-Expert Member
Jul 31, 2017
1,607
2,000
Utii wa Sheria Bila Shuruti

====
Polisi Wilayani Hai, wamemtia mbaroni mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya hiyo, Helga Mchomvu kwa amri ya Mkuu wa Wilaya, Lengai Ole Sabaya ambaye amemtaka pia Mbunge wa Arusha mjini, Godbless Lema kujisalimisha.

Taarifa zaidi zinafuata
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom