Exclusive: Red Cross yapongezwa kwa "Red Alert" | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Exclusive: Red Cross yapongezwa kwa "Red Alert"

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mzee Mwanakijiji, Jan 29, 2010.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Jan 29, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,364
  Likes Received: 6,396
  Trophy Points: 280
  Watu mbalimbali walikuwa wakichangia jana kwenye kampeni ya kuchangia Mfuko wa Vodacom (Vodacom Foundation) ili uweze kusaidia wahanga wa mafuriko yanayoendelea nchini walijikuta wakifurahia kwa kadiri kampeni inavyoenda vizuri. Katika furaha yao hiyo baadhi ya watu walipiga simu Shirika la Msalaba Mwekundu (Red Cross) kuwapongeza kuwa kampeni inaenda vizuri.

  Hata hivyo, Red Cross ilishindwa kupokea pongezi hizo kwani kampeni ya Red Alert ilikuwa si ya kuchangia Chama cha Msalaba Mwekundu (Red Cross) kama ilivyokuwa inadhaniwa.

  Mmoja wa wachangiaji ambaye alifuatiliwa nami aliamini kwa alikuwa anachangia Chama cha Msalaba Mwekundu kwanza kwa sababu, nilikuwepo na kuzungumza na kipindi cha Power Breakfast wiki karibu mbili zilizopita kuhamasisha watu kuchangia Chama cha Msalaba Mwekundu na walijua kuwa kampeni ya Red Alert iliyokuwa inaendeshwa kuanzia kipindi hicho hicho ilikuwa ni sehemu ya kamepeni ile ile.

  "Labda hata rangi zimetuchanganya kidogo, kampeni zote mbili zinatumia rangi zile zile yaani nyekundu na nyeupe" ameniambia Dada Stella.. X wa Mikocheni.

  Haijulikani hata hivyo kama VodaCom Foundation itatoa sehemu ya mapato yake hayo kwa Chama cha Msalaba Mwekundu ili kuzidi kukiwezesha.

  Kampeni yetu ya kusaidia Chama cha Msalaba Mwekundu bado inaendelea wakati ile ya Red Alert inatarajiwa kukoma mwisho wa wiki hii.

  Ukitaka kuchangia Chama cha Msalaba Mwekundu tuma neno "TPN" kwenda namba "15522". Utakatwa shs 250 kujiandikisha na shilingi 150 kwa siku thelathini, sawa na sh 4500.

  Sehemu ya pili ya michango yetu inatarajiwa kukabidhiwa kwa Red Cross Jumamosi hii.

  Pamoja tunaweza.
   
 2. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #2
  Jan 29, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,364
  Likes Received: 6,396
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
   
 3. Sanctus Mtsimbe

  Sanctus Mtsimbe Tanzanite Member

  #3
  Jan 29, 2010
  Joined: Jul 14, 2008
  Messages: 1,815
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Hongera sana Mwanakijiji;

  Hakika umeonyesha njia kwa vitendo kwa kuchangia . . . .

  Mengine ya kuchanganya Kampeni . . . No comment kwa sasa.

  Ninachofurahi ni kuwa tumeweza kutoa changamoto na uongozi kuwa tuzinduke sasa na kuendesha mambo yetu wenyewe. Hakika hilo sasa linafanyika tofauti na ilivyokuwa mwanzo.

  Pamoja tunaweza.
   
 4. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #4
  Jan 29, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  1. Duu hizo laki moja na ishirini ni fedha za Kitanzania au US dollars na kama ni fedha za kitanzania mbona ndogo kiasi hicho yaani mwanaharakati kama wewe unachangia laki moja na ishirini...give me a break..

  2.Mbona kila siku mnaongeza siku mara ijumaa.mara jumamosi ndio round ya pili kesho mtatuambia mtapeleka jumatatu ijayo..tupe sababu za kusogeza siku am sorry sijajua why mmepeleka mbele.
   
 5. Sanctus Mtsimbe

  Sanctus Mtsimbe Tanzanite Member

  #5
  Jan 29, 2010
  Joined: Jul 14, 2008
  Messages: 1,815
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  GS;

  Katika kupokea misaada Red Cross wana utaratibu wao. Ni lazima misaada ipokelewe kwa uwazi tena na Senior Officials. Last Friday baadhi walikuwa wako Field na wengine Bagamoyo kikazi.

  This week, tumekubaliana tufanye Jumamosi mchana ingaswa upande wetu tulipanga Ijumaa.

  GS: Just curious, wewe umechangia kiasi gani kama hujali kusema?
   
 6. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #6
  Jan 29, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Asante kwa maelzo mazuri...nimekuelewa..

  Sidhani kama ni vyema nikataja mchango wangu.
   
 7. Nsiande

  Nsiande JF-Expert Member

  #7
  Jan 29, 2010
  Joined: Jul 27, 2009
  Messages: 1,649
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  tehe mimi pia nimechangia...
   
 8. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #8
  Jan 29, 2010
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,657
  Likes Received: 35,418
  Trophy Points: 280
  I don't get this....changia uende zako.....
   
 9. Mchaga

  Mchaga JF-Expert Member

  #9
  Jan 29, 2010
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 1,371
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  ?????????
   
 10. Mchaga

  Mchaga JF-Expert Member

  #10
  Jan 29, 2010
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 1,371
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  !!!!!!!!
   
 11. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #11
  Jan 29, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,364
  Likes Received: 6,396
  Trophy Points: 280
  kwani miye Vodacom ndugu yangu; kidogo nilichonacho ndiyo hicho. Wakitokea Wabongo wengine 1000 tu tukachanga hizo laki moja na ishirini kila mmoja guess what? So.. mtu yeyote anayeona ni kidogo animatch au anipiku kusaidia Red Cross.
   
 12. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #12
  Jan 29, 2010
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 867
  Trophy Points: 280
  Wiki iliyopita nilikuwa mmoja wa waongozaji wa harakati za kukusanya michango kwa ajili ya kusaidia Haiti kwa niaba ya jumuia ya wanafunzi wenye asili ya kiafrika katika chuo chetu. Mwanzoni nilikuwa dissapointed nilipoona bosi wangu anatoa $20, lakini kadri kampeini ilivyozidi kuenda, nikajikuta ninapokea kiasi hicho hicho na chini yake; ni wachache sana (<10) waliotoa michango ya kufikia dola $50 katika harakati ile. Hata hivyo watu waliojitolea michango walikuwa ni wengi sana kiasi kuwa mwisho wa wiki tulipofunga mahesabu yetu tukawa tumeshakusanya kiasi cha $14,000 na ushee ambazo zilizidi kabisa lengo letu la kukusanya $10,000.

  Nimejifunza moja kuwa hata kwenye hili la kwetu, kama watu wote wakijituma na kutoa kidogo kidogo walicho nacho, tutaweza kufanikiwa na kuwasaidia ndugu zetu kwa ufanisi zaidi. Tatizo letu ni kuwa kuna watu wanapiga domo tu bila kutoa chochote, na wengine wanadhani kuwa ni aibu kutoa kidogo walicho nacho wakidhani kuwa watadharuliwa. Post hii niliyonukuu hapo juu inaonyesha mawazo ya baadhi yetu katika uchangiaji huu.
   
 13. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #13
  Jan 29, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,364
  Likes Received: 6,396
  Trophy Points: 280
  mwalimu ndiyo maana sisi tumefikiria kuchanga 4500 kwa mwezi; hata hivyo tutaona itakavyokuwa, kuna vya kushangaza next week.
   
 14. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #14
  Jan 29, 2010
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,343
  Likes Received: 1,810
  Trophy Points: 280
  Michango hii imetuonyesha njia. wengi tumezoea ile ya harusi na kitchen party. Mambo makubwa yanataka kujipanga na katika kyatekeleza kuna makosa ya hapa na pale yatatokea. Kubwa ni kuwa tayari kuzitumia learning tunazopata kujitahidi kufanya vema zaidi siku za usoni. Hii ni Tanzania yetu. Kama hatuijali, siyo Ghadafi wala mtu awaye yote ataweza kuichukulia serious. Ni sisi wenyewe kwa umoja wetu
   
 15. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #15
  Jan 30, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Shukrani Mkuu...nimekupata ile mbaya....Hongera kwa harakati nzuri huko Haiti.
   
Loading...