Mwanakijiji
nimesoma hii thread mara mbili lakini bado najaribu kujiuliza sababu zilizokusukuma kutumia neno Taifa lisilokuwa na shukrani.
Moja ya matatizo makubwa tuliyo nayo nchini kwetu ni hili la watu kutokuwa na integrity.
Watu wanajifanya kwamba wako victims of circumstances, kwamba kuna natural forces zilizo kubwa kuliko wao, kuna mabosi wamewataka wasaini mikataba na hawakuweza kukataa, kuna nidhamu ya kijeshi isiyoruhusu maswali ambayo iliwataka warushe hizi ndege na wasingeweza kukataa.
Guess what? This notion is wrong.
Ni kweli mwanajeshi hatakiwi kukataa amri, lakini si kweli kwamba mwanajeshi mwenye integrity hawezi kujiuzulu kazi yake, even at the risk of being court marshalled, kama anaona analazimishwa kufanya kitu against his will/ sense of integrity.Ndiyo maana hata utetezi wa the Nuremberg trials kwamba "sisi tulikuwa foot soldiers tu, tulipokea maagizo kutoka juu" haiwezi kusimama leo.
Mimi naendelea ku maintain, kwa mtu mwenye ushujaa hasa na integrity ya hali ya juu hawezi kukubali kurusha hizi ndege kwani ni hatari, na kama jeshi halina ndege nyingine ataondoka kwenda kutafuta kazi kwingine, na ikibidi anakuwa hata whistleblower kueleza uchakavu huu wa ndege.
Tunahitaji whistleblowers zaidi, tunahitaji watu wenye integrity zaidi, tunahitaji watu ambao hawaogopi kusema ukweli kwa kufikiri kitumbua kitaingia mchanga au kibarua kitaota nyasi, tunahitaji watu wanaoweza kumwambia hata rais, rais sijui kama nikikuambia ukweli kazi yangu nitakuwa nayo kesho, au sijui kama nitakuwa huru, lakini ukweli ni huu, ndege zetu mbovu na ni hatari kwa wananchi na wanajeshi wetu, na mimi siwezi kurusha ndege hizi.
Hili ni tatizo si katika swala hili tu, hili tatizo partly ndilo linalosababisha mikataba mibovu, watu wanategeana, bosi anaamrisha rushwa kwa kutegea wa chini yake wakubali hivyo yeye asiwe na sole responsibility, wa chini wanakubali kwa kutegea kwamba ni amri ya bosi na hawana jinsi.
Guess what, ukishazaliwa binadamu tu ushakuwa na jinsi.Hata hao wanyama mwitu wengine tumeshindwa kuwa domesticate widely, itakuwa sisi binadamu?
Kusema kwamba hawana jinsi, wamepewa amri kutoka juu, nidhamu ya kijeshi hairuhusu dissent etc ni kutukana intelligence zao.Hawa watu wanarusha ndege, they can't be that stupid.
Mwanakijiji
nimesoma hii thread mara mbili lakini bado najaribu kujiuliza sababu zilizokusukuma kutumia neno Taifa lisilokuwa na shukrani.
Hiyo ndege nadhani ni Shenyang J-5 ya Kichina ambayo inafanana sana na Mig 17 ya Kirusi..Mwaka gani?... utachoka google hizo ndege kisha mnambie wenyewe ni aibu tupu..inasikitisha kuona bado tuko nyuma kiasi hiki..
Mkuu, sasa kama tunazo hizo Mig 29, hii ndege ilikuwa angani ili iweje?..Kihsa unajua wazungu huwa hawafichi uwezo wa jeshi la nchi fulani kwa sababu contract za kununua ndege za kivita mara nyingi huwa wazi kwa sababu ya kisheria na malipo..Sioni kabisa mahala wanatupa nguvu ya kununua hizo Mig 29...Na sidhani kama tumezinunua kisiri hali vifaa vingine vya kivita tulokuwa navyo vinaonyeshwa wazi. Au Mig za Kichina? haaa! haaa! haaa!