Exclusive: Picha ya ndege yetu iliyoanguka na Taifa lisilo na shukrani! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Exclusive: Picha ya ndege yetu iliyoanguka na Taifa lisilo na shukrani!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Jul 1, 2010.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Jul 1, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  [​IMG]

  [​IMG]

  VIDEO YA KUAGWA MASHUJAA

  Na. M. M. Mwanakijiji

  Sikutaka kutoa maoni yoyote kwa siku kadhaa nione kama watawala wetu wanatambua kuwa vifo vya wanajeshi wetu wakiwa kazini ni kitendo cha kishujaa wakati wote. Kinachoniudhi kuwa tunaishi bila kutambua mashujaa; yaani wale wanaojitoa maisha yao ili kuokoa wenzao.

  Alipokufa yule mwanamama mjeshi kwenye ile ajali nyingine ya ndege ni watu jeshini zaidi waliona kitendo hicho ni cha kishujaa na labda mimi ni mtu pekee niliyeandika kutambua damu hiyo ya binti wa kitanzania ikimwagika. Nikiwa na ndugu waliolitumikia JWTZ kwa uadilifu na wengine kumwaga damu katika utumishi najikuta kila wakati ninasisima ninaposikia vitu kama hivi vinatokea.

  Habari hii ilivyoripotiwa imeripotiwa pasipo kuelewa kwa njia rahisi tu kuwa Rubani Meja Cuthbert Leguna na Luteni Andrew Kijangwa waliamua kufanya kitu cha kujitoa mhanga kwa kukwepesha ndege hiyo kuangukia makazi ya watu na kujaribu kutua barabarani. Na hata hapo barabarani walipoona kuna basi la Simba Mtoto na gari la Watalii huku ndege yao ikienda kuanguka walijitahidi kulikwepesha na katika kufanya hivyo wao pekee ndio wamekufa katika tukio hilo la kusikitisha lakini lenye kila chembe ya ushujaa.

  Taifa lisilo na shukrani linachukulia tu kuwa ni ajali na "ajali haina kinga" kumbe wapiganaji wetu wamekinga ajali kubwa zaidi kwani leo tungekuwa na kilio kikubwa zaidi. Sijui kama Rais wenu, waziri mkuu wenu, au hata wabunge wenu wameonesha shukrani yoyote Bungeni au mahali pengine popote kwa kitendo hiki cha kishujaa. Yaani, waliona ni bora wao wawili wafe kuliko makumi au mamia kuangamia!

  Nikiwa nimelengwa na machozi na nikitambua uzalendo huu wa hawa vijana wapiganaji ambao licha kupoteza ndugu, baba, kaka na watoto katika familia zao wamepoteza vile vile hazina kubwa ya ujuzi na utaalamu katika Jeshi letu, utaalamu ambao taifa linatumia kiasi kikubwa sana kupata. Wakati ndege ni rahisi kununua (wakiacha ufisadi kidogo) maisha yao na uzoefu wa ujuzi wao hauwezi kurudishwa kamwe.

  Ninatoa shukrani kutoka familia moja ya kijeshi kwenda familia nyingine, Ninawapigia saluti wapiganaji hawa na kusema asante kwa kitendo chao cha kizalendo na kishujaa kupita kiasi. Wakati mafisadi wenu wanaendelea kutanua na kubishana nani ale nini zaidi hapa leo wanalala mautini wale ambao labda hata baada ya siku chache hawatakumbukwa, familia zao zitarudishwa kijijini, watoto wao watakosa elimu n.k n.k Laiti tungejua kusema asante kwa kafara hii ya utumishi.

  Asante Meja Leguna
  Asante Luteni Kijangwa

  Majina yenu yatabakia moyoni..

  Mungu Ibariki Afrika
  Mungu Ibariki Tanzania

  Mlale salama enyi wana wa Tanzania, mlale salama mashujaa!!


  Saluti!
   

  Attached Files:

  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 2. Bantugbro

  Bantugbro JF-Expert Member

  #2
  Jul 1, 2010
  Joined: Feb 22, 2009
  Messages: 2,684
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Saluti:humble:
   
 3. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #3
  Jul 1, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,194
  Trophy Points: 280
  May all beings attain enlightenment.

  Hivi JK hajasema "kazi ya mungu" tu bado? Najua kuna swala la usalama hapa linaloweza kufanya hata transparency yetu ndogo isiwepo kabisa, lakini hili halinizuii kuuliza, hivi hii midege inafanyiwa ukarafati unaotakiwa? Standard zetu za usalama zikoje?
   
 4. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #4
  Jul 1, 2010
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Jamani msiba huu umenigusa sana nilikuwa JKT Makutupola 92-93 Operation vyama vingi na Meja Cuthbert Leguna Kombania moja. Wengine tuliamua kwenda chuo kikuu baada ya kutumikia Jeshi. Huyu jamaa yangu aliamua kubaki jeshini na kupelekwa kusomea nyota Monduli (Officer cadet). Baadaye alipelekwa kusomea urubani China. Carthbert alipangiwa kazi ya ukufunzi wa marubani kwenye Kambi ya jeshi Ngere Ngere (Kizuka). Muda mwingi nikiwa Tanzania tumekuwa karibu kwenye masuala ya kijamii na burudani. Cuthbert kijana wa kigogo, Mtanzania aliipenda kazi yake. Daima nitakukumbuka kwa uchangamfu wako na ukarimu. Pole sana kwa familia na ndugu na marafiki wote, watoto na mama mjane.

  RIP Cathbert Leguna

  Masa K
   
 5. Maverick

  Maverick JF-Expert Member

  #5
  Jul 1, 2010
  Joined: May 29, 2008
  Messages: 308
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mkuu hapa umenena!. Sina cha kuongeza!
   
 6. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #6
  Jul 1, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280

  kwenye masuala ya ndege za kijeshi, hatuna tatizo kwa kweli. Tuna timu ya mainjinia wa kijeshi, na vifaa constantly kutoka China. Toka zamani sana kumekuwa na Wachina wakiservicia na kutrain wapiganaji wetu pale Kipawa, Kange (kambi ya Ulinzi wa Anga) na hasa Ngerengere ambapo ni center yetu ya aerial defence. Ila kitu kimoja ni kuwa bado hatujafanya a major upgrade of our military aircrafts kwa muda sasa. Japo sources zangu ndani ya jeshi zinadokeza kuna major military purchase inakuja ambayo itahusisha pia ndege za kisasa kutoka Uchina - Wachina ndio wana mkataba mkubwa wa mambo ya kijeshi kwa muda mrefu.
   
 7. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #7
  Jul 1, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,194
  Trophy Points: 280
  Wachina ni kati ya watu wanaoongoza kwa utamaduni wa kutokuwa na Quality Assurance, kwa hiyo the fact kwamba tunafanya kazi na wachina halinipi confidence kabisa. Sijui kama huu utamaduni wao unabadilika jeshini, lakini sina sababu yoyote ya kutegemea hilo. Na kitu ninachoshangaa ni kwa nini hatusikii ajali kama hizi zaidi, sio kwa sababu naombea iwe hivyo, bali kwa sababu inaonekana hatuna ukarafati wa kutosha, na hata walimu wetu ni watu wanaojulikana kwa ku cut corners.
   
 8. Q

  Qadhi JF-Expert Member

  #8
  Jul 1, 2010
  Joined: Oct 27, 2009
  Messages: 235
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Saluti..Tunatambua na kuheshimu mchango wenu katika taifa letu la Tanzania,pole sana wafiwa.

  Mkuu Mwanakijiji,ningependa kujifunza technolojia iliyotumika kujua kwamba hawa wapiganaji wetu walifanya hizo jitihada za hali ya juu sana kuokoa maisha ya raia( kama ambavyo waliapa kwamba watalinda mipaka ya nchi na usalama wa raia).... au ......walikuwa wanawasiliana na wenzao somewhere?
   
 9. BabaDesi

  BabaDesi JF-Expert Member

  #9
  Jul 1, 2010
  Joined: Jun 30, 2007
  Messages: 2,795
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Aina ya hizo ndege kama iliyoko kwenye picha ni vema zikawa phased out. kumbukumbu yangu inaniambia ni za zamani mno. kwa hakika pengine ingefaa ziwe grounded.

  Kuhusu ushujaa wa hawa mapilot kukwepesha janga kwa kukwepa kugonga magari ya abiria inanikumbusha mwaka 1979 wakati wa sherehe rasmi za kuwakaribisha nyumbani wanajeshi waliotoka vitani Uganda kumng'oa Nduli Amin ndege moja ilipata hitilafu wakati ikipita uwanja wa taifa na ikawa inaelekea kuanguka katikati ya uwanja uliojaa watu na wanajeshi na mgeni wa heshima mwalimu Julius Nyerere ambapo nukta chache kabla ya kuanguka kwa ushujaa mkubwa mapiloti wake wawili wakaielekeza ndege hiyo kuanguka nje ya uwanja wa Taifa palipojengwa uwanja mpya na kutoa mshindo mkubwa uliofanya watu kutaharuki na kukimbia ovyo.

  ma-pilot wale ambao nimesahau majina yao walikufa pale pale lakini wakawa wameepusha vifo vya watanzania wengi iwapo ndege ile ingeangukia katikati ya Uwanja taifa.
  Ukajengwa Mnara wa kumbukumbu na watu wakaahidi kwa mbwembwe kuutunza.
  Miaka michache tu baadae mnara ule ukawa hauonekani kutokana na kuzungukwa na kichaka.
  Ningependa kufahamu iwapo mnara ule bado upo na unatunzwa kama watu walivyoahidi ama ulikuwa ni majeruhi wa ujenzi wa uwanja wa kisasa na umebaki hadithi tu ya kuhadithia wajukuu!!
   
 10. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #10
  Jul 1, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  mzee mara ya mwisho kusikia Wachina wamepata matatizo katika vyombo vyao vya kijeshi ni lini? Linapokuja suala la dhana za kijeshi na kivita Wachina are at par with almost all the other military powers of the world. Tatizo lao lipo kwenye mambo ya consumer products ambapo ni sawa kabisa katika udhaifu na vifaa vya Wamarekani! Tatizo vya Wamarekani vinaenda kwa sababu ya jina la nchi zaidi na makampuni.. QA ya Marekani katika consumer products bado iko chini kulinganisha na sehemu nyingine duniani. Inawaridhisha zaidi wamarekani wenyewe kulikow atu wengine.
   
 11. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #11
  Jul 1, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,194
  Trophy Points: 280
  Baba Desi hiyo story ya taifa niliisikia.

  Halafu umeleta a whole new dimension, mimi nilikuwa naongelea ukarafati in general nikaambiwa tuna ukarafati mzuri kwa msaada wa Wachina, kitu ambacho nimeeleza kutoridhishwa nacho. Wachina ndio watupe ukarafati mzuri wakati China maisha ya mtu hayathaminiwi kabisa?

  Lakini wewe umekuja na isue nyingine iliyo juu ya ukarafati kabisa, kwamba kuna midege fulani imeshapitwa na wakati kiasi kwamba hata ukarafati utakuwa ni uzushi tu. There is a reason Dudu Baya aliimba "Dege la Jeshi" na hii phrase kwa ujumla ikawa na maana ya kitu chenye hatari sana.Ndege zetu za jeshi ni za zamani sana.

  I can see the challenge for a poor nation like Tanzania with no immediate military threat amassing state of the art jets, I will be the first to condemn that as extravagant military spending, but at the same time these old aircrafts are too risky, it is safe to go with the thinking that our QA and security standards are very low ( we are taught by the Chinese for god's sake!)

  Zaidi ya hapo, despite genuine security concerns regarding transparency, tungependa kuona a slimmer of transparency, especially on an as needed basis kwa sababu otherwise wanajeshi na wananchi wetu wataendelea kufa kirahisi bila msaada wowote.

  Ingawa kwa taifa masikini ni vigumu ku balance spending na security, hii haimaanishi tusifanye chochote vile vile.
   
 12. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #12
  Jul 1, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  kwa kweli haiitaji teknolojia ya ajabu.. bali uwezo kidogo tu wa kufanya rational deduction kwa kutumia ubongo kwa muda mfupi tu ukiwa na facts mbalimbali at hand.
   
 13. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #13
  Jul 1, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Yeah.. nilikuwa najibu swali la ukaravati ambao binafsi na knowledge yangu kwa muda mrefu najua kuwa wamejitahidi sana.. kumbuka katika ajali za jeshi hii imetokea muda mrefu kweli ukiondoa zile za Bell choppers na kwa upande wa za kiraia kulinganisha na ile ya A320 ambazo zote ni western.

  Lakini, ukweli mwingine ambao unaudokeza na kwangu ni muhimu ni kuwa hatufikirii kwenda na wakati katika masuala ya usalama. Leo hii tunataka kuwa na visima vya mafuta on shore na off shore tena mengi tu, lakini we don't have a credible navy to defend them.. leo hii tunategemea navy ya RSA kulinda maji yetu kwani mitumbwi yetu ya kijeshi haiwezi kwenda kwenye deep water huko.

  Ndio maana utawala wa kifisadi hudumu. Tunahitaji the whole Navy Brigage ya kisasa ambayo angalau ingekuwa na fleet moja ya meli za kivita (na wala hatuhitajia ma aircraft carriers). Lakini hawaoni umuhimu huo. Wanaendelea kulinda utajiri wetu kwa pinde!
   
 14. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #14
  Jul 1, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,194
  Trophy Points: 280
  Mwanakijiji hizo picha ni accurate as far models are concerned? Au ni file pictures tu mradi kuna ndege?

  Maana hiyo moja ya juu inaonekana kama ndege za WWII .
   
 15. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #15
  Jul 1, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280

  hahaha.. hiyo picha ya kwanza ndiyo iliyoanguka, hiyo nyingine iko katika fleet ya ndege zetu sasa hivi.. na ninazo picha nyingine na nafikiri nyingine zilishawekwa hapa. Bado tunatumia ndege nyingi za Mig za zamani. Ndio maana nafikiri mojawapo ya purchases mpya ni kuupgrade ndege zetu kutoka Uchina (maana China wanachukua kutoka kwa Warusi muundo wao). Tumepeleka wanafunzi wengi kidogo Uchina katika mambo haya ya urubani wa kijeshi.. sasa tunahitaji tu vitendea kazi. Kwa sababu nadhani hata Rwanda na Burundi tayari wameshaupgrade baadhi ya ndege zao.
   
 16. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #16
  Jul 1, 2010
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Nilikuwa nimehama kabisa katika hizi jazba za kuandika andika hapa JF ,ila habari kama hizi zinanifanya nijiulize kama kweli mwandishi ni mpiganaji au mwanajeshi aliekomaa kiakili na kisiasa zaidi amenigusa aliposhusha neno la kiuzalendo ,kwamba wajeshi waliofariki walijitahidi kiasi cha uwezo wao kukwepesha ajali kubwa kana kwamba vile nae alikuwa mmoja ya marubani au alikuwemo ndani ya ndege iliyopata ajali na amejaaliwa kupona ,hivyo yale yote yaliojiri ndani ya ndege wakati wapatashika aliyaona live na kuyasikia kwa jinsi alivyohadithia ,labda ameyapata kutokaa black box ,huwezi kujua !

  Kinachoniuma hapa ni kuona kuwa mjeshi huyu alie hai amekasirishwa na kuhuzunishwa sana kiasi ya kuandika mlolongo wa maneno yanayohuzunisha na kuonyesha udhaifu wa serikali na kumfanya msomaji aone hawa ni wa kupigiwa mfano na kuenziwa.
  Hapa inaonyesha kuwa huyu mtu haijui historia ya utawala uliopo madarakani,kwamba wanakutumia na ikifika wakati wanakupiga buti na kukudharau na unakuwa si lolote si chochote pengine ni afadhali ya sikerepu kuliko wewe unaejitutumua kuilinda nchi hii na kuitetea kwa hali na mali na roho.

  Kuna visa vingi vya majeshi kuingia uraiani na kutoa kisago kitakatifu ,wakitumia mikanda mabundi na karate za hapa na pale ,majeshi hawahawa wanatumika katika kuhakikisha CCM na utawala wake unaendelea kubaki madarakani ,jambo ambalo ndio baya kuliko yote yale yanayoweza kuhusishwa na utumiaji mbaya wa vyombo vya umma ,hapa Tanzania bara bado CCM haiojapata upinzani wa kutishia madaraka yao ingawa sehemu zingine zimeanza na polisi tu ndio wanaotumika lakini kule Zanzibar upande wa pili wa Jamhuri yetu majeshi wanatumika kikamilifu wakiwa na zana nzito wakisaidiwa na vifaru kupita mabarabarani wakati wa uchaguzi ili kuteka ushindi .

  Haya ni mambo ya kutumika au kutumiliwa vibaya kwa vyombo vya dola na utawala , utawala usio na fadhila au shukurani NA SIO KAMA mwandishi alivyoandika TAIFA lisilo na shukurani. Hapa anaposema TAIFA ,mimi sikubaliani nae kabisa kabisa na nampinga vikali sana. Nionavyo Utawala usio na shukurani , kwa maana kadiri inavyovitumia vyombo hivi vya dola ,inashindwa kabisa kujumuika nao katika mambo ya misiba inayowakuta waajiriwa hawa.

  Hivyo vyama vya upinzani vinaposema mujiepushe katika kuibeba CCM ,basi muelewe kwa kina kabisa kuwa hii sio nchi ya CCM bali ni nchi yenye vyama vingine vya kisiasa vyenye dhamana sawa sawa na CCM na inabidi vyombo hivi viweke heshima na usawa kwa vyama vyote ili kujenga Taifa lenye utawala bora ,kwa maana hiyo viwe ni vyombo vyenye kufuata sheria za nchi na kujihusisha katika kulinda amani kwa wananchi wote kwa usawa kabisa bila ya kubaguwa kutokana na imani ya watu na chama wanachokipenda.

  Hii ndege iliyoanguka sijui ni aina gani na sijui ina miaka mingapi lakini inaonyesha ni modeli za kizamani sana sana pengine kwenye vita ya pili ya dunia na ni tofauti kabisa na ndege za kileo zinatumika katika ufundishaji wa ndege za kivita ,ilikuwaje kuwaje hadi leo hii bado inarushwa au ndio uhodari wa mapilot wetu.

  Naungana na mtoa habari kuwapa pole wafiwa na kuwa na subira ,vilevile kwa wajeshi wote ambao wameguswa na msiba huu ,yes we lost them na hatuwezi kuwarudisha tena.
   
 17. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #17
  Jul 1, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,194
  Trophy Points: 280
  Not to make light of this sad occassion, but I couldn't help noticing.

  Usikute ndege kama hizi nchi zilizoendelea zinaweza kuwa ziko katika makumbusho ya kijeshi tu na watu hawazirushi, tunaweza kuingia katika Guiness Book of Records kama jeshi la anga lenye kupaisha ndege za zamani.

  Tanzania vipaji vingi tu, lakini mpaka aje mzungu kutushtua.
   
 18. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #18
  Jul 1, 2010
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Mwiba's counter argument shows JF maturity in debates. Great work!
   
 19. Semilong

  Semilong JF-Expert Member

  #19
  Jul 1, 2010
  Joined: Mar 5, 2009
  Messages: 1,711
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  kwani wachina si ndio hao wanaoleta products nzuri ulaya, marekani na dunia kwa ujumla.

  tatizo lipo kwa wafanyabiashara wa TZ ambao wanapenda vitu vibovu ili waje kuviuza na kupata faida mara mbili.
   
 20. BabaDesi

  BabaDesi JF-Expert Member

  #20
  Jul 1, 2010
  Joined: Jun 30, 2007
  Messages: 2,795
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Mkuu Kiranga, una point hapo. Hebu kumbuka mara mwisho picha uliyoona ambayo Jet Fighter iko flat mbele kama hiyo picha hapo juu, flatness ambayo sana sana itapunguza tu spidi ya ndege hiyo, badala ya kuwa sleek na kuishia na 'sindano' mbele. Wajuzi wa kubandika picha bila shaka watatubandikia hapa picha ya Jet Fighter ya kisasa tulinganishe na 'ngwalangwala' letu.
   
Loading...