Watu wengi wamekua wakiuliza swali hili, hasa wale wanaofanya kazi kama waalimu, ambao wanatakiwa kuwa-grade wanafunzi kulingana na matokeo ya mitihani kwa kutumia Microsoft excel.
Nimeona watu wengi wametoa maelekezo kwa kutumia function ya "If" na ndiyo niliyokua naijaribu katika kutatua tatizo hilo lakini baadae nimeona ni ndefu sana, na mahali fulani unaweza kujivuruga wakati wa kupanga mambo. Kwa mfano nilikua naangalia maelekezo ya Kyatsvapi akiwa anajibu swali hilo. Ni njia nzuri na ndiyo niliyokua natumia kwa muda mrefu.
Lakini nilikua nafikiria Kutumia function ya "Vlookup" kupanga points na baadae kutumia function ya "sum" pamoja na ya "small" Kupata divisions.
SASA TWENDE HATUA KWA HATUA.
Kwanza, nina wanafunzi wangu
Na hizo ndo marks zao.
Pili
Mahali fulani kwenye excel yangu natengeneza refference table yangu
Column ya kwanza ni Marks ya pili kama unavoona ni kwamba mark inaangukia kwenye A au B,C nk ya tatu ni points husika.
Tatu
Naenda kwenye cell ambayo nitacopy table ya matokeo na badala ya marks table itaniletea sasa Points kwa kila somo lililo kwenye table ya matokeo.
Namna rahisi ni kwa kutumia alama "=" Naiweka mahali ninapo taka table yangu itokekee,
kisha naclick cell ya juu kushoto ya table yangu
kisha enter
cell niliyochagua itajirudia kwenye point niliyo chagua
Kisha na-drag kwenda kulia kwa kushika dot ya chini ya cell
Mpaka row yote itokee namna hii
halafu naselect tena cell mbili za kushoto kabisa, maana column ya sex itajirudia
Nashika dot kwenye kona ya cells hizo na kudrag chini
Hadi cell za kwenda chini zitokee
Table yangu ipo tayari kwa kujaza points
Hapa ndio tunaanza kuweka mambo ya "Vlookup" na tunaanza na cell yenye marks za Biology za mwanafunzi Chungwa Tamu. pale andika alama ya sawasawa, kisha vlookup kisha fungua mabano =vlookup(
Kisha click Marks za biology za Chungwa Tamu kwenye ile table yenye marks
bonyeza mkato , Kisha select ile table ya refference yote
Bonyeza F4 ili alama za dolar zitokee kwenye hiyo refference, au table array
Bonyeza mkato tena tayari kwa kuweka return value ya table ya refference, ambayo ni column ya value unayotaka irudi. Ka case yetu ni column ya tatu
Kwa hiyo baada ya mkato tunaweka 3
Mkato tena, sasa hapo kuna true na false. True kama ni approximate match, au False kama ni exact match. Lakini kwasababu kenye refference table yetu kutoka 0 hadi 30 kuna namba katikati na zinatakiwa zikadiriwe kuwa ni poit 5 au 4 kwahiyo jibu letu ni True approximate.
Sasa kitu chetu kitaonekana hivi
Hapo gonga enter. Na utaona 1 inatokea ikimaanisha 89 ambayo ni marks ya Chungwa tamu katika Biology, ikipimwa na table yetu inakua ni point 1.
Sasa shika tena kona ya cell hiyo na uivute hadi mwisho
Kisha ushike tena kona hiyo uivute hadi chini
Na kila kitu kitakua kimejaa kwa mwendo wa point.
Wamenikataza nisiongeze picha. Naomba niishie hapa kwanza. Halafu nitaendeleza kwa mwendo sasa wa division na kumalizia kila kitu. Kimsingi maelezo ni mengi sana, lakini unapokuja kwenye uhalisia na kuelewa itakua ni kitu cha dakika chache tu. Pia kuna mambo ya kurahisisha, kwa mfano baada ya kudrag kwa kukatisha, unapotaka kujaza kwa kwenda chini select viboksi vitupu vya chini kisha bonyeza control na D.
Nitaendelea. Baadae nitaleta sample na utaona ni rahisi sana.