Excel kupanga matokeo, divisions na points

Excel kupanga matokeo, divisions na points

Kama kuna paper 1,2 &3
Nataka kama mwanafunzi hajafanya paper mojawapo awe incomplete formula inakuwaje?
 
Kama kuna paper 1,2 &3
Nataka kama mwanafunzi hajafanya paper mojawapo awe incomplete formula inakuwaje?
=IF(G20="", "Incomplete")
G20 ni sehemu ambayo unajaza marks, na hiyo formula utaiandika ktk cell unayotaka hilo neno la incomplete litokee
 
Sehemu za kujaza marks hapo zitakuwa g20,h20 na i20
Angalia hii screen shot, nikitype formula inajikata
IMG_20190412_230912_617.JPG
 
Hiyo iko poa! Ila bado ni manual work mimi nina mfumo (full automatic) kwa ajili ya management ya shule nzima kuanzia udahili kuchakata matokeo (mzazi au mlezi anaweza kuona matokea hayo) , tarifa za walimu (hr na finance ) makusanyo ya ada na n.k kwa maelezo zaidi anayetaka anione pm
weka hapa watu wasome....kama mdau anavofanya...mambo ya pm ya nini?? Tunaendaga pm tukitaka kutongoza
 
Asanteni sana wadau. Nashukuru.
Sasa table yetu ikijaa itafanana namna hii

View attachment 452437

Kwa maelezo kifupi, tuangalie function ya Vlookup, na utaratibu tulio tumia.
Katika utaratibu wetu tumekua na table A, B na C kama ifuatavyo.
(A)Table original, ambayo ina majina ya wanafunzi na Marks zao
(B) Table ya refferences, ambayo ina mgawanyiko wa scores na points kulingana na Marks. Kwa mfano 45 ni alama C na pia ni 3 points.
(C) Table mpya inayotengenezwa, inayoonyesha sasa points kwa kila somo katika table A, kulingana na utaratibu ulio katika table B.

Function ya vlookup yenyewe imegawanyika katika sehemu 4. Sehemu hizo zinaonekana baada ya kuandika "=vlookup(" na sehehemu hizo hutenganishwa kwa alama ya mkato","
Kwa mfano wetu function yetu ilionekana kama hivi "=vlookup(E3,$A$19:$C$24,3,True)
hapa ukitazama kila baada ya mkato utagudua kuwa sehemu hizo ni nne:-

(1)="E3"
ambayo ni cell (kiboksi) katika table A (original) yenye Maksi unayo taka kubadili kuwa Point. Kawaida hii italinganishwa na column ya kwanza kabisa / ya kushoto kabisa, katika selection ya Table B

(2)="$A$19:$C$24
ambayo ni range (mipaka) ya table B (refferences). Kawaida range hiyo ingekuka hivi A19:C24, Lakini alama za dola "$" zinaongezwa ili range ya Table B isisogee wakati unapo drag kujaza cells "vyumba/viboksi" kwenye table ya matokeo (Table C).
Alama hii ya dola huongezwa kirahisi kwa kubonyeza key "F4" unapokua umechagua mipaka ya Table B.

(3)="3"
Kama nilivyo sema awali, ni namba ya column ikihesabiwa kutoka kushoto katika Table B. Kwamba ni katika column ipi (yangapi toka kushoto) ya Table B, utataka kitu kipelekwe kama jibu kwenye Table C, endapo namba uliyochagua kwenye Table A itafanana na yoyote iliyo katika column ya kushoto katika table B. (sijui nimechanganya maneno au imeeleweka?)

4)="True"
Hapa tunatakiwa tujaze "True" au "False". Kwamba namba iliyochaguliwa kwenye Table A inafananaje na namba iliyo katika column ya kushoto ya Table B. Hapa tuna True ambayo ni approximate match na False ambayo ni Exact match",
Kwa kilugha chetu tungesema "ni (TRUE), inayohusiana nayo kiaina au NI (FALSE) kwamba ni yenyewe moja kwa moja". Kama ni inayohisianahusiana nayo tunasema "True", kama ni yenyewe moja kwa moja tunasema "False". Kwa hiyo Maksi 0hadi 29.999, inahusiana na 0, na maksi 31 hadi 44.999 inahusiana na 30. Kama kwa mfano wetu, tungekua tumeweka False, manake namba ambazo zingerudisha majibu toka table A ni zile zenye 0, 30, 45, 65 na 75 tu. Nyingine tofauti na hizo zingeleta error (kosa).

Sasa kwa uelewa huu, Tukirudi kwenye matokeo yetu katika Table C, ambayo tulikua na points. Tukizifuta na kubaki na kiboksi kimoja, cha kwanza juu kushoto,

View attachment 452439

"ilitusipoteze formula yetu" Kwenye formula ya Vlookup tukirekebisha kipengele namba tatu. Badala ya "3"
Tuweke "2"

View attachment 452441
Kisha Enter.
Tukidrag,(kuvuta) kushoto kisha chini.
Matokeo yatakua sasa kwa alama badala ya Points.

View attachment 452442

Naomba tena niishie hapa kwa sasa. Baada ya muda nitarudi na suala la Division.
Mchana mwema.
Mkuu uko njema Sana katika Excel
 
Kwa kutumia vlookup command naona hata kea ambao hawajafanya inawawekea F vipi hapo tunaweza kuhandle vipi situation kama hii
 
Mkuu vipi kwa kutumia vlookup kea data zinazomiss (hamna data katika cell)
Unataka Vlookup idisplay blank kama cell ni empty or? If yes, andika

=IF(VLOOKUP(D6,H8:M20,2,FALSE)="","", VLOOKUP(D6,H8:M20,2,FALSE))
 
  • Thanks
Reactions: a45
Mkuu vipi kwa kutumia vlookup kea data zinazomiss (hamna data katika cell)
Kama ulimaanisha lookup value ndiyo inayomiss,andika

=IFERROR( VLOOKUP(D6,H8:M20,2,FALSE),"")
 
Kwa kutumia vlookup command naona hata kea ambao hawajafanya inawawekea F vipi hapo tunaweza kuhandle vipi situation kama hii
Inakuja F kwasababu, vlookup ikikutana na empty cell (cell zisizojazwa value yoyote) huwa inaitreat kuwa zero (zero ni F ndo mana inadisplay hivyo)
 
  • Thanks
Reactions: a45
Inakuja F kwasababu, vlookup ikikutana na empty cell (cell zisizojazwa value yoyote) huwa inaitreat kuwa zero (zero ni F ndo mana inadisplay hivyo)
Nilikua namaanisha hii uliyo jibu hapa mkuu
 
Back
Top Bottom