Njia ya pili na ambayo itabadilisha points na division ukibadili marks za mwanafunzi.
Sasa kwanza download excel yangu hapo inayoitwa "Mfano Marks" halafu tuelekezane. (Kwa bahati mbaya office yangu ni 2007, pengine tunaweza kupishana kama una version ya mbele).
Utaona ina tabs tatu (Original, Points na Final) Kwenye excel tabs zinaweza kuongezwa na kupewa majina.
View attachment 453675
1. Kwenye Tab ya kwanza, utaona nimeweka table original zenye marks za wanafunzi, pamoja na vi-refference table viwili. Kimoja cha points na kingine cha divisions.
(By the way :- Unaweza pia kuweka kila kitu kwenye tab moja ila kazi itakua pana sana, kama unajua mbinu za kuhide cells inakua vizuri pia)
2. Kwenye tab ya Pili nimetengeneza Table ya vlookup.
Nimefanyaje.
Kwanza nikiwa hapo kwenye "tab" ya "points", nimeclick cell ya kwanza kabisa ambayo ni A1. Nikaweka alama ya swasawa "=". Nikaenda kwenye tab ya Original, nikaclick cell ya A1 ambayo ni "Student name" kisha nika bonyeza enter, Student name ikaja kwenye A1 ya tab ya Points. Nika click cell hiyo na kuivuta kwa kikona kwenda pembeni hadi mwisho. kama 0 zikitokea umepitiliza, zifute.
View attachment 453682
Kisha nika-select Student name na Sex hapohapo, nikazivuta kwenda chini kwa mtindo huo huo.
View attachment 453685
Nikaenda kiboksi cha kwanza juu kushoto C2 kenye tab hiyo hiyo ya Points, nika-click na nikaanza kuandika formula yangu ya vlookup.
Nikaandika hivi
=vlookup( kisha nikaclick tab ya
original, halafu nikaclick
C2 pale original, nikabonyeza
mkato (coma). Baada ya hapo natakiwa niweke table array, nikaselect
table B yote isipokua heading yake, kisha nikaboyeza
F4 kuweka alama ya Dollar, nikabonyeza
mkato tena, halafu nikaandika
3 kwamba ninachotakiwa kupata hapo ni points column ya tatu,
mkato tena, halafu nikaandika
true Nikafunga
mabano. nikapress
enter. Kwenye kiboksi C2 kwenye tab ya points ikaja point. Nikaiselect kisha nikaidrag kushoto kisha chini kama kawaida kujaza viboksi vya points vilivyo baki.
Kisha hapo hapo kwenye tab ya points nikaongeza column za columns za Points na divisions
3.Kwenye divisions nikatumia utaratibu wa
Sum na small kama maelekezo awali.
4. Kwenye division nikaandika vlookup namna hii
Kwanza nikaclick kiboksi cha kwanza ambacho ni M2, kisha nikaandika
=vlookup( kisha nikaclick kiboksi cha nyuma yake ni
L2, nikabonyeza
mkato, kisha nikaclick tab ya
original, nikaselect
table C yote isipokua heading, kisha nikabonyeza
F4 kuweka alama za dola, kisha nikaweka
mkato tena, nikaandika
2 kisha
mkato, nikaandika
true kisha, nikafunga
mabano, kisha nikabonyeza
enter. Division ikaja kwenye kiboksi cha M2 kwenye tab ya points. Nikaishika kwa kona nikaidrag chini kama kawaida kujaza viboksi vyote.
5. Kwenye tab ya
final cell A1, nikaweka alama ya
"=" Kisha nika-click tab ya points, na pale nikaclick cell ya kwanza yaani A1, nikabonyeza
enter, Student name ikaja kwenye cell ya A1 kwenye tab ya final. Nikadrag kushoto, kujaza, kisha nika select student name na Sex, nikadrag chini kama nilivyo fanya awali kwenye tab ya points.
Nikaenda kwenye tab ya points tena. nikaclick cell ya somo ya kwanza juu kushoto, yaani C2. Nika-right click kisha nika-copy. Nikaenda kwenye tab ya final kwenye C2 nika-paste. Ikaja function ya vlookup niliyotumia kwenye tab ya points. Nikaenda kwenye kipengele cha 3 cha function hiyo ya vlookup, nikabadili 3 kuwa 2, kisha nikabonyeza enter. Kwenye kiboksi cha C2 kwenye tab ya final ikaja "A" ambayo ni mark ya mwanafunzi Chungwa Tamu katika somo la Biology.
View attachment 453690
Nika drag kushoto kisha chini kama kawaida kujaza viboksi vyote
6. Kwenye kiboksi cha L2 kwenye tab ya final, ambacho ni points za mwanafunzi Chungwa, nikaweka alama ya sawasawa
"=" , kisha nika-click tab ya points nikaclick pale kiboksi L2, kisha enter. Points za mwanafunzi chungwa zikatokea pia kwenye kiboksi cha L2 kwenye tab ya final. Nikadrag kushoto hadi usawa wa division, kisha nikadrag zote chini hadi mwisho kujaza points na division kwenye tab ya final. Kitu kikawa kimetokea na mabadiliko yoyote ya marks yatakayo fanyika kwenye tab ya original tatatokea kila mahali.
View attachment 453691
Ndefu sana, lakini jaribu kuielewa. Usisahau kudownload excel yenyewe