Ex wangu bana! Mungu amsaidie tuu

Ex wangu bana! Mungu amsaidie tuu

Bado unampend, unampa na ratiba zako za safari na kukutana nae wakati alikuita kafiri. You are not serious ni suala la mda utamrudia tu huna msimamo kaka

Si lazima mtu mkiacha ndo hata kuongea nae huwez.


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Alifanya maamuzi sahihi kutokuolewa na kafiri , naona shetani anamchezea anataka kurudi alipotoka
 
Iko hivi...

Mwaka 2013 nilimaliza Bachelor na kurudi Dar, nilikutana na mtoto mmoja mzuri hatari. Alionekana ana stress kiasi na mzee baba nikajikaza na kuomba namba. Nilivyompeleleza baadae nikagundua ni stress za kukosa ajira.

Baada ya wiki kadhaa nikamtongoza na safari ya mapenzi ikaanzia hapo. Alikuwa anakuja sana 'ghetto' mpaka nikamkabidhi funguo, akawa anakuja muda wowote atakao, mimi nikiwa job (niliajiriwa fasta sana baada tu ya kumaliza chuo).

Kwa malezi yangu niliyolelewa nikaona kulala na mtoto wa mtu ndani bila wazazi wake kujua alipo sio poa. Nikawaza nimletee wazo la ndoa, maana katika story zetu alikuwa akizungumzia sana "Mr. Liverpool utanioa lini au ndio unanit*mba tuu?"

Ila kabla ya ndoa nikawaza nimtafutie ajira ili tuingie ndani ya ndoa tukiwa wote tunaingiza kipato. Nilihustle sana kutuma applications kila ofisi nikisikia hata tetesi natuma. Mara Mungu bariki akapata serikalini.

Ikapita miezi 3 nikaona ndio wakati wa kuleta proposal ya ndoa. Nilivyoiwakilisha mbele yake jibu alilonijibu "Mimi nafikiri siwezi kuolewa na mkristo, huo ni ukafiri" Aisee! asikwambie mtu, lile jibu liliniuma sana tena sana. Nilivyomwambia tuoane kila mtu abakie na dini yake (ilikuwa tarehe 01/May), mara tarehe 20/May naona anapost Facebook picha za ndoa, tena na 'baharia' waliokutana ofisiniI kwenye kazi niliyomtafutia.

Dah! Yule dada aliniuma sana. Yaani kujitoa kote kule, leo haya ndio malipo yangu? Time heals na nikasahau..

Mwaka huu mwezi wa 9, mara namba ngeni ikaingia. Kupokea kumbe ni yeye. Tuliongea mengi ila alileta proposal anataka kurudi kwa kafiri. Kisa mumewe ameoa mke wa pili na yeye uke wenza hawezi. Nilichomjibu mimi ni "Pambana na hali yako, mimi siwezi kufanya hivyo". Yeye akasema "Basi hata uwe mchepuko wangu?" Mimi nikasema "Siwezi aisee kumzunguka mwana kwa nyuma japo yeye alinizunguka".

Juzi kati nikapata safari ya kwenda Dar, akaniomba tuonane. Tukakutana mitaa ya Uwanja wa Ndege. Aisee! Amekonda. Tako lote limeyeyuka. Shape yote imesepa. Yaani mpaka namuonea huruma.

Tuliongea sana na nikamuomba kuondoka. Aliendelea kuomba ila nilichomjibu "Siwezi kukusaidia kwa lolote". Japo namuonea huruma sana ila "Kila mtu avune alichopanda".

Ukipendwa, pendeka mtoto wa kike.

Wanaume, tutumia kichwa kikubwa cha juu, cha chini huwa kinatudanganya sana.

#ASANTE
#YNWA
Achana nae bwege huyo.
 
Alifanya maamuzi sahihi kutokuolewa na kafiri , naona shetani anamchezea anataka kurudi alipotoka
Wewe SUNNI au SHIA..
Kama ni SHIA basi ni KAFIR MWENZANGU...

#YNWA

Wrote from Anfield...!!!
 
Back
Top Bottom