Ex wangu bana! Mungu amsaidie tuu

Ex wangu bana! Mungu amsaidie tuu

Liverpool_Jr

JF-Expert Member
Joined
Sep 7, 2019
Posts
1,220
Reaction score
1,417
Iko hivi...

Mwaka 2013 nilimaliza Bachelor na kurudi Dar, nilikutana na mtoto mmoja mzuri hatari. Alionekana ana stress kiasi na mzee baba nikajikaza na kuomba namba. Nilivyompeleleza baadae nikagundua ni stress za kukosa ajira.

Baada ya wiki kadhaa nikamtongoza na safari ya mapenzi ikaanzia hapo. Alikuwa anakuja sana 'ghetto' mpaka nikamkabidhi funguo, akawa anakuja muda wowote atakao, mimi nikiwa job (niliajiriwa fasta sana baada tu ya kumaliza chuo).

Kwa malezi yangu niliyolelewa nikaona kulala na mtoto wa mtu ndani bila wazazi wake kujua alipo sio poa. Nikawaza nimletee wazo la ndoa, maana katika story zetu alikuwa akizungumzia sana "Mr. Liverpool utanioa lini au ndio unanit*mba tuu?"

Ila kabla ya ndoa nikawaza nimtafutie ajira ili tuingie ndani ya ndoa tukiwa wote tunaingiza kipato. Nilihustle sana kutuma applications kila ofisi nikisikia hata tetesi natuma. Mara Mungu bariki akapata serikalini.

Ikapita miezi 3 nikaona ndio wakati wa kuleta proposal ya ndoa. Nilivyoiwakilisha mbele yake jibu alilonijibu "Mimi nafikiri siwezi kuolewa na mkristo, huo ni ukafiri" Aisee! asikwambie mtu, lile jibu liliniuma sana tena sana. Nilivyomwambia tuoane kila mtu abakie na dini yake (ilikuwa tarehe 01/May), mara tarehe 20/May naona anapost Facebook picha za ndoa, tena na 'baharia' waliokutana ofisiniI kwenye kazi niliyomtafutia.

Dah! Yule dada aliniuma sana. Yaani kujitoa kote kule, leo haya ndio malipo yangu? Time heals na nikasahau..

Mwaka huu mwezi wa 9, mara namba ngeni ikaingia. Kupokea kumbe ni yeye. Tuliongea mengi ila alileta proposal anataka kurudi kwa kafiri. Kisa mumewe ameoa mke wa pili na yeye uke wenza hawezi. Nilichomjibu mimi ni "Pambana na hali yako, mimi siwezi kufanya hivyo". Yeye akasema "Basi hata uwe mchepuko wangu?" Mimi nikasema "Siwezi aisee kumzunguka mwana kwa nyuma japo yeye alinizunguka".

Juzi kati nikapata safari ya kwenda Dar, akaniomba tuonane. Tukakutana mitaa ya Uwanja wa Ndege. Aisee! Amekonda. Tako lote limeyeyuka. Shape yote imesepa. Yaani mpaka namuonea huruma.

Tuliongea sana na nikamuomba kuondoka. Aliendelea kuomba ila nilichomjibu "Siwezi kukusaidia kwa lolote". Japo namuonea huruma sana ila "Kila mtu avune alichopanda".

Ukipendwa, pendeka mtoto wa kike.

Wanaume, tutumia kichwa kikubwa cha juu, cha chini huwa kinatudanganya sana.

#ASANTE
#YNWA
 
Katika viumbe vyenye dharau na wenye kujisahau ni hawa watoto wakike ,pole kiongozi na shukuru mungu kwa kupona majiraha ...

Mimi nilishawahi kataliwa enzi hizo sina kitu akaja olewa na mtu ambaye kwa wakati huo alikuwa na vyuma(pesa) ila mambo hayakuchukuwa muda kwa upande wao kubadilika na kushuka chini na mimi kuja juu ,[emoji23] alijirudi ila huwa namwambia huwa sisahau ubaya mtu naonifanyia kama ilivyokuwa unaponifanyia jema [emoji23] haya maisha yaache tu kama yalivyo ,tujifunze kutokumaliza maneno
 
yani huyo dada kifurushi chake kimebaki Dakika 5 kiishe

akiangalia salio anaambiwa

Ndugu mteja una dk 5600 za kupiga mitandao yote

SMS 280000000, DK 480000 ZA KUPIGA NNJE YA NCHI

data GB 35 za 4G

Kifurushi chako kitaisha ndani ya dk 5 zijazo.


(dada haelewi yaniiiiiiii)
 
Wazungu wanasemaga KARMA NEVER FORGETS..
Katika viumbe vyenye dharau na wenye kujisahau ni hawa watoto wakike ,pole kiongozi na shukuru mungu kwa kupona majiraha ...

Mimi nilishawahi kataliwa enzi hizo sina kitu akaja olewa na mtu ambaye kwa wakati huo alikuwa na vyuma(pesa) ila mambo hayakuchukuwa muda kwa upande wao kubadilika na kushuka chini na mimi kuja juu ,[emoji23] alijirudi ila huwa namwambia huwa sisahau ubaya mtu naonifanyia kama ilivyokuwa unaponifanyia jema [emoji23] haya maisha yaache tu kama yalivyo ,tujifunze kutokumaliza maneno
 
Nilimpa WAZO la KUWA MTEJA WANGU wa JUMLA ili apate pesa ARUDISHE TAKO..!!
Hata mimi ningekuwa wewe ningefanya hivyohivyo, urafiki unaweza usife iwapo eye atasisitiza ila hautakuwa wa karibu na mapenzi ndo kabisaaa hayatakuwepo.

Matata K.
Ila analeta mambo ya KITANDANI..

Nimepita mbali kama JET..

#ASANTE
#YNWA
 
Nilikutana nae ili nimpe wazo la Biashara "Awe mteja WANGU wa JUMLA wa DSM""
Bado unampend, unampa na ratiba zako za safari na kukutana nae wakati alikuita kafiri..... .... you are not serious ni suala la mda utamrudia tu huna msimamo kaka
Ila alivyoleta mambo ya KITANDANI..

Nimetemana nae..

#ASANTE
#YNWA
 
Back
Top Bottom