Ex boyfriend anataka nimlipe gharama zake

Ex boyfriend anataka nimlipe gharama zake

Wee mrudishie vitu vyake alafu ukome kudate na wazee' uache tamaa ya kudeal na wazee wenye familia kisa pesa utaja uwawa bure ona sasa anavyokutia jamba jamba mpaka unakimbilia chooni, manake inaonekana huyo mzee ni kigogo mpaka umesema anajuana na polisi sana sio mchezo!
 
mie nisingemrudishia hata sent 5......ningemwambie ye anilipe vyangu angeweza maana vingine havilipiki

hakuna cha kuku ufoo wala nini halafu kumbe ana mke kosa lake si angekua mkweli tangu mwanzoni

Yani apo ana mdai shingapi si amulipe tu aepukane na kero shida wanawake ni wepesi wakudanganyika huwa mnachukulia easy especially kwenye mahusiano first of all inatakiwa mtuchunguze wengi wetu wanaume wanao honga wana wake nyumbani
Jamani mfanye research wakina dada
 
Inategemea alikupa nini na kwa makubaliano gani. Lakini ikiwa ni zawadi za kawaida hana haki ya kudai.
 
Hilo ndilo tatzo la kuDeal na wazee wame za watu kwa tamaa za pesa, mpaka wanasahau familia zao sasa mke wa huyu mzee maombi yake yamejibiwa kwa dizain hiyo mwaka huu utakimbilia sana chooni' acheni maisha ya shortcut tafuta hele na vitu vyako mwenyewe!!

ha ha ha yaani mzee ndo anamuita ex-boy.. wanawake wanamambo jamani.. kumbe ni kibabu
 
Huyo malizana nae tu,kila mtu ana roho yake ,usishangae kudaiwa kama makubaliano siyo
 
Mwambie na wewe akurudishie mihemuko na penzi ulilokuwa unampa.
 
Wee mrudishie vitu vyake alafu ukome kudate na wazee' uache tamaa ya kudeal na wazee wenye familia kisa pesa utaja uwawa bure ona sasa anavyokutia jamba jamba mpaka unakimbilia chooni, manake inaonekana huyo mzee ni kigogo mpaka umesema anajuana na polisi sana sio mchezo!

Atakua ni mzee wa mjini huyo
 
Kabla ya kutoa maoni naomba kukuuliza maswali yafuatayo.Nyumba unayoishi kwa sasa ni yako au yakwake.swali la pili .kama nyumba sio ya kwake hainahaja kuwa na wasiwasi maana hamkufunga ndoa cha msingi ni kuripoti polisi kuwa umetishiwa maisha maana hili ni kosa la jinai.PIa kama unaweza unaweza tafuta ndugu au marafiki wa kuishi nao hapo washirikishe wazazi .
Ajipime,ajitafakari kwa kina na ajihoji km hana nia chafu ya kudhulumu jasho la mtu....vinginevyo akilinde asije wakam-ufoo saro!
 
ndugu wana mmu naomba msaada kwani nimejaribu kutafuta kwa njia ya kawaida nimekosa msaada,tatizo ni ex wangu yapata mwezi na kitu tangu tumeachana anataka nimrudishie gharama zake pamoja na baadh ya vitu alivyoninunulia,kanitumia msg za vitisho ila kikubwa ni kwamba niligundua ana mke muda kidogo lakini kila nilipomwambia tuachane anasema nimrudishie kila kitu,tangu mwezi sasa nimefanya maamuzi magumu lakin ndo kama imekua mwiba kila saa sms na cm za kunitisha jana kaja kanigongea mlango nikakimbilia chooni maana taa ilikua inamulika hivyo hakuniona baadhi ya vitu alivyonipa kasoro kimoja ndo kina jina lake sasa nafanye kumbukeni kanitumia na kumbukeni ni mtu anaefahamiana na polisi sasa nafanyaje????

Weka mkataba hapa tuupitie kwanza ndiyo tuanze kukupa za uso
 
Wee mrudishie vitu vyake alafu ukome kudate na wazee' uache tamaa ya kudeal na wazee wenye familia kisa pesa utaja uwawa bure ona sasa anavyokutia jamba jamba mpaka unakimbilia chooni, manake inaonekana huyo mzee ni kigogo mpaka umesema anajuana na polisi sana sio mchezo!

Kweli huyu atakua kibabu labda ni kapuy@ ha ha ha
 
Pole sana, ila hili liwe fundisho kwa wadada wengine, kuwa makini pindi mtu anapotaka kuanzisha mauhusiano.
Kumchunguza kwanza kama anakupenda atakusubiri kipindi unamchunguza.

Kuhusu wewe na huyo jamaa yeye ana wivu umempiga chini, so maumivu ya kuachwa hayo.
Jaribu kushirikisha watu wenu wa karibu, kama unasema anajuana na polisi.
Aseme ni kiasi gani na mtasuluhishwa, ikishindikana kamshtaki mahakamani. Anakunyima uhuru na kukutishia.
 
Yani apo ana mdai shingapi si amulipe tu aepukane na kero shida wanawake ni wepesi wakudanganyika huwa mnachukulia easy especially kwenye mahusiano first of all inatakiwa mtuchunguze wengi wetu wanaume wanao honga wana wake nyumbani
Jamani mfanye research wakina dada

si nyingi lakini naeza ita nyingi kwani sina uwezo wa kuirudisha na pia hakuna makubaliano yoyote ya mimi kurudisha ni pesa za kawaida ambazo hata wewe kama una mpenzi una weza kumpa
 
ha ha ha yaani mzee ndo anamuita ex-boy.. wanawake wanamambo jamani.. kumbe ni kibabu

Itakuwa tu huyo ni mzee japo hakutaka kutwambia, ila kwa hakili tu ya kawaida utajua tu huyo mtu ni wamakamo na inaonekana kamgharamikia sana huyu mdada, na inaweza kuwa huyu mdada ndio mwenye makosa labda kaleta king'asti kwenye room aliopangishiwa na huyo jamaa huwezi jua!!
 
Pole sana, ila hili liwe fundisho kwa wadada wengine, kuwa makini pindi mtu anapotaka kuanzisha mauhusiano.
Kumchunguza kwanza kama anakupenda atakusubiri kipindi unamchunguza.

Kuhusu wewe na huyo jamaa yeye ana wivu unempiga chini, so maumivu ya kuachwa hayo.
Jaribu kushirikisha watu wenu wa karibu, kama unasema anajuana na polisi.
Aseme ni kiasi gani na mtasuluhishwa, ikishindikana kamshtaki mahakamani. Anakunyima uhuru na kukutishia.

asante ila sieezi kwani alishawahi nipiga kwa hiyo kumuita kusuluisha itakua ngum
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom