EWURA yapandisha Mafuta kwa ongezeko la wastani wa Shilingi 200/ltr

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Aug 24, 2011
49,242
103,943
Kumekucha watanzania na wapiga kura wa nchi hii.Wakuu wa EWURA huku wakiwa na nyuso za bashasha kana kwamba wanatangaza jambo jema,wametangaza Bei mpya ya nishati ya mafuta.

Mafuta yamepanda kwa wastani wa TShs 200 kwa lita.Sababu kubwa ikiwa na kupanda kwa dola.Wachumi mtuambie hii italeta madhara makubwa kiasi gani kwa mtanzania wa kawaida.

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU BEI KIKOMO ZA MAFUTA AINA YA PETROLI KUANZIA JUMATANO, TAREHE 1 JULAI 2015

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) inatangaza bei kikomo za bidhaa za mafuta ya petroli hapa nchini.

Bei hizi zitaanza kutumika kuanzia Jumatano, Tarehe 1 Julai 2015. Pamoja na kutambua bei kikomo za bidhaa mbalimbali za petroli nchi nzima, ni muhimu kuzingatia yafuatayo:-

(a) Bei za jumla na rejareja kwa mafuta ya aina zote yaani Petroli, Dizeli na Mafuta ya Taa zimebadilika ikilinganishwa na toleo lililopita la tarehe 3 Juni 2015.

Kwa Mwezi Julai 2015, bei za rejareja kwa Petroli, Dizeli na Mafuta ya Taa zimeongezeka kama ifuatavyo: TZS 232/lita sawa na asilimia 11.82 TZS 261/Lita sawa na asilimia14.65 na TZS 369 /lita sawa na asilimia 22.75 sawia.

Kwa kulinganisha na toleo la mwezi uliopita, bei za jumla kwa mafuta ya Petroli, Dizeli na Mafuta ya Taa nazo zimeongezeka kama ifuatavyo: TZS 232.35/lita sawa na asilimia 12.49 TZS 261.15/lita sawa na asilimia 15.57 na TZS 369.41/lita sawa na asilimia 24.32.

Mabadiliko haya yametokana na mabadiliko ya bei za mafuta katika soko la dunia, kuendelea kudhoofu kwa thamani ya shilingi dhidi ya dola ya Marekani pamoja na mabadiliko ya tozo za Serikali katika mafuta kuanzia mwezi wa Julai 2015.

Kwa kulinganisha thamani ya Shilingi dhidi ya dola ya Marekani kwa machapisho ya bei za mwezi Juni na Julai 2015, Shilingi ya Tanzania imepungua thamani kwa TZS 175.11 kwa dola ya Marekani sawa na asilimia 8.65.

(b) Kwa mujibu wa Sheria ya Mafuta ya mwaka 2008, bei za bidhaa za mafuta ya petroli zitaendelea kupangwa na soko. EWURA itaendelea kuhamasisha ushindani kwa kutoa taarifa za bei kikomo za bidhaa za mafuta.

Taarifa hizi zina lengo la kuwasaidia wadau kufanya maamuzi stahiki kuhusu manunuzi ya bidhaa za mafuta.

(c) Kampuni za mafuta zipo huru kuuza bidhaa za mafuta ya petroli kwa bei ya ushindani ilimradi bei hizo ziko chini ya bei kikomo (price cap) kama ilivyokokotolewa na fomula iliyopitishwa na EWURA na ambayo ilichapwa kwenye Gazeti la Serikali Na. 7 la tarehe 4 Machi 2015.

(d) Vituo vyote vya mafuta vinatakiwa kuchapisha bei za bidhaa za mafuta katika mabango yanayoonekana bayana na yakionyesha bei ya mafuta, punguzo, vivutio vya biashara au promosheni zinazotolewa na kituo husika. Pale ambapo inawezekana kuchagua, wateja wanashauriwa kununua bidhaa za mafuta kutoka kwenye vituo vinavyouza mafuta kwa bei ndogo zaidi ili kushamirisha ushindani. Ni kosa kuuza mafuta bila kuweka mabango ya bei inayoonekana vizuri kwa wateja na adhabu itatolewa kwa kituo husika.

(e) Wanunuzi wanashauriwa kuhakikisha kuwa wanapata stakabadhi ya malipo inayoonesha jina la kituo, tarehe, aina ya mafuta yaliyonunuliwa na bei kwa lita. Stakabadhi hiyo ya malipo itatumika kama kidhibiti cha mnunuzi wa mafuta endapo kutajitokeza malalamiko ya ama kuuziwa mafuta kwa bei ya juu kuliko bei kikomo; ama endapo utakuwa umeuziwa mafuta yenye kiwango cha ubora kisichofaa.

A: BEI ZA REJAREJA






BeiKikomo


Mji

Petroli
(Sh/Lita)

Dizeli
(Sh/lita)

MafutaYaTaa
(Sh/Lita)
DaresSalaam
2,198
2,043
1,993
Arusha
2,282
2,127
2,077
Arumeru (Usa West)
2,282
2,127
2,077
Karatu
2,300
2,145
2,095
Monduli
2,287
2,133
2,083
Ngorongoro (Loliondo)


2,338


2,184
2,134
Kibaha
2,203
2,048
1,998
Bagamoyo
2,209
2,054
2,004
Kisarawe
2,205
2,050
2,000
Mkuranga
2,208
2,053
2,003
Ruiji
2,226
2,071
2,021
Dodoma
2,257
2,102
2,052
Bahi
2,264
2,109
2,059
Chemba
2,283
2,128
2,078
Kondoa
2,289
2,135
2,085
Kongwa
2,254
2,099
2,049
Mpwapwa
2,258
2,103
2,053
Iringa
2,262
2,107
2,057
Kilolo
2,266
2,112
2,062
Muindi (Mainga)
2,272
2,117
2,067
Njombe
2,290
2,135
2,085
Ludewa
2,328
2,173
2,123
Makete
2,321
2,166
2,116
Wanging'ombe (Igwachanya)


2,288


2,133
2,083
Bukoba
2,413
2,258
2,208
Biharamulo
2,387
2,233
2,183
Karagwe (Kayanga)
2,429
2,275
2,225
Kyerwa (Ruberwa)
2,435
2,280
2,230
Muleba
2,413
2,258
2,208
Ngara
2,378
2,224
2,174
Misenyi
2,421
2,267
2,217
Geita
2,363
2,208
2,158
Bukombe
2,352
2,197
2,147
Chato
2,384
2,229
2,179
Mbogwe
2,401
2,246
2,196

Nyang'hwale 2,378 2,223
2,173
Kigoma 2,429 2,274
2,224
Uvinza(Lugufu) 2,441 2,286
2,236
Buhigwe 2,418 2,263
2,213
Kakonko 2,386 2,231
2,181
Kasulu 2,415 2,260
2,210
Kibondo 2,393 2,238
2,188
Moshi 2,272 2,117
2,067
Hai(Bomang'ombe) 2,275 2,120
2,070
Mwanga 2,265 2,110
2,060
Rombo(Mkuu) 2,293 2,138
2,088
Same 2,258 2,103
2,053
Siha(SanyaJuu) 2,278 2,123
2,073
Lindi 2,257 2,102
2,052
KilwaMasoko 2,232 2,077
2,027
Liwale 2,278 2,123
2,073
Nachingwea 2,286 2,131
2,081
Ruangwa 2,284 2,129
2,079
Babati 2,320 2,165
2,115
Hanang(Katesh) 2,331 2,176
2,126
Kiteto(Kibaya) 2,331 2,176
2,126
Mbulu 2,333 2,178
2,128
Simanjiro(Orkasumet) 2,352 2,197
2,147
Musoma 2,376 2,221
2,171
Rorya(Ingirijuu) 2,385 2,230
2,180
Bunda 2,367 2,212
2,163
Butiama 2,373 2,218
2,168
Serengeti(Mugumu) 2,422 2,267
2,217
Tarime 2,387 2,232
2,182
Mbeya 2,305 2,150
2,100
Chunya 2,314 2,160
2,110
Ileje 2,318 2,163
2,113
Kyela 2,321 2,166
2,116
Mbarali(Rujewa) 2,289 2,134
2,084
Mbozi(Vwawa) 2,314 2,159
2,109
Momba(Chitete) 2,323 2,168
2,118
Rungwe(Tukuyu) 2,314 2,159
2,109
Morogoro 2,223 2,068
2,018
Mikumi 2,239 2,084
2,034
Kilombero(Ifakara) 2,261 2,106
2,056
Ulanga(Mahenge) 2,271 2,117
2,067
Kilosa 2,241 2,087
2,037
Gairo 2,241 2,087
2,037
Mvomero (WamiSokoine) 2,233 2,079
2,029


Turian 2,248 2,093
2,043
Mtwara 2,270 2,116
2,066
Nanyumbu(Mangaka) 2,319 2,164
2,114
Masasi 2,296 2,141
2,091
Newala 2,302 2,147
2,098
Tandahimba 2,295 2,141
2,091
Mwanza 2,348 2,193
2,143
Kwimba 2,384 2,229
2,179
Magu 2,356 2,201
2,151
Misungwi 2,353 2,199
2,149
Sengerema 2,380 2,225
2,175
Ukerewe 2,407 2,252
2,202
Sumbawanga 2,371 2,216
2,166
Kalambo(Matai) 2,363 2,208
2,158
Nkasi(Namanyele) 2,384 2,229
2,179
Katavi(Mpanda) 2,405 2,251
2,201
Mlele(Inyonga) 2,384 2,229
2,179
Songea 2,321 2,166
2,116
Mbinga 2,355 2,200
2,150
Namtumbo 2,350 2,196
2,146
Nyasa(MbambaBay) 2,357 2,202
2,152
Tunduru 2,380 2,225
2,175
Shinyanga 2,327 2,172
2,122
Kahama 2,340 2,185
2,135
Kishapu 2,355 2,200
2,150
Simiyu(Bariadi) 2,368 2,213
2,163
Busega(Nyashimo) 2,361 2,206
2,156
Itilima(Lagangabilili) 2,371 2,216
2,166
Maswa 2,359 2,205
2,155
Meatu(Mwanhuzi) 2,366 2,212
2,162
Singida 2,289 2,134
2,084
Iramba 2,301 2,146
2,096
Manyoni 2,273 2,118
2,068
Ikungi 2,284 2,129
2,079
Mkalama(Nduguti) 2,313 2,158
2,108
Tabora 2,352 2,197
2,147
Igunga 2,306 2,151
2,101
Kaliua 2,370 2,215
2,165
Ulyankulu 2,364 2,209
2,159
Nzega 2,316 2,162
2,112
Sikonge 2,364 2,209
2,159
Urambo 2,365 2,210
2,160
Tanga 2,244 2,089
2,039
Handeni 2,224 2,069
2,019


Kilindi 2,258 2,103
2,053
Korogwe 2,237 2,082
2,032
Lushoto 2,247 2,092
2,042
Mkinga(Maramba) 2,258 2,104
2,054
Muheza 2,244 2,089
2,039
Pangani 2,251 2,096
2,046


B:BEIZAJUMLA

Beiza Jumla -DSM Petroli(Sh/L) Dizeli(Sh/L) MafutayaTaa(Sh/L)
BeiKikomo 2,093.03 1,938.24 1,888.27
MKURUGENZI MKUU EWURA


Felix Ngamlagosi
http://www.ewura.go.tz/newsite/attachments/article/252/Cap Prices WEF 01 July 2015 -Swahili.pdf
 
Bei ya mafuta jioni hii apa kasulu ni sh 2415/= toka sh. 2,183/=. nilivyouliza kwenye vituo hivi,nieambiwa unataka pesa ya kampeni kwa chama tawala itoke wapi? nilipoconnect dots, nimegundua ndiyo maana wabunge wa ccm waliipitisha bajeti yenye ongezeko la bei ya mafuta ya taa,diseli na petrol. jambo la kujiuliza, serikali kwanini inasimamia uhuni huu? wananchi tujianda, tuhamasishane maamuzi magumu ya kuisambaratisha ccm
 
Bei ya mafuta jioni hii apa kasulu ni sh 2415/= toka sh. 2,183/=. nilivyouliza kwenye vituo hivi,nieambiwa unataka pesa ya kampeni kwa chama tawala itoke wapi? nilipoconnect dots, nimegundua ndiyo maana wabunge wa ccm waliipitisha bajeti yenye ongezeko la bei ya mafuta ya taa,diseli na petrol. jambo la kujiuliza, serikali kwanini inasimamia uhuni huu? baya zaidi ewura leo wako apa kasulu mjini huku ufedhuri unaendelea. wananchi tujianda, tuhamasishane maamuzi magumu ya kuisambaratisha nyinyiem
 
Gapco morogoro mjini saa moja na nusu jioni 30/06/2015 ilikuwa ni Tsh 1991/= wakati mafuta ya taa yakikosekana vituo vyote Simba oil, Lake Oil, Camel, BP, ATN, Gapco.
 
Bei ya mafuta jioni hii apa kasulu ni sh 2415/= toka sh. 2,183/=. nilivyouliza kwenye vituo hivi,nieambiwa unataka pesa ya kampeni kwa chama tawala itoke wapi? nilipoconnect dots, nimegundua ndiyo maana wabunge wa ccm waliipitisha bajeti yenye ongezeko la bei ya mafuta ya taa,diseli na petrol. jambo la kujiuliza, serikali kwanini inasimamia uhuni huu? baya zaidi ewura leo wako apa kasulu mjini huku ufedhuri unaendelea. wananchi tujianda, tuhamasishane maamuzi magumu ya kuisambaratisha ccm

Maisha bora kwa kila Mtanzania...
 
Kama unadhani ufisadi aliofanya EL miaka michache nyuma hauna madhara, angalia bei za vitu kama mafuta, vipuli, vifaa vya ujenzi, thamani ya fedha za kigeni ukilinganisha na shilingi yetu na kadhalika, ndo utajua hata mimba hutoa mtoto baada ya kipindi fulani kupita. Kwa hyo sema hapana kwa mzee wa ngarashi kwa sababu tukimwendekeza tutakuja kujuta kuwa watanzania. SAY NO TO EL
 
Mbona dola imeshuka sana jamani kuonyesha kuwa dafu limeanza kupanda thamani. Sasa kwanini bei ipande hivi?
 
Hii ni mbinu ya CCM kujipatia fedha kwa ajili ya Kampeni naandika hiki nikiwa na uhakika kwani wauzaji wa mafuta wakubwa hapa nchini wengi wao ni viongozi na wengine ni wanachama wa CCM na nikiunganisha Dot na kauli ya Ndugai Bungeni juu ya Hoja ya Mnyika ninajihakikishia kuwa mpango huu umepangwa ili CCM ipate fedha za kampeni za uchaguzi mkuu ingawa wanakuja na hoja eti thamani ya shillingi imeshuka sikubaliani na hili.
 
Wakati duniani kote bei ya mafuta inashuka Tanzania inapanda; amazing. Halafu mamlaka ya kupandisha bei wanapewa na nani? Navyojua mimi, waziri Mkuya ndio mtu pekee mwenye maamuzi hayo na kasema yatapanda kwa sh/100, mia mbili tena imetoka wapi?

If there is unjustified cos kuna watu annually itawa cost kiasi inabidi wakate tu matumizi mengine kufidia kodi na tozo za serikari it is very expensive to live in Tanzania under the minimum wage.
 
Kama unadhani ufisadi aliofanya EL miaka michache nyuma hauna madhara, angalia bei za vitu kama mafuta, vipuli, vifaa vya ujenzi, thamani ya fedha za kigeni ukilinganisha na shilingi yetu na kadhalika, ndo utajua hata mimba hutoa mtoto baada ya kipindi fulani kupita. Kwa hyo sema hapana kwa mzee wa ngarashi kwa sababu tukimwendekeza tutakuja kujuta kuwa watanzania. SAY NO TO EL

Khaaaa kwa hiyo lowasa anahusika kwenye kila kitu nchi hii? IPTL, escrow, epa, meremeta, kagoda, mabehewa feki, mikataba feki ga madini, gesi etc etc kote huko lowasa anahusika? Aaaah acheni umaskini wa fikra, naona kila kitu tunajificha kwenye kivuli cha Lowassa...
 
Watanzania hatuna pa kukimbilia. Mara thamani ya shilingi imeshuka, mara mafuta yamepanda, mara Escrow; kote huko ni kutunyonya wanyonge. Ni nadra kusikia jambo la afueni, kwa raia ni vibano tu..!
 
Back
Top Bottom