EWURA wavifungia vituo vinne vya mafuta kuuza Petroli

Mwanajamii

JF-Expert Member
Mar 5, 2008
7,063
68
Serikali kwa mara nyingine imevifungia vituo vinne vya mafuta jijini Dar es Salaam kuuza Petrol baada ya kukiuka bei elekezi zilizotolewa kwa madai kuwa ni ndogo. Vituo vilivyofungiwa ni GBP shekilango, Camel Oil Tabata, Camel Oil Mbagala na Gapco fire.

Pamoja na hatua hiyo, vituo vingine nane vimeonywa.
 
Nilitaka kusema mwanzo mzuri,nikakumbuka kumbe ni mwaka 50 wa uhuru wa Tanganyika!
Naona serikali inajitahidi kuchezacheza mfukoni mwa wafanyabiashara!
 
Ina maana hivyo vilivyo onywa ndo vimeruhusiwa kuuza kwa bei ya juu kwa muda au mie ndo sijaelewa vizuri?
 
wamevuna walichopanda haiwezekani bei ikipanda wanachekelea na ikiSHUKA WAGOME.HUU NAO NI UFISADI NA NI UHUJUMU UCHUMI
 
Bei za mafuta nchi hii ni upuuzi mtupu wala sioni la maana linalofanywa na hao EWURA wala serikali yenyewe. Zamani wakati watu wakificha vitu na kuviuza kwa bei ya kuruka WALIKAMATWA na walikuwa wanauza kwa uficho! Leo hii WALANGUZI hao wanauza HADHARANI na hakuna anaewagusa.

Hali halisi inaonesha kwamba, wengi wa wafanyibiashara ya mafuta ni WANASIASA, NA VIGOGO. Aidha wengi wao ni wafanyibiashara walio wafadhili wa vyama vya siasa, michezo na mashirika ya dini. Na hali inaonesha kwamba SERIKALI INAWAOGOPA NDIO MAANA SI WAO WALA WALE 'WACHUUZI WAO' WANAOWAPA MAFUTA ILI WATULANGUE MITAANI HAWAGUSWI KANA KWAMBA WANAFANYA JAMBO LA MSAADA SANA!

Inafikia hatua mtu unajiuliza "HIVI ILIKUWAJE UKAJIKUTA UMEZALIWA TANZANIA"
 
Ni hatua nzuri ili wengine ambao hatua hii haijawakumba wasije kufanya hivyo.
 
A
Bei za mafuta nchi hii ni upuuzi mtupu wala sioni la maana linalofanywa na hao EWURA wala serikali yenyewe. Zamani wakati watu wakificha vitu na kuviuza kwa bei ya kuruka WALIKAMATWA na walikuwa wanauza kwa uficho! Leo hii WALANGUZI hao wanauza HADHARANI na hakuna anaewagusa.

Hali halisi inaonesha kwamba, wengi wa wafanyibiashara ya mafuta ni WANASIASA, NA VIGOGO. Aidha wengi wao ni wafanyibiashara walio wafadhili wa vyama vya siasa, michezo na mashirika ya dini. Na hali inaonesha kwamba SERIKALI INAWAOGOPA NDIO MAANA SI WAO WALA WALE 'WACHUUZI WAO' WANAOWAPA MAFUTA ILI WATULANGUE MITAANI HAWAGUSWI KANA KWAMBA WANAFANYA JAMBO LA MSAADA SANA!

Inafikia hatua mtu unajiuliza "HIVI ILIKUWAJE UKAJIKUTA UMEZALIWA TANZANIA"
Wewe kabla hujaandika jaribu kufanya utafiti kwanza
Hata kidogo tu. Acha uvivu na sweeping statements.
 
GBP shekilango!!!!!!? they cant be serious, halafu oilcom wameachiwa?
 
Back
Top Bottom