nyumbu mwerevu
Member
- Nov 11, 2016
- 88
- 92
Jamani pia fanyeni uchunguzi kwa vituo vya mafuta vya BAGENI vilivyopo kanda ya ziwa,lita 5 unapimiwa lita 4
Ukiwapa taarifa wanafanyia kazi suala hili Mkuu wapo kila Mkoa Tanzania hiiBasi hii changamoto inamhusu, sijui kama huwa wanafanyia kazi taarifa kama hizi au nao ni kama PCCB na NEMC
Pole sana mkuu.
Hayo yapo sana. Mi huwa nahisi wauza nafuta wanazichezea pump kiasi kwamba hata wakaguzi wa vipimo huwa hawang'amui ama wanakula nao maana utakuta ukaguzi wameufanya jana na kuweka stika zao/ wakala wa vipimo lakini bado hakuna mabadiliko.
Ina kera sana hii hali.
Vituo gani mkuuVituo vya ridhiwani ndio balaa mpaka bodaboda wamesanuka
Nipo mjini Morogoro, siku kadhaa zilizopita nilikwenda kununua petroli kwenye kituo cha mafuta kilichopo opp na stand ya Dodoma, ambapo bei zao kwa lita ni shilingi 2348, mafuta hayo yalikwisha baada ya mizunguko yangu ya kilomita kadhaa na nikapata hofu, jana nikahamia kituo kingine kilichopo na eneo hilohilo, mafuta niliyopata yalinifikisha umbali uleule wa juzi na yakabaki, nikapata wasiwasi kwamba kituo kimoja kinafanya ujanja.
Leo nimekutana na vijana wawili wanaouza mafuta ya kupima kwenye chupa, vijana hao hununua mafuta kwenye vituo hivyo viwili tofauti, leo walipokutana wakawa wanapeana uzoefu kuwa wakinunua mafuta ya shilingi 56000 kwenye kituo kinachouza mafuta kwa bei ya juu wanapata lita 22.29 lakini kwenye kituo kinachouza mafuta kwa bei ya chini wanapata mafuta pungufu zaidi, kitu kinachoashiria kuwa kuna wizi unafanyika.
Kwa scenario hizo mbili, mkasa wa kwangu na wale vijana wawili ninajifunza kuwa EWURA mnatakiwa kufanya ukaguzi wa kushitukiza kubaini ujanja unaofanywa na vituo vya mafuta, nimejifunza pia kuwa wengi wa wahanga wa wizi huu ni wanunuzi wanaoweka mafuta kwenye matanki ya magari moja kwa moja, wenzetu wanaonunua kwenye madumu wanaweza kubaini mchezo huo mchafu kwa urahisi zaidi.
Mimi acha nionekane mshamba tu ila natembea na dumu langu
nikilipa 20 liters naziona ...wengine unakuta inazidi mpka 5,000 then wananiambia ni offer kumbe washaona 20 lots haijafika
Huu mchezo una mnyororo mrefu kuanzia wauza mafuta pump attendants mmiliki wa kituo hadi hao sijui wewura! Pump zinachezewa na mafundi, mmiliki ana mtu wake huko wewera siku wakipanga hizo safari za kishtukiza mtu wa wewera anampigia mmiliki simu fasta fundi anaitwa wanarekebisha hata wakija kusoma zinatoka lita zilezile za kipimo. Kingine kwenye hizo filling stations kuna pump moja ambayo wanaichezea na hiyo ndo kula ya mwenye pump mwisho wa mwezi pump attendtants wanapewa bonus kama responsibility allowance elfu hamsini maisha yanasonga. Usitarajie wewera kuwakamata kwa kushtukiza ni mpango usio rasmi wameuweka.
Swala la uaminifu ni sifuri kwa jamii zetu, hata Dar kuna "sheli" ukithubutu kujaza mafuta imekula kwako. Tunawaza kuiba mda wote...
Pole sana mkuu.
Hayo yapo sana. Mi huwa nahisi wauza nafuta wanazichezea pump kiasi kwamba hata wakaguzi wa vipimo huwa hawang'amui ama wanakula nao maana utakuta ukaguzi wameufanya jana na kuweka stika zao/ wakala wa vipimo lakini bado hakuna mabadiliko.
Ina kera sana hii hali.
Mkuu mbona nimetaja vyote viwili, labda rudia kusoma uzi vizuri.
umeshindwa kulikabili kabisaMkuu ili suala ni kubwa mi nshamuachaga Mungu maana unajaza mafuta lakini unatembea kwa hofu