Faana
JF-Expert Member
- Dec 12, 2011
- 31,281
- 32,325
Nipo mjini Morogoro, siku kadhaa zilizopita nilikwenda kununua petroli kwenye kituo cha mafuta kilichopo opp na stand ya Dodoma, ambapo bei zao kwa lita ni shilingi 2348, mafuta hayo yalikwisha baada ya mizunguko yangu ya kilomita kadhaa na nikapata hofu, jana nikahamia kituo kingine kilichopo na eneo hilohilo, mafuta niliyopata yalinifikisha umbali uleule wa juzi na yakabaki, nikapata wasiwasi kwamba kituo kimoja kinafanya ujanja.
Leo nimekutana na vijana wawili wanaouza mafuta ya kupima kwenye chupa, vijana hao hununua mafuta kwenye vituo hivyo viwili tofauti, leo walipokutana wakawa wanapeana uzoefu kuwa wakinunua mafuta ya shilingi 56000 kwenye kituo kinachouza mafuta kwa bei ya juu wanapata lita 22.29 lakini kwenye kituo kinachouza mafuta kwa bei ya chini wanapata mafuta pungufu zaidi, kitu kinachoashiria kuwa kuna wizi unafanyika.
Kwa scenario hizo mbili, mkasa wa kwangu na wale vijana wawili ninajifunza kuwa EWURA mnatakiwa kufanya ukaguzi wa kushitukiza kubaini ujanja unaofanywa na vituo vya mafuta, nimejifunza pia kuwa wengi wa wahanga wa wizi huu ni wanunuzi wanaoweka mafuta kwenye matanki ya magari moja kwa moja, wenzetu wanaonunua kwenye madumu wanaweza kubaini mchezo huo mchafu kwa urahisi zaidi.