ntamaholo
JF-Expert Member
- Aug 30, 2011
- 12,906
- 6,909
Wana Bodi salamuni.
Naomba kuwasilisha kuwa, Mwenyekiti wa Ulinzi na Usalama mkoa wa Mwanza, Mhandisi Evarist Ndikilo, yuko katika wakati mgumu kutokana na yeye kushiriki kikao cha usuluhishi ambacho badala ya kuamua mambo kwa kuzingatia sheria za nchi, alitumia ukuu wake wa mkoa kuamua jambo lililokuwa mbele yake.
Jijini Mwanza, kumefukuta mgogoro wa kidini kati ya WAISLAM na WAKRISTO. Mggogoro huo ulianzia pande za IGOMBE-KAYENZE, ambako mchungaji mmjoa wa kanisa la kipentecoste alichinja ng'ombe kwa ajili ya kitoweo kwa watu waliofika kuhani msiba. Kwa kuwa msiba ni suala la kijamii, linawajumuisha WAKRISTO, WAISLAMU na dini nyingine, waislam walisusia chakula kile kwa kudai kuwa aliyechinja hakua muislam. Na wakapitisha maazimio kuwa, wao watakuwa wanashiriki misiba tu lakini vyakula vya msibani hawatakula kwa kuwa vinaandaliwa na makafiri.
Mchungaji yule alipata misukosuko lakini kwa kuwa hakuna sheria ya kumshitaki, aliachiwa huru huku kukiwa na bifu kati ya waumini wa dini hizi mbili.
Ndipo migogoro mingine imeibuka, na katika juhudi za kuitatua, Mkuu wa Mkoa alijikuta akisahau kutumia katiba ya nchi na sheria zake kwa kutamka mbele ya hadhara iliyokuwepo, kuwa WAISLAM ndio wenye jukum la kuchinja. Tamko hili liliwatifua na sasa wanahamasihsana waweke watu wao kule machinjioni na wafungue bucha waandike kabisa bucha ya mkristo.