Evarist Chahali: Kila mwenye mapenzi ya dhati na Tanzania amwambie Magufuli "unaipeleka nchi kusikofaa"

Hivi sisi waafrica zimo kweli? ujue mimi wakati mwingine huwa sielewi kama tuko sawa au ni laana inatusumbua,unaua mtu ili ushinde siasa, halafu hizo siasa zitakupeleka wapi maana ni kitu cha muda tu, hebu ccm acheni hizi tabia, tumieni elimu na busara kupima mambo, itafika wakati tukiwaona tunakimbia.
 
.....Someni basi habari muielewe ndiyo mkimbilie ku comment......''ni mtanzania, naishi New Zealand....''..........Wewe kwenye hiyo bolded red umetoa wapi??
Wewe mwenyewe kusoma habari na kuilewa hujaweza

Aliyesema anaishi New Zealand ni mwingine kabisa sio Chahali
Chahali yupo Uscotch huko
 
KAMA NA WATUMISHI WA IDALA NYETI NAO WANAANZA KUGEUKA BASI TUNAPOELEKEA SIO PAZURI NI VYEMA BUSARA NA HEKIMA ZIKAANZA KUTUMIKA
CCM siku zote inafanyaga kweli,mambo yasio ya kiungwana,LAKINI bwana usalama hakutaka kumalizia habari labda akiba ya maneno ni kinga kamili,kuna kesho na keshokutwa.
CCM kwa nje ni chama cha siasa lakini kwa ndani mmmh anakatika mtu mbele ya mic,na wala wazee wenyewe akina Mwl.Nyerere wala hawakushangaa pale Dodoma.
Je kuna mtu anajua mbunge majinuni alichohaidiwa au kilichomkimbiza mbio hadi kahama upinzani,sio bure.Walishasema watatawala miaka elfu kama dunia itakuwa bado ipo.
 
Richard
Zaidi ya kuonyesha na wewe ni usalama wa taifa umeandika mashudu tu hapa hamna facts zozote

Haya hongera kwa kuwa usalama wa taifa ..kama wewe ndio reference ya watu waliopo huko hii idara inahitaji kufumuliwa yote

Ni wapi Chahali alishawahi kumsapoti Lowasa ? Oh double agent ...huu uongo pekee umetosha kuonyesha ulivyo na hizo sijui unazoita facts.
 
Hahaha hata waliomsifia wanaanza kumkana.
Hata ukioga kwenye vinu vya chibuku hulewi, kumbe pombe mpaka uinywe.
 
Mkuu, Evarist Chahali

Kwanza nipende kukukumbusha kwamba wewe sasa hivi huwezi kuaminiwa na nchi kama unafaa tena kuwa mlinzi wa taifa kutokana na rekodi yako ya huko nyuma.

Pili, mpaka sasa hujaeleza ni sababu zipi zilipekea wewe kukimbilia Scotland na kuishi huko mika 15 bila kutia mguu Tanzania kwa miaka 15!

Tatu, ni kwamba ikiwa ulilipwa kumpigia kampeni Rais wa sasa John Magufuli baada ya kuwa ulikuwa ukimuunga mkono Edward Lowasa, basi hakuna shaka kwamba wewe ni "double agent" na hufai kuaminiwa hata ukielezacho hapa.

"Double agent" mara nyingi anazungumza kwa kutumia lugha ya "double digits" na hawezi kuaminika kwa hilo.

Nne, ukiwa afisa wa zamani hupaswi kuwa na maoni ya kuegemea upande mmoja isipokuwa kama umeanzisha kampuni yako ya kutoa ushauri "consultancy firm" ambapo unalipwa kwa kazi mbalimbali za mikataba iwe serikalini au kwenye shughuli za wateja binafsi na hii ndiyo wanafanya huko Ulaya au Marekani.

Bila shaka kwa uzoefu wako wa kuishi huko Ulaya utakuwa unatambua kuwa ni lazima pia uwe una namba maalum na ukihitajika unakuwa "available" wakati wowote ule.

Tano, suala la vifo vya Daniel John na Aquilina Akwilina ni suala tata na mpaka sasa haijathibitishwa kwamba ni nani alitupa risasi, inaweza kuwa na askari polisi au mhuni yoyote yule alieshiriki zile ghasia.

Sita, wewe umeishi Scotland kwa miaka 15 unaona ni sawa kufanya maandamano yasiyo na kibali tena majira ya jioni?

Kwa maana huko wenzetu wanafuata taratibu na sheria za kufanya maandamano bila tatizo lolote.

Mbona umeandika kama vile mtu ambae hujaishi Scotland kwa miaka 15?

Maana hata rais Magufuli mwenyewe akisoma hapa atakushangaa sana.

Sasa tukirudi kwenye hoja yako ya msingi kwamba rais John Magufuli anaipeleka nchi kusikofaa naona kama umetoa hukumu kwa kesi ambayo bado hata haijafika mahakamani.

Watu 40 wamekamatwa wakiwamo polisi 6 na uchunguzi bado waendelea maana ni lazima apatikane yule alietumia bunduki kutupa risasi.

Mimi ni mmoja wa watu ambao tunapenda kuongea kwa kutumia "facts" na kama huna "facts" basi unasubiri.

Lakini mojawapo "facts" zilizopo ni kwamba waloandaa maandamano yafanyike jioni tena bila kibali ni Freeman Mbowe na voiongozi wengine wa Chadema.

Pili, ni makosa ya jeshi la polisi kutumia silaha za moto badala ya maji, mabomu ya kutoa machozi au risasi za bandia hivyo kuwaweka katika wakati mgumu wa kujitetea kama wao si wauaji wa yule binti.

Ulipaswa kuandika kwa kuonyesha uwiano wa lawama zako na sio kuegemea moja kwa moja upande mmoja.

Ukifanya hivyo unakuwa unaondoa sifa ya kuwa na uwezo wa kufikiria mambo kwa undani na kuyafanyia utafiti kabla ya kuyazungumza.

Na hiyo sio sifa ya wanajumuiya wa zamani.
Wewe ni mnafki,kila maandamano yana sababu zake na maandamano ni haki ya kikatiba,na je sababu ya maandamano no IPI?
 
Pengine sauti za watu kama nyinyi akina Everist Chahali itasaidia. Kuna ndoa ya usalama wa taifa (taasisi yako uliyoitumikia) na usalama wa CCM. Bahati mbaya hakuna udhibiti wa kutosha na umo ndani kunazalishwa 'rogue groups'. Bahati mbaya Rais wetu wa sasa (na waliopita) hawana moral authority ya kukemea na kuyatatua. Ukitaka kujua tuna tatizo kubwa zungumza hata na ofisa mkubwa tu wa JWTZ. Kuna mmoja aliwahi kusema vyama vya upinzani haviwezi kushinda kwa sababu havina 'Jeshi'. Kwa maana hiyo anafikiria JWTZ ni jeshi la CCM!
 
Ndio maana Kenya wanatuuita, "The Sleeping Giant". Watu badala ya kujadili hoja za mtoa mada wao wanamjadili mtoa mada.

Kipi alichokisema ambacho hakiaksi ukweli. Kama alimuunga Magufuli kipindi hicho kwa kudhani alikuwa ni 'Presidential Material' lkn sasa anaona yuko tofauti, sasa asiseme? Na yeye hataki kuwa mnafiki kama walivyo wa Tz wengi, what's wrong with that?

Tuheshimu uhuru wa watu kuwa na maoni tofauti.
 
"Pili, mwaka 2015 nilishiriki kikamilifu katika kampeni zilizomwingiza madarakani Rais John Magufuli. Kwa upande mmoja nililazimika kumkampenia Magufuli kwa vile nilikuwa nina "sababu binafsi" dhidi ya aliyekuwa mpinzani wake mkuu, mgombea urais wa tiketi ya UKAWA, Edward Lowassa. Wanasema "adui ya adui yako ni rafiki yako."Kwa upande mwingine, nililipwa kutoa huduma ya ushauri wa kitaalamu (usadi, yaani consultancy kwa kimombo) hususan kwenye mitandao ya kijamii. Natanabaisha hili ili asije akakurupuka mtu na kusema "ah ulishiriki kutupigia kampeni kwa vile tulikupa pesa.""

Kumbe huyu jamaa nguvu zote zile kumpigia kampeni Magufuli, kisa Lowassa kujiunga UKAWA, alikuwa amevuta. Ghafla tone yake ilibadilika, alikuwa mtu critical, mara akaanza kumsifia Magufuli na maCCM. Tulimshangaa na akaishia kutu-block kule Twitter. Kumbe alilipwa bana. It makes sense now. Hata Mzee Mwanakijiji na Dr. Slaa ni wa mkumbo huo huo. Walilipwa kumpigia kampeni Magufuli na kudhoofisha harakati za upinzani/UKAWA.
Huyu jamaa hata mimi aliniblock twitter kutokana na uchaguzi 2015 nilikua sielewi kwann aligeuka ghafla kumbe alivuta mpunga
 
Mange,kuwa makini na huyu mtu anaejiita Evarist Chahali,usije ukamuamini ukadhani anania moja na wewe otherwise you are a dead meat.

Hawa walioko huko ulaya,watajidai kuiponda serikali kama njia moja ya kuikumbusha sr.kali hii dhalimu kuwa niwakati wake kuingia kazini.
Kwamba yupo,na yupo tayari kutumika,,,kaa chonjo wafwaaaaa
 
Mnafiki katika ubora wako. Wewe na Mwanakijiji mlimfanyia kampeni Magufuli leo mnalalamika nini? Tulieni dawa iwaingie kisawa sawa
 
Chachali umenena vyema kabisa, binafsi ninaona sasa ni wakati muafaka kwa bunge kufanya marekebisho ya sheria ili kuondoa mfumo wa vyama vingi nchini,,, maana kuna kila dalili ya maambukizi ya chuki miongoni mwa watanzania kwa sababu ya vyama hivi vya siasa ambavyo watawala hawavihitaji kabisa katika nafisi zao.
 
Back
Top Bottom