Evarist Chahali: Kila mwenye mapenzi ya dhati na Tanzania amwambie Magufuli "unaipeleka nchi kusikofaa"

Ukyakya

Senior Member
Jun 17, 2013
183
208
Andiko hili ni zito, limeandikwa na Evarist Chahali, Ofisa Usalama wa Taifa wa Zamani. (LISOME KWA UTULIVU).
_______________________________________

Kila Mwenye Mapenzi Ya Dhati na Tanzania Amwambie Magufuli "Unaipeleka Nchi Kusikofaa"

Tarehe 18 Februari 2018.

Nianze makala hii kwa kutoa salamu zangu za pole kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki wa marehemu Daniel John, ambaye hadi alipouawa kinyama alikuwa Katibu wa Chadema kata ya Hananasifu, na pia kwa familia, ndugu,jamaa na marafiki wa marehemu Acqulina Akwilin (samahani kama nimekosea jina).

Kwa mujibu wa maelezo yaliyotolewa na Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe, mwili wa marehemu Daniel uliokotwa kwenye ufukwe wa Coco jijini Dar es Salaam ukiwa na majeraha. Alieleza kuwa awali marehemu alichukuliwa na Land Rover nyeupe na watu waliohifanya askari polisi, lakini tangu wakati huo Polisi hawakuwa na taarifa zozote za kiuchunguzi, na hata jitihada za kupatikana mwili huo zilifanywa na Chadema wenyewe.

DAR: Katibu wa Kata ya Hananasifu(CHADEMA) afariki dunia katika mazingira yenye utata. Mwili wake umekutwa ukiwa na jeraha la Panga kichwani

> Mwenyekiti wa CHADEMA, @freemanmbowetz amelitaka Jeshi la Polisi kufanya uchunguzi | Soma Mbowe ataka uchunguzi kifo cha kiongozi wa CHADEMA, Daniel John pic.twitter.com/KLJ2vstMBL
— Jamii Forums (JamiiForums) February 14, 2018

Kwa upande wa marehemu Acquilina, kifo chake kilisababishwa na kasumba hatari inayozidi kuzoeleka kwa watumishi wa vyombo vya dola kufanya mzaha katika matumizi ya silaha za moto, ambapo katika tukio husika, polisi waliokuwa wakizuwia maandamano ya wafuasi wa Chadema, walitumia risasi za moto,na moja kati ya risasi hizo ilipelekea kifo cha binto huyo, ambaye hadi mauti yanamfika alikuwa mwanafunzi katika Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) akisomea shahada ya ununuzi na ugavi.

Mwanafunzi afariki baada ya kupigwa risasi Tanzania Mwanafunzi afariki baada ya kupigwa risasi Tanzania
— bbcswahili (@bbcswahili) February 17, 2018

Ni muhimu kutambua kuwa vifo vyote hivi viwili vingeweza kuepukika laiti utu na ubinadamu wetu ungewekwa mbele ya chuki za kisiasa. Huhitaji kuwa mjuzi wa uchunguzi wa mauaji kufahamu kuwa vifo hivyo ni matokeo ya chuki, hujuma, uonevu na kila aina ya baya dhidi ya chama kikuu cha upinzani, Chadema, kuhusiana na kampeni za uchaguzi mdogo katika jimbo la Kinondoni, ambalo kama ilivyo kwa jimbo la Siha, ni "piga ua" kwa CCM ishinde. Yaani chama hicho tawala kilitarajiwa kutumia kila mbinu kuhakikisha inashinda katika majimbo hayo mawili.

Lakini kabda sijaingia kwa undani katika mada hii - ambayo lazima nikiri kwamba inanipa wakati mgumu sana kuiandika kwa sababu nimebanwa na mchanganyiko wa majonzi na hasira, sambamba na hofu ya kuona taifa langu likisukumwa kuelekea kwenye upotevu wa amani na mshikamano wetu – naomba kuweka wazi masuala matatu ya msingi kunihusu mie mwandishi wa mwakala hii.

Kwanza, mimi licha ya kuwa na makazi nje ya Tanzania kwa takriban miaka 15 sasa bado no Mtanzania. Utanzania wangu ni haki nilioirithi kutoka kwa wazazi wangu, na itabaki hivyo milele. Naeleza hili kwa sababu kuwa wabaguzi wanaopenda kutuhukumu Watanzania tunaoishi huku ughaibuni, na kutaka tuonekane kama Utanzania wetu sio kamili. Kwa mantiki hiyo, kama Mtanzania, nina kila haki ya kutoa maoni yangu kuhusu mustakabali wa taifa letu, hususan katika nyakati hizi ambapo kuna dalili za wanaotaka kulipeleka kubaya taifa letu.

Pili, mwaka 2015 nilishiriki kikamilifu katika kampeni zilizomwingiza madarakani Rais John Magufuli. Kwa upande mmoja nililazimika kumkampenia Magufuli kwa vile nilikuwa nina "sababu binafsi" dhidi ya aliyekuwa mpinzani wake mkuu, mgombea urais wa tiketi ya UKAWA, Edward Lowassa.

Wanasema "adui ya adui yako ni rafiki yako."Kwa upande mwingine, nililipwa kutoa huduma ya ushauri wa kitaalamu (usadi, yaani consultancy kwa kimombo) hususan kwenye mitandao ya kijamii. Natanabaisha hili ili asije akakurupuka mtu na kusema "ah ulishiriki kutupigia kampeni kwa vile tulikupa pesa."

Tatu, huko nyuma nilikuwa mtumishi wa Idara ya Usalama wa Taifa. Na kabla ya kuanza utumishi katika taaluma hiyo muhimu na nyeti, nilikula kiapo kwa nchi yangu, kiapo ambacho nitaishi nacho hadi ninaingia kaburini. Kiapo hicho sio cha kukitumikia chama flani au viongozi wake bali Tanzania yetu. Nchi ni muhimu kuliko vyama vya siasa au wanasiasa.

Mtu aliyepikwa na kuiva kwenye taaluma ya uafisa usalama wa taifa, katika nchi yoyote ile, anapaswa kubaki kuwa mtiifu kwa nchi yake bila kujali yupo ndani au nje ya ajira ya taasisi inayohusika na usalama wa taifa wa nchi husika.

Wanasema hata nje ya ajira rasmi, kila mtu aliyewahi kuwa afisa usalama wa taifa anaendeshwa na "sense of public duty born in their previous lives" yaani wajibu kwa umma uliozaliwa katika maisha yao huko nyuma. Jasusi mmoja mstaafu anaeleza “...I have obligations, professional obligations. If there’s a national security emergency or possible national security issue, I should report it."

“ ‘You know, I have obligations, professional obligations. If there’s a national security emergency or possible national security issue, I should report it.’ ” ~ Steele
— Evarist Chahali (@Chahali) February 8, 2018

Kwahiyo, hata kama "maafisa wenzangu wa zamani" wataamua kukaa kimya kwa sababu moja au nyingine – wengi wanahofia usalama wa maisha yao – sie wengine hatuwezi kukaa kimya, hasa kwa vile baadhi yetu tumeshalipa gharama kubwa kwa kelele zetu. Kukaa kimya ni sawa na kuafiki uhuni unaoendelea ambao ni tishio kwa usalama wa taifa.

Lakini licha ya wajibu huo unaotokana na utumishi wetu kwa nchi huko nyuma, Rais Magufuli amefanikiwa kuvifunga mdomo vyombo vya habari kiasi kwamba haviwezi kusema lolote kuhusu "mabaya" yake, na amefanikiwa kuvijengea nidhamu ya uoga vyombo hivyo vya habari kiasi kwamba habari pekee zenye umuhimu kwao ni za kumtukuza na kumpamba "mungu-mtu" huyo.

Kwahiyo na sie tuliopikwa na kuiva kuhusu ujasiri, kujitoa mhanga na kutokuwa waoga tukiufyata na kukaa kimya - ilhali media zetu ndio zishapigwa kufuli - hali itazidi kuwa mbaya.

Rais wa Tanzania John Magufuli ayaonya baadhi ya magazeti nchini humo IDHAA YA KISWAHILI | DW
— DW (Kiswahili) (@dw_kiswahili) January 13, 2017

Baada ya kuweka wazi nafasi yangu, sasa tuangalie kwa kina kinachoendelea huko nyumbani hasa kuhusiana na uchaguzi mdogo kwenye jimbo la Kinondoni na Siha na kuuawa kwa Daudi na Acquiline.

Ni muhimu kutambua kwamba ukandamizaji dhidi ya vyama vya upinzani sio kitu kilichoanza chini ya utawala wa Magufuli bali hali hiyo imedumu mfululzo tangu kuanzishwa kwa mfumo wa siasa za vyama vingi mwaka 1992. Labda kilicho tofauti kwa zama hizi ni "ujasiri" wa Magufuli kutoficha chuki yake dhidi ya vyama vya upinzani. Yaani angalau akina Mwinyi,Mkapa na Kikwete walikuwa "wanauma na kupuliza." Kwamba angalau walikuwa na "mshipa wa aibu" na walijitahidi japo kutowaonea Wapinzani waziwazi.

Kwa wanaojua "yanayojiri nyuma ya pazia" watakwambia kuwa hujuma dhidi ya vyama vya upinzani ni miongoni mwa vipaumbele vikubwa kwa CCM na serikali zake, na hiyo imepelekea kujengeka "symbiotic relationship" kati ya chama hicho tawala na taasisi za dola, ambapo kila mmoja anategemea uhai wa mwenzie.

Lakini kama kuna kitu kinachokera zaidi kuhusu hujuma dhidi ya demokrasia ni pale CCM na taasisi zake hasa za dola wanapoweka mbele maslahi yao mbele ya utu na uhai wa Watanzania. Na hili halijaanza jana au katika kampeni za chaguzi ndogo katika majimbo ya Kinondoni na Siha.

Uchaguzi mkuu wa kwanza wa vyama vingi mwaka 1995 ulihusisha matukio mengi tu ambayo kwa makusudi hayapo kwenye kumbukumbu za wazi (japo yamehifadhiwa mahala flani).

Lakini kama wanavyosema "amekula asali sasa anachonga mzinga," baada ya hujuma za kimyakimya za mwaka 1995 kuzaa matunda, CCM na taasisi zake ikanogewa, na matokeo yake ni kwamba uchaguzi mkuu uliofuata, mwaka 2000 uliweka doa kubwa kwa historia ya Tanzania yetu ambapo kwa mara ya kwanza nchi yetu ilizalisha wakimbizi kufuatia unyama uliofanyika huko Zanzibar na kupelekea vifo kadhaa (idadi halisi ya vifo haijawahi kuwekwa hadharani japo "wenyewe" walisema zaidi ya watu 19 ndio waliokufa kwenye machafuko hayo. Wasichosema pia ni idadi ya watu waliobakwa, kuteswa na kuwekwa kizuizini.

Kwamba hujuma hizo za CCM dhidi ya demokrasia zilipelekea vifo na majeruhi ni kitu kibaya kabisa. Lakini kitu kingine kibaya ni ukweli kwamba hakuna mtu hata mmoja aliyechukuliwa hata kutokana na unyAma waliofanyiwa Wazanzibari hao.

Kwa namna ya kipekee, CCM ikawa kama imepewa ruhusa ya kutumia vyombo vyake vya dola kufanya lolote itakalo ili ifanikishe hujuma zake dhidi ya Wapinzani na demokrasia kwa ujumla, kisha iibuke na ushindi.

Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005 ulikuwa na "uchafu kupindukia." Kundi lililofahamika kama "mtandao" lilijipenyeza katika kila sekta, kuanzia kwenye vyombo vya habari, taasisi za dola hadi kwenye taasisi za dini. Yayumkinika kabisa kuhitimisha kwamba yaliyojiri wakati "mtandao unafanya jitihada za kumwingiza mtu wao Ikulu" ni mabaya zaidi ya haya tunayoshuhudia sasa tangu Magufuli aingie madarakani.

Kwanini basi hayo yaliyojiri kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2005 hayajulikani? Jibu ni kwamba, wakati mbinu iliyotumika mwaka 1995 na 2000 ilitegemea zaidi vyombo vya dola, uchaguzi wa mwaka 2005 na 2010 ulitegemea zaidi nguvu ya fedha, nyingi zikiwa fedha haramu. Na sehemu ya fedha hiyo ilitumika "kununua ukimya" wa wanahabari wengi tu.

Lakini si fedha tu bali pia kuna hujuma mbalimbali – nyingine chafu na za kuchefua – zilizotawala safari za ushindi wa chama tawala kwenye chaguzi hizo.

Image result for lowassa kikwete 2005

Labda tofauti nyingine kuhusu mwaka 2005 na 2010 ni ukweli kwamba wakati chaguzi hizo zilihusisha "kikundi binafsi" yaani hicho cha wanamtandao ambacho hakikuwa taasisi ya serikali au chama.

Lakini muda wote huo, CCM ilikuwa kama imepwa ruhusa na Watanzania kuendeleza hujuma zake dhidi ya Wapinzani na demokrasia kwa ujumla. Hakujawahi na utashi miongoni mwa Watanzania kutaka kukabiliana kwa dhati za uhuni/uhalifu wa kisiasa. Na kwa bahati mbaya, kwa vile vipaumbele vya Watanzania wengi ni kwenye "ubuyu" na "kubeti/mkeka" basi habari mbaya ni uwezekano wa CCM kuendelea kufanya itakavyo kwa muda mrefu sana.

Sio kama kwa kubashiri kuwa unyanyasaji wa CCM utaendelea muda mrefu sana ninamaanisha kuwa nimekata tamaa. Hapana. Ninakuwa mkweli tu. Tatizo ni zaidi ya CCM na uhuni wake. Watanzania wenyewe ni sehemu ya mfumo unaowezesha CCM kufanya uhuni/uhalifu huo.

Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 ulihusisha pia matuki kadhaa yaliyojiri "nyuma ya pazia." Na ukitaka kufahamu kuwa Tanzania yetu haijawahi kuhangaishwa na mauaji ya kisiasa – kuanzia yale ya mwaka 2001 huko Zanzibar hadi haya ya Daudi wa Hananasifu na dada Acquilina – ni kifo cha Mchungaji Christopher Mtikila.

Mchungaji Mtikila afariki kwa ajali ya gari Chalinze mkoani Pwani | Soma FikraPevu | JamiiForums' News Site [HASHTAG]#RIPMtikila[/HASHTAG] pic.twitter.com/HoNnzkjy3w
— FikraPevu (FikraPevu) October 4, 2015

Kwahiyo, na ninaandika haya kwa uchungu mkubwa uliochanganyika na hasira, kuuawa kwa Daudi na Acquilina kutaishia kuwa moja tu ya matuko yaliyowahi kutokea katika Tanzania yetu. Tutawasikia wanasiasa wetu wa vyama vya upinzani wakiongea kwa hisia kubwa.

Tutashuhudia pia wanafiki wengi tu miongoni mwa wasanii wetu nao wakijifanya kuguswa na vifo hivyo, lakini wakiwa makini kuepuka kumuudhi "Bashite na baba yake" au kuitibua CCM. Tutashuhudia pia kundi la wanafiki hatari ndani ya CCM wakijifanya kuumizwa na mauaji hayo, na kutaka uchunguzi ufanyike, ilhali nao ni kondoo waliojivika ngozi ya mbwa mwitu.

Cheap politics + unafiki. Mbwa mwitu wanaojivika ngozi ya kondoo. Inapofika wakati wa kujitoa mhanga kwa minajili ya kuondoa mfumo kandamizi, hawa wanafiki huonyesha rangi yao halisi na kujivika ukada. Tanzania Updates on Twitter
— Evarist Chahali (@Chahali) February 17, 2018

Bora tu JPM au Polepole ambao wapo honest kuhusu chuki zao kwa Upinzani/Wapinzani kuliko wanafiki "wanaouma na kupuliza." Bora maadui milioni kuliko "rafiki" mmoja mnafiki Tanzania Updates on Twitter
— Evarist Chahali (@Chahali) February 17, 2018

Kama ambavyo "mauaji mengine ya kisiasa" yalivyoruhusiwa kupita kimyakimya, ndivyo unyama huu uliofanywa dhidi ya Daudi na Acquilina utakavyoruhusiwa uishe kimyakimya.

Kwa upande mmoja tusitarajie Rais Magufuli awajibike – sio kwa yeye binafsi kujiuzulu kwa sababu hilo litakuwa kutarajia zaidi ya muujiza – kwa kumtimua Waziri husika na watendaji katika jeshi la polisi. Kwa upande mwingine, hakuna wa kumshinikiza Rais Magufuli achukue hatua stahili dhidi ya wahusika.

Na nisingependa kuuma maneno hapa. Yeye Magufuli mwenyewe ni chanzo muhimu cha siasa hizi za uhasama zinazoendelea kuitafuna Tanzania yetu. Huyu ni mtu ambaye wala hapati shida kuonyesha chuki zake za waziwazi dhidi ya Wapinzani, Upinzani na demokrasia kwa ujumla.

Tufike mahala tuambiane ukweli: @MagufuliJP anaipeleka Tanzania kusikostahili. And that is too bad. But what's even worse ni kwamba asilimia kubwa ya Watanzania wanasubiri miujiza, kwamba siku moja huyu bwana atabadilika. He won't. Worse is yet to come (God forbid)[HASHTAG]#MarkThisTweet[/HASHTAG] pic.twitter.com/Uy3VnkOKOH
— Evarist Chahali (@Chahali) February 17, 2018

Kama ilivyo kwa madikteta wengine duniani, Magufuli amefanikiwa kwa kiasi kikubwa kutumia ajenda yake ya ufisadi kama kisingizio cha kusigina haki za binadamu nchini Tanzania, na kubinya kila fursa ya haki za kidemokrasia na uhuru wa habari. Kama nilivyoeleza awali, amefanikiwa kuviziba midomo vyombo vya habari na ndio maana hata habari za kusikitisha kuhusu mauaji ya Daudi na Acquiline hazijaripotiwa vya kutosha.

Kwa kuviziba midomo vyombo vya habari Magufuli amefanikiwa kuzuwia "habari asizozipenda" na ndio maana hadi muda huu ni Watanzania wachache tu wanaofahamu kilichojiri huko MKIRU katika kilichoitwa "operesheni dhidi ya ugaidi." Kuna siku yaliyojiri huko – na ambayo yamechangia "kupotea" kwa mwandishi wa gazeti la Mwananchi Azory Gwanda – yatajulikana hadharani. Haijalishi itachukua miaka mingapi.

Baraza la Habari Tanzania (MCT) limesema mwandishi wa Mwananchi aliyetekwa, Azory Gwanda alikuwa anafuatilia taarifa za mauaji ya chini kwa chini yaliyokuwa yanaendelea Kibiti

> Wanadhani mazingira haya ndio yatakuwa yamepelekea usalama wake kuwa hatarini#JFLeo pic.twitter.com/HPsQzmc3XI
— Jamii Forums (JamiiForums) December 9, 2017

Lakini "yaliyojiri MKIRU" ni uthibitisho mwingine wa hicho nilichoeleza hapo juu kuwa Watanzania wenyewe ndio wanaopaswa kubeba lawama nyingi katika kasumba ya CCM kutojali uhai katika harakati zake za kukandamiza demokrasia. Kwamba kama yaliyojiri MKIRU yameachwa yaishe kienyeji, kwanini tutegemee hali tofauti kwa vifo vya Daudi na Acquiline?

Kama ndugu zetu wa Chadema (na kila mpenda haki) "wamekubali yaishe" kuhusu kifo cha Kamanda Mashaka, "kupotea" kwa kada Ben Saanane (hata zile kampeni za [HASHTAG]#BringBackBenAlive[/HASHTAG] zimejifia kifo cha asili), na hawasumbuliwi na serikali ya Magufuli kupuuzia jaribio la mauaji dhidi ya Tundu Lissu, kwanini tutarajie jipya katika mauaji yaliyofanywa dhidi ya Daudi na Acquiline?

Yaani Mnadhimu Mkuu wa upinzani anamwagiwa risasi hadharani wakati mkutano wa bunge unaendelea huko Dodoma, na tunaambiwa kuwa tukio hilo lilitokea katika eneo lenye ulinzi mkubwa na lenye CCTV, kwanini basi wanaosumbuliwa na tukio hilo wasitafute njia stahili za japo kuifanya serikali ione aibu na kufanya japo "uchunguzi wa kizushi"?

Kuhusu hujuma "za kawaida" za uchaguzi, kama kila aina ya uhuni uliofanywa na CCM kwenye chaguzi ndogo za madiwani katika kata 43 uliofanyika Novemba mwaka jana uliruhusiwa upite "kimya kimya" – kwa maana kwamba hakuna hatua zozote zilizochukuliwa dhidi ya uhuni huo – kwanini basi chaguzi hizi ndogo katika jimbo la Siha na Kinondoni zilitarajiwa kuwa tofauti?

Na katika hili, inapaswa wana-Chadema wajiulize kuhusu busara za viongozi wao kuamua kushiriki katika chaguzi hizo ndogo Siha na Kinondoni ilhali mazingira yaliyokuwepo yalikuwa yaleyale yaliyopelekea chama hicho kususia chaguzi nyingine ndogo tatu katika majimbo ya Longido, Singida Kaskazini na Songea Mjini uliofanyika mwezi uliopita.

Hadi wakati ninaandika makala hii, tayari Tume ya Uachaguzi ilikuwa imeshamtangaza mgombea wa CCM jimbo la Siha, Godwin Mollel kuwa mshindi kwa tofauti kubwa tu ya kura dhidi ya mgombea wa Chadema. Hata kama CCM wameiba kura, ukubwa wa tofauti kati ya kura za mgombea wao na huyo wa Chadema zinaashiria kuwa chama hicho kikuu cha upinzani kilipitisha mgombea fyongo.

Mgombea wa CCM, Dk Godwin Mollel ametangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuwa mshindi wa Ubunge Jimbo la Siha baada ya kupata kura 25,611 dhidi ya mpinzani wake, Elvis Mosi wa CHADEMA aliyepata kura 5,905 - Mwananchi pic.twitter.com/hG6oT9GUpZ
— Kwanza TV (@kwanza_tv) February 18, 2018

Na kama ilivyotarajiwa mgombea wa CCM jimbo la Kinondoni, Maulid Mtulia, naye ametangazwa mshindi.
Breaking news: Aliyekuwa Mgombea Ubunge kwa ticket ya CCM, Maulid Mtulia ametangazwa kuibuka mshindi katika uchaguzi mdogo wa marudio wa Jimbo la Kinondoni.
Mtulia amepata kura 30,313 dhidi ya mpinzani wake Salum Mwalim (CHADEMA) aliyepata kura 12,353#MillardAyoUPDATES pic.twitter.com/rYsb0Jgbie
— millardayo (@millardayo_) February 18, 2018

Mie mtumishi wako nilishabashiri mapema tu kuwa chama hicho tawala kingeshinda majimbo hayo, "iwe isiwe."

Ushindi kwa wagombea hao wa CCM ulipaswa kupatikana kwa gharama yoyote kwa sababu laiti wangeshindwa, kinachoelezwa kama "mkakati wa Magufuli kuua upinzani kwa kununua wabunge na madiwani wa Upinzani" kingemfanya achekwe hata huko kwenye chama chake.

Na kwa vile hadi sasa wabunge na madiwani waliohama upinzani na kujiunga na CCM wamefanikiwa kurudi madarakani baada ya chama hicho tawala kuwapa fursa ya kuwa wagombea wake kwenye chaguzi ndogo, na kuwasaidia kwa hali na mali washinde, tutarajie wabunge na madiwani wengin zaidi kuhama vyama vya upinzani na kujiunga na CCM. Kisa? "Dili hilo linalipa," kwa CCM na kwa wanasiasa hao wanaohama.

Na unadhani mbunge au diwani "mwenye moyo mwepesi" akiona jinsi chama chake "kilivyochukulia poa" yaliyowasibu akina marehemu Mashaka na Daudi, na yaliyowasibu Ben Saanane na Lissu, kwanini iwe ngumu kwake kushawishika kuhama?

Ningetamani sana kuhitimisha makala hii kwa kushauri nini kifanyike lakini itakuwa kupoteza muda wangu na muda wako msomaji. Ni vigumu mno kuwashauri watu waliokubali kwamba mgao wa umeme ni stahili yao kwa zaidi ya miaka kumi sasa, na ambao kila mara umeme unaporudi wanashangilia kana kwamba wamepewa upendeleo flani.

Kama Watanzania wameshindwa kuilazimisha Tanesko iache mgao wa umeme, wataweza kweli kuilazimisha CCM iache hujuma dhidi ya vyama vya upinzani na demokrasia kwa ujumla? Ndio maana bila utu wala aibu, chama hicho tawala kinapata ujasiri wa kukifanyia mzaha kifo cha Acquiline ambapo kwa kudai polisi (haohao waliomuua binti huyo) wachukue hatua dhidi ya Mbowe. Utterly disgusting!

@ccm_tanzania This is too low. Kwanini msitumie akili badala ya makalio kutambua mnachofanyia mzaha huu ni uhai wa Mtanzania uliokatishwa kinyama na polisi haohao mnaowapa kinga kwa kumsingizia @freemanmbowetz? Hamna utu wala mshipa wa aibu? Mungu awalaani kwa hili
cc @MagufuliJP pic.twitter.com/7lgzKh0ofe
— Evarist Chahali (@Chahali) February 18, 2018

Na kama mauaji mbalimbali ya kisiasa huko nyuma yameachwa yapite na kusahaulika, kwanini tutarajie miujiza kwenye mauaji haya ya sasa dhidi ya wapendwa wetu Daudi na Acquline?

Na ukweli mchungu ni kwamba Magufuli ataendelea kuwapelekesha Watanzania atakavyo ka sababu si watangulizi wake -Mwinyi, Mkapa na Kikwete – wenye jeuri ya kumwambia "Ee bwana ee, huku unakoipeleka nchi siko." Hawawezi kwa sababu nao ni kama "mateka." Madhambi waliyofanya kwenye tawala zao yanawafanya wahofie hatma yao pindi wakimkosoa "mungu-mtu" aliyepo madarakani.

Na wakati wastaafu au watumishi wa zamani wa Idara za Usalama wa Taifa kwenye nchi kama Marekani wamekuwa mstari wa mbele kukemea kila tendo linalotishia usalama wa nchi hiyo – kwa mfano 'ndoa' kati ya Rais Donald Trump na Russia – wastaafu wetu sie hawana jeuri ya kufungua mdomo sio tu kwa vile wanahofia kuathiri posho na marupurupu yao bali kwa vile nao ni mateka wa "madudu" waliyofanya walipokuwa madarakani. Ukiwa mchafu unajinyima uhuru wa kukemea uchafu.

James Comey mkuu wa zamani wa FBI na John Brennan mkuu wa zamani wa CIA ni miongoni mwa sauti muhimu kuhusu mustakabali wa taifa la Marekani. Wako wapi "akina Comey na Brennan" wetu kuhusu mustakabali wa Tanzania yetu? pic.twitter.com/DSA0mWYZ8A
— Evarist Chahali (@Chahali) February 17, 2018

Basi niishie hapa kwa kurejea tena salamu zangu za pole kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki wa marehemu Daudi na Acquiline. Ni vigumu kuwaambia maneno yanayotosha kuwaliwaza lakini la muhimu ni kuendelea kuzikumbuka roho za marehemu hao, hasa katika kipindi hiki cha Kwaresma ambapo sisi Wakristu tunaadhimisha mateso ya Bwana Yesu Kristo. Pumziko la Milele awape Bwana, na Mwanga wa Milele awaangazie, wapumzike kwa amani. Amen

[HASHTAG]#Credit[/HASHTAG] to #Evarist_Chahali
 
"Pili, mwaka 2015 nilishiriki kikamilifu katika kampeni zilizomwingiza madarakani Rais John Magufuli. Kwa upande mmoja nililazimika kumkampenia Magufuli kwa vile nilikuwa nina "sababu binafsi" dhidi ya aliyekuwa mpinzani wake mkuu, mgombea urais wa tiketi ya UKAWA, Edward Lowassa. Wanasema "adui ya adui yako ni rafiki yako."Kwa upande mwingine, nililipwa kutoa huduma ya ushauri wa kitaalamu (usadi, yaani consultancy kwa kimombo) hususan kwenye mitandao ya kijamii. Natanabaisha hili ili asije akakurupuka mtu na kusema "ah ulishiriki kutupigia kampeni kwa vile tulikupa pesa.""

Kumbe huyu jamaa nguvu zote zile kumpigia kampeni Magufuli, kisa Lowassa kujiunga UKAWA, alikuwa amevuta. Ghafla tone yake ilibadilika, alikuwa mtu critical, mara akaanza kumsifia Magufuli na maCCM. Tulimshangaa na akaishia kutu-block kule Twitter. Kumbe alilipwa bana. It makes sense now. Hata Mzee Mwanakijiji na Dr. Slaa ni wa mkumbo huo huo. Walilipwa kumpigia kampeni Magufuli na kudhoofisha harakati za upinzani/UKAWA.
 
Wameongezeka sio hao wawili tu, wapo akina Mawazo Alphonce (wauwaji wake wanafahamika naskia), Daudi Mwangosi (mmuwaji yake anajulikana), Wapo wale watoto wa Arusha kwenye Mkutano wa CHADEMA walipopigwa bomu!!! Wapo wengi na inavyoelekea watakua wengi zaidi, hizi ni reported cases kwenye matukio ambayo hayana kificho, kuna wale wa baharini na kuna wale wa......MUNGU ibariki Tanzania.
 
Huwezi zuia asubuhi kupambazuka
Ulaya na America zimejengwa kwa jasho la damu na vifo vya walimwengu. Ntakua sijakosea nikisema this is the natural way of human development. Ila kwa kua majira na nyakati ubadirika, hatuna budi kuamini the new begining is yet to come under the expence of milions of death and torturing.
 
everest Chahali
Ukyakya
Wakuu,
Poise, ni mtanzania, naishi New Zealand naipenda nchi yangu Tanzania mno mno na nimetumikia sehemu nyingi za nchi yetu na nje ya nchi.
Sijawahi kuwa na sitakuwa mwanachama wa chama chochote kile cha siasa hapo Tanzania wala sehemu nyingine ile hapa duniani.
Hivyo, niliandika humu JF platform naandika pasipo ubaguzi au kuegemea upande wowote wa chama.

Ila sasa its time for CCM to go...

Kifo cha kikatili cha Binti yetu , Akwilina A.B, asiye hatia, asiye mfuasi wa chama cha siasa ni chachu tosha kabisa ya kuiondoa na kusema kuwa CCM must go...

Tunaomba , management ya NEC na DED wa kinondoni watumbuliwe, wakamatwe na wafungwe.

Polisi ni kweli wametumia nguvu kubwa ila , wasitolewe kafara hasa hao polisi 6 waliotajwa kuwa watachukuliwa hatua.
Tunaomba walio waagiza kuzuia msafara wa Mr. Mbowe ndiyo wachukuliwe hatau stahiki.

Mr. Mbowe na wanachama zaidi ya 40+ wa CDM waachiwe au wasisumbuliwe kwa sababu, wauaji wa Binti Akwilina A. B, wote wanajulikana kuwa ni watu wa ngazi za juu wa serikali ya CCM kuanzia DED wa Kinondoni, Management ya NEC na wengine sitawataja.

Viongozi wa serikali waache unafiki na uhuniuhuni tu wa kutoa pole kwa watanzania wenzentu kupitia social media platform kama Instagram, Facebook WhatsApp na mitandao mingine siijui majina yake.
Bali njia rasmi za serikali zitumeke kutoa pole kwa watanzania wenzentu mfano, gazette, radio, barua zenye nembo ya taifa na anwani ya ofisi husika au luninga ili hadi Bibi na Babu kule Nanjilinji , katoke, Kishumundu waweze kusikia pole hizo.

CCM must go...

Kagame must be stopped visiting Tanzania (Huyu ndiye adui wa nje wa watanzania wenzentu ambaye amekaribishwa na kuwa adui mara mbili yaani adui wa ndani na nje ya nchi ya Tanzania)

R.I.P Binti yetu Akwilina A. B,
Ndoto zako zote zimezimwa ghafula kama vile mshumaa uzimwavyo.

Daima tutakukumbuka Binti, Kristo Yesu akuangazie mwangaza wake wa milele. Amina.
 
Chahali ni nani?
ni mwanausalama aliyeasi na kukimbilia ukimbizini scotland...mshabiki kindakindaki aliyekuwa ana mpigia debe magufuli na kumkebehi lowassa kipindi cja kampeni ,ila leo ndio anaona magaufuli hafai baada ya kukosa uteuzi, anaogopa kukanyaga nchini kisa idara yake ya zamani inamsaka kwa udi na uvumba siku atikia mguu bongo
binafsi uwa namfananisha na mange kimambi ,uzuri wa chahali hana matusi kama mange
 
Kwanza huwezi kua unaipenda Tanzania akati huna mchango wowote tofauti hizi pumba unazoleta hapa.
 
Swali ambalo tunatakiwa tujiulize watanzania wote ni je tutaendelea kuuliwa na hawa ccm mpaka lini? maana kwa maelezo hayo hapo juu, inaonenakana haya mauji yote yamepangwa, polisi wanatekeleza maagizo tu, na ni mwendelezo wa mauji ambayo yamekuwepo muda mrefu, sasa tufanyeje, maana hatuwezi kuumia kila mwaka kwa ajiri ya watu wachache wafurahie, tuje na mikakati kabambe na iwe sera endelevu kwa watu ambao hatupo kwenye mfumo wa ccm, tujikinge vipi maana sote sio salama tena, sio salama kwa sababu tumezungukwa na wana mfumo hata mitaani kwetu.
 
ni mwanausalama aliyeasi na kukimbilia ukimbizini scotland...mshabiki kindakindaki aliyekuwa ana mpigia debe magufuli na kumkebehi lowassa kipindi cja kampeni ,ila leo ndio anaona magaufuli hafai baada ya kukosa uteuzi, anaogopa kukanyaga nchini kisa idara yake ya zamani inamsaka kwa udi na uvumba siku atikia mguu bongo
binafsi uwa namfananisha na mange kimambi ,uzuri wa chahali hana matusi kama mange


.....Someni basi habari muielewe ndiyo mkimbilie ku comment......''ni mtanzania, naishi New Zealand....''..........Wewe kwenye hiyo bolded red umetoa wapi??
 
Back
Top Bottom