Evarist Chahali: Kila mwenye mapenzi ya dhati na Tanzania amwambie Magufuli "unaipeleka nchi kusikofaa"


Tatizo Tanzania hatuna watu wengi wenye mapenzi na Tanzania. Tuna wengi wasiojua maana ya kuwa na mapenzi na Tanzania, na wengine wengi tu wenye mapenzi na CCM kutokana na historia yake, na wale wenye mapenzi na Magufuli mwenyewe kwa sababu ambazo ni ngumu kwa mtu mwenye akili au asiye mlevi kuelewa.
 
kwani mauwaji yameanza leo, alikuja kikwete mkasema analea mafisadi, mara dhaifu..tumpe mda mh. rais kwani ata yeye binadamu so malaika.
 
Arudishe demokrasia na uhuru wa mihimili.Hii kasi ya fitina inaua umoja wa Watanzania kila uchao.
 
.....Someni basi habari muielewe ndiyo mkimbilie ku comment......''ni mtanzania, naishi New Zealand....''..........Wewe kwenye hiyo bolded red umetoa wapi??
Kwani alojitambulisha kuwa Yuko New Zealand ndo mleta mada? Kasome wewe watu wanazo data mbona mleta mada anajulikana sana tu
 
hata kama huyó chahali hakuasi taifa na alikuwa anasomeshwa huyó kwao ifakara leo anajifanya analipenda taifa kisa umetajiwa nchi tofauti anayoishi je hakulitia hasara taifa kwa kuwa kibaraka wa wazungu kutoa siri za taifa unamtetea
CCM wacheni hujuma. kwahiyo msaliti wa nchi mkamlipa fedha awafanyie kampeni kwenye mitandao?

Kwa jinsi hii mnaonyesha dhahiri nchi imewashinda
 
Kwahio wataka kusema ikifika time fulani wanagawana kama bilioni 3 hivi na maisha yanaendelea, siyo?

Yaani kwa mfano yule gavana wa BOT mzee Florens Luoga ameingia pale baada ya Ndulu kuambiwa apishe jikoni.

Halafu yule Dr Phillip Mpango eti ni jasusi la kutukuka.

Hivyo ikifika time watu wanagawana pesa na yule jamaa wa TRA anaulizwa figures za kila mwisho wa mwezi.

Halafu eti mkulu mwenyewe fikiria, shahada ya kanza DSM, Shahada ya uzamivu DSM na Phd ni DSM, usiidharau sana DSM.

Haya ni maneno yanazungumzwa mitaani hivyo sishangai hayo madai yako.

:D:D:D
Iwe mfia nchi, labda pia ni beneficiary wa mfumo.. Mnapata wapi mabilioni ya kurudia chaguzi tena kwa muda mfupi angali wastaafu mnawaweka bila mafao yao kwa miezi 9 mpaka mwaka?

Tukisema hizo pesa mnagawana unaweza kubisha? Si makusanyo mnasema yameongezeka?
 
Mimi ni rai wa kawaida na mdau kama wewe.

Ila ninayo haki ya kupinga kwa hoja alichoandika ndugu Evarist Chahali.
Wewe kama ni raia wa kawaida rejea ulichokiandika hapo juu ,hivi unaona kila mtu mpumbavu humu ?

Uliposema" Chahali hawezi kuaminiwa na nchi kama unafaa tena kuwa mlinzi wa taifa kutokana na rekodi yako huko nyuma "
Hawezi kuaminiwa wewe ukiwa kama nani unayetoa hiyo kauli

Nani ana access ya rekodi za nyuma za Chahali akiwa TISS ? Au hizo rekodi huwa zinawekwa kwenye public domain ???

Hiyo access ya kujua rekodi za Chahali uko nyuma wewe ulipata wapi ?

Ukasema " Chahali alikuwa ana muunga mkono Lowasa hivyo ni double agent ...naomba unionyeshe ni lini na wapi Chahali aliwahi kumuunga mkono Lowasa


Ukasema "Lazima uwe na namba maalumu na ukihitajika unakuwa available "
Mimi raia wa kawaida haya ya namba maalum siyajui wewe unaesema ni raia wa kawaida umeyajulia wapi ?

Mwisho ukasema "Na siyo sifa za wanajumuhiya wa zamani "

Hizo sifa za wanajumuhiya wewe unaesema ni raia wa kawaida umezijulia wapi ?


Ulicho kiandika hapo ni ili na wewe ujulikane ni afisa muandamizi wa TISS ,

Sawa tumeshakujua then what ?????

Ndio maana hii idara inatakiwa ifumuliwe yote imejaa uchafu tu
 
By 2020 Bunge la ccm pekee halipo salama pia,litapunguzwa say 50% na kubaki bila meno,kama alama tu Kikatiba.
 
Mkuu, Evarist Chahali

Kwanza nipende kukukumbusha kwamba wewe sasa hivi huwezi kuaminiwa na nchi kama unafaa tena kuwa mlinzi wa taifa kutokana na rekodi yako ya huko nyuma.

Na hiyo sio sifa ya wanajumuiya wa zamani.

Nimeishia kusoma hapo kwenye no 5...

Kama na ww umeweza kuamini Aquilina aliuawa na waandamanaji basi kuna tatizo mahali
 
Upo ushahidi wa kutosha Magufuli na makonda wapi kwenye mission ya kuendesha mauaji ukiona mkoa gani watu wanakufa kama kuku hao ndio watoa Amri we never thought kaapishwa banyamulenge

Ni vizuri kama unaamini huo ushahidi upo na unaweza kutumiwa kuwafikisha wahusika mahakamani.
 
Ni muhimu kukemea maovu yote yanayotokea nchini mwetu.

Isitishe ni muhimu pia kukemea mauaji ya Daniel John, msichana Aquilina, mashambulizi risasi kwa mbunge Tundu Lissu na upotevu wa watu wengi kwa kutupwa kwenye viroba.

Pia ni muhimu kukemea utakaji na kupotezwa kwa watu kama Ben Saanane.

Lakini hakuna ushahidi wala majivu ya utekezaji wa ushahidi huo unaoinganisha serikali au kiongozi yoyote yule wa nchi.

Sisi raia tunabakia tu kudhani au kuamini kwamba ni wao wanahusika.

Freeman Mbowe siku zake za kubainika uovu anaoutenda na uhuni wake wote zinakaribia.

Tutakuja tena hapa kutoa ushuhuda.

Mkuu, mimi kama mdau nimetoa maoni na mtazamo wangu tu si vinginevyo.
 
46 Reactions
Reply
Back
Top Bottom