Eu ushauri wenu kwa tz umechelewa!

MAKOLE

JF-Expert Member
Feb 5, 2012
618
280
Gazeti la Mwananchi la leo tarehe 21/11/2012 limechapisha habari kuwa Jumuiya ya Ulaya imeishauri Tanzania Kuboresha Bandari ya Dar es Salaam. Kwa wanaofuatilia habari za nchi ya kenya, BBC wametangaza taarifa ihusuyo mradi mkubwa wa Bandari kubwa kabisa katika ukanda wa Afrika inayojengwa (na tayari ujenzi umekwisha kuanza) katika eneo la Lamu nchini Kenya. Hapa naona Ushauri wa EU kwa Tanzania hautasaidia kwani wakati hiyo bandari ya Lamu haijakamilika tayari wafanyabiashara wengi huitumia bandari ya Mombasa, ikikamilika hiyo ya Lamu, ambayo itakuwa ama ni kubwa au miongoni mwa bandari kubwa hapa Afrika itakuwaje?

source, mwananchi na BBC leo tarehe 21/11/2012
 
Sisi tumeashindwa kuboresha ya Dar na ya Mtwara tunataka kujenga nyingine bagamoyo
 
Gazeti la Mwananchi la leo tarehe 21/11/2012 limechapisha habari kuwa Jumuiya ya Ulaya imeishauri Tanzania Kuboresha Bandari ya Dar es Salaam. Kwa wanaofuatilia habari za nchi ya kenya, BBC wametangaza taarifa ihusuyo mradi mkubwa wa Bandari kubwa kabisa katika ukanda wa Afrika inayojengwa (na tayari ujenzi umekwisha kuanza) katika eneo la Lamu nchini Kenya. Hapa naona Ushauri wa EU kwa Tanzania hautasaidia kwani wakati hiyo bandari ya Lamu haijakamilika tayari wafanyabiashara wengi huitumia bandari ya Mombasa, ikikamilika hiyo ya Lamu, ambayo itakuwa ama ni kubwa au miongoni mwa bandari kubwa hapa Afrika itakuwaje?

source, mwananchi na BBC leo tarehe 21/11/2012

Hakuna ushauri uliochelewa hapa. Biashara ya bandari siyo kama kupanga meza sokoni. Leo hii bandari kubwa East Coast of Africa ni Durban lakini haitishii bandari nyengine kama Maputo, Beira, DSM, au Mombasa.

Biashara ya bandari inategemea mambo mengi kama urasimu katika upakuaji, umbali wa wateja wako , mipaka ambayo mizigo inabidi ivuke ili kuwafikia wateja wako, urasimu wa uafirishaji wa mizigo nchi kave, etc.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom