commonmwananchi
JF-Expert Member
- Mar 12, 2011
- 3,377
- 1,957
Historia ni somo zuri maana huwa halidanganyi.
Tunawaona hawa EU wanavyojifanya sasa kutaka kutuaminisha kwamba ni wapenda demokrasia mahiri.mimi binafsi na pia wengi wenye mtazamo kama wangu tunashangaa sana.
Na maswali haya hayawezi kupita bila kuulizwa. Enzi za kupigania uhuru wa zaire wakati huo ikiongozwa na shujaa Patrice lumumba,ni hii ubelgiji ndio nchi ambayo ilihakikisha inasaidiana na wamarekani kumuua Lumumba na kumtumbukiza kwenye pipa la acid ili atokomee kabisa.
Baada ya hapo wakamuweka kibaraka wao Mobutu seseko na kongo iko kwenye uporwaji mpaka leo.
Je leo hii wanatokea wapi kusema haya wayasemayo?
Marekani imeharibu demokrasia ya kiarabu huko Iraq,Afghanistan,Syria,Libya,Tunisia na Egypt. Sasa hivi hata amani ya ulaya iko kwenye tishio kutokana na rundo la wakimbizi wanaovuka Mediterranean sea kukimbia vita alivyovianzisha marekani bila sababu za msingi zaidi ya ulafi wa maliasili za nchi hizo na bado hana aibu anajifanya kutusema Tanzania, lakini kisa ni udhibiti wa maliasili zetu (makinikia na Tanzanite).
Wahispania wana hasira nasi shauri ya deep sea ya Tanzania. Haya yote ukitaka kuyajua rejea ile team makinikia waliokuja hapa nchini na uangalie cv zao hapo utaelewa ninachokimaanisha.
Kuna mambo makubwa yanatokea huko marekani na yasiyo ya kidemokeasia kabisa, lakini hayaonwi kama tatizo ila tanzania ndio yanaonekana?!
Ushahidi ni jinsi maafisa waandamizi wa marekani wakiendelea kujiuzuru kwa kutofautiana na Rais wao Trump.
Wa hivi karibuni kabisa ni waziri wa ulinzi wa marekani Bw mattis.
Kuna nchi nyingi za kiafrika na ulaya zina matukio makubwa sana yanayopaswa kutolewa matamko ya kulaaniwa lakini hatuwasikii wakitoa tamko lolote.je kuna nini hapo?
Wazungu hawajawahi kumpenda muafrika kamwe bali huwa wanatuchanganya na kututumia kisha kututupa kama ganda la ndizi.