Sam Naipenda
Member
- Mar 1, 2018
- 97
- 720
Sikilizeni watanzania, huu sio wakati wa kutegemea kutetewa na Uingereza.
Leo mchana wengi wetu tumeshangazwa na tulichokiona kutokea Ikulu. Tumemwona waziri wa Maendeleo ya Kimataifa wa Uingereza Bi Penny Mordaunt alipomtembelea Mh Rais Magufulu na yeye akielezea kwamba amepewe kiasi cha shilingi 307.5B za kitanzania kama msaada wa kuendeleza kazi za serikali yake katika elimu, afya na mapambano dhidi ya rushwa. Hatujachukia kusaidiwa maana tunataka misaada.
Kilichoshangaza wengi ni kuona katika mazingira ya kisiasa tuliyonayo ambayo Mh Rais JIWE na baadhi watendaji wake aliowateua wameamua kuendesha nchi kikatili, wakivunja au kutokufuata sharia, wakikandamiza haki za binadamu, kuminya uhuru wa kujieleza na vyombo vya habari, na wakiharibu misingi mingi tu ya mfumo wa demokrasia, bado taifa kama Uingereza linampa misaada anayojigamba nayo hadharani. Wengi wetu tulitegemea nchi kama Uingereza ambayo ni moja ya nchi zinazoamini katika misingi ya demokraisa duniani kuwa mstari wa mbele katika kukemea, kukaripia, na hata kumwadhibu Mh Rais JIWE kwa yanayoendelea nchini.
Uingereza na mwenzake Marekani wamekua viranja wa demokraisia duniani miaka yote na mara zote ndio wamekua mstari wa mbele kuadhibu viongozi wanaokiuka misingi hiyo. Cha ajabu inaonekana sasa sio tu kwamba wanaachana na ukiranja huo, bali wako tayari kuwapa kiburi viongozi madikteta kama Mh Rais JIWE watawale vizuri. Nini kinaendelea? Ina maana Uingereza haioni kwamba kumpa misaada Mh Rais JIWE ambaye ameonesha wazi kwamba ana kiu, hamu, njaa, na kila aina ya uhitaji wa MISIFA YA KIJINGA ni kumuongezea ujasiri na misifa ya kijinga katika mkakati wake wa kukandamiza wananchi kwa kigezo cha maendeleo? Wanajua vizuri sana wanachokifanya.
Sikiliza mtanzania, kama unafuatili mambo yanavyokwenda duniani utaelewa kwamba nchi zilizokua mstari wa mbele kupigania demokrasia kwa ujasiri kama Uingereza na Marekani, wana matatizo lukuki ndani ya nchi ya nchi zao ambayo ni vipaumbele Zaidi na haviwapi muda wa kujisumbua na nchi wasizo na maslahi mapana nazo. Kivipi?
Sikiliza watanzani, Rais JIWE sio mjinga. Anajua kabisa kwa sasa hakuna mtu atamtisha maana viranja wako kimya. Anajua Kiranja Uingereza anamhitaji yeye kuliko yeye anavyowahitaji. Kwani hatujaona wasemaji wake kama kina Kabuni na yeye wenyewe wakijisifu kwamba nchi za nje wanatambua kazi anayofanya na kumsifu kuliko sisi watanzania? Au hatuelewi hiyo kauli inamaanisha nini? Rais JIWE anajua itachukua muda mrefu sana hadi atishiwe na mtu yoyote musishangae muda sio mrefu ataitoa Tanzania katika mahakama ya The Hague.
Sikilizeni watanzania, Tusishangae Uingereza kumsaidia Rais JIWE. Tena tusishangae tukiona wanamsifia hadharani. Wanafanya hivyo kutetea maslahi yao na unafuuu wa watu wao kiuchumi. Wana mengi ya kuvuna hapa kwetu na hivi vibilioni walivyotoa ni chenchi tu. Kupiga kelele kwetu hakuwagusi na haiwahusu. Sisi ndio tunayaelewa machungu yetu. Tunaelewa shida zetu. Tunaelewa maumivu tuliyonayo. NA SISI NDIO WA KUJITAFUTIA TIBA WENYEWE.
Mtumishi wa Umma

- Kule Uingereza wna wakati mgumu sana kutokana na kinachoendelea baada ya kura ya Brexit. Wananchi wake wana hofu kubwa na viongozi wa serikali pamoja na bunge wako bize na maslahi ya nchi yao baada ya kujitoa Jumuiya ya Ulaya na jinsi ambavyo wanaweza kuendelea kufaidika nayo. HAWANA MUDA NA DEMOKRASIA NA HAKI ZA BINADAMU TANZANIA.
- Uingereza wako bize kutazama "malisho mapya" baada ya kujitoa EU. Wanapambana kujenga mahusiano na mazingira mazuri ya kiuchumi na nchi za Jumuiya ya Madola ambazo nasi ni wanachama. Wanajenga mahusiano na nchi yoyote ile watakayoweza kufaidika kiuchumi na kupanua himaya yao ya utawama mamboleo. HAWANA MUDA NA DEMOKRASIA NA HAKI ZA BINADAMU TANZANIA.
- Waziri mkuu Theresa May hajawahi kukanyaga Afrika tangu achaguliwe. Sina hakika hata kama kuna waziri wake wa mambo ya nje ambaye ndio anamfuata kwa uzito kafanya hivyo. Presha aliyonayo May kwenye nchi yake ni kubwa kupita kiasi na amekua akiongoza baraza la mawaziri lililogawanyika kuhusu kujitoa EU. Kule Bungeni anabanwa na kina Corbyn kupita maelezo. HANA MUDA WA KUFUATILIA NA KUJICHOSHA NA DEKOMRASIA YA TANZANIA.
- Hali ya uchumi wa Uingereza sio nzuri sana. Ukifuatilia habari zao utaona maisha yanakua magumu, kazi ni tabu, wanakata bajeti kwenye maeneo mengi ya muhim kama afya, elimu, nk. Haya ndio vipaumbele vyao na HAWAWEZI KUTUMIA RASILIMALI ZAO HABA KUFUATILIA DEMOKRASIA NA HAKI ZA BINADAMU TANZANIA.
- Kwa kuwa wanataka kujenga mahusiano mapya kama mkakati mbadala baada ya kujitoa EU wanaogopa kukosana na mataifa wanayoyawinda hivyo hawawezi kuonesha misimamo migumu kuhusu mambo yao ya ndani. HAWANA MUDA WA KUINGILIA MAMBO YA NDANI YA TANZANIA.
- Kwa upande wa Marekani, ina janga la uongozi wa Trump ambaye karibu kila asubuhi kuna jipya la kukabiliana nalo. Huyu kama sio mifumo imara wa nchi yake naye angekua na mtindo wa utawala usiotofautiana na Rais JIWE. Hana mpango na demokrasia na anaonesha viashiria vingi vya kuikanyaga hata ndani ya nchi yake. Naye ni mbabe na asiyeogopa kukanyaga haki za binadamu. Kwa tabia zake, kawafanya hata maseneta na wabunge wa bunge la wawakilishi kua na mambo mengi ya nchi yao kuliko kujishughulisha demokrasia. Majuzi tumesoma kwamba tangu Trump aingine madarakani hajateua balozi wa kuja Tanzania na aliyepo anakaimu tu. Hii inatosha kuonesha kwamba hana mpango na maslahi yetu na huenda hata hajui jina la Rais JIWE
- Nchi za Jumuiya ya Ulaya? Sidhani. Ufaransa na Ujerumani haina maslahi makubwa na Tanzania na ni mara chache wanaongelea maslahi yetu. Kule Afrika Magharibi Ufaransa inaleo madikteka kadhaa hivyo sio tabu kwao.
- Nchi za EU zilizobaki ni ndogondogo zina matatizo mengi, na zisizo na historia ya kuhangaika na mambo ya nchi zingine "to that extent".
- Binamu yetu China yeye haamini katika Demokrasia na ndio baba wa MAJIWE Afrika. Anawapenda, anawakumbatia na anawasaidia kufanikisha ujiwe wao. Si umeona anamjengea JIWE na chama chake chuo pale Kibaha?
- Japan yeye hana shida na maisha ya watu na utawala wao. Mradi munanunua magari yake na bidhaa zao zingine yuko tayari kuwafadhili kwa chochote. Kwani umejiuliza kwa nini Rais JIWE katika mikakati yake ya kubana matumizi hajawahi kugusa eneo la magari ambalo limelalamikiwa tangu Enzi za Mkapa kwamba ni linatupotezea fedha sana? Hujaona wanavyotumia magari ya Japan ovyo hata kumlinda Mwita Mwikabe? Hagusi magari maana hataki kuigusa Japan.
- Waarabu wao wala hawajui demokrasia nini ili mradi kuna halua mezani. Maisha yao yote wanatawaliwa na familia za kifalme na jambo lolote lisilogusa dini yao hawana habari nao.
- Nchi jirani? Tunajua sote kwamba zinaongozwa na MAJIWE pia.