Eti tupungeze kuzaa...! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Eti tupungeze kuzaa...!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mtambuzi, Sep 26, 2012.

 1. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #1
  Sep 26, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  [​IMG]

  Katika utafiti uliofanyika hivi karibuni imebainika kwamba, idadi ya watu waliowahi kuishi hapa duniani ni kubwa ukilinganisha na idadi ya wale waliopo leo. Kwa mujibu wa tafiti mbali mbali zilizowahi kufanywa imebainika kwamba ni asilimia 30 tu ya watu wote wamewahi kuishi hapa duniani. Pamoja na ongezeko kubwa la idadi ya watu katika kipindi cha karne moja iliyopita, bado inaonekana kwamba watu waliowahi kuishi hapa duniani ambao sasa ni marehemu ni kubwa kuliko ile ya watu walio hai sasa hivi, hiyo ni kwa mujibu wa tafiti mbalimbali zilizofanywa mwaka 2002, mojawapo tafiti hizo ni ile ya mtaalamu wa idadi ya watu aitwae Carl Haub.

  Mtafiti huyo aliangalia mabadiliko ya idadi ya watu kutoka kizazi kimoja hadi kingine akizingatia mabadiliko ya mazingira, uchumi na matatizo ya uzazi na vifo. Akifanya utafiti wake kwa kuanzia kipindi cha Adam na Eva, kilichoanza miaka 50,000 kabla ya kuzaliwa Bwana Yesu Kristo. Kumbe Adam na Eva walikuwepo hapa duniani miaka 50,000 kabla Yesu hajazaliwa. Ingawa sina uhakika miaka hiyo ilipimwa kwa kalenda gani, lakini hilo tuachane nalo.

  Kwa kuangalia tafiti nyingine zilizofanywa imebainika kwamba, tangu kuumbwa kwa binadamu wa kwanza, dunia imewahi kukaliwa na watu zaidi ya bilioni 105. Hii ina maana kwamba idadi ya watu walioko duniani hivi sasa ni asilimia 7 tu ya watu ambao waliwahi kuishi hapa duniani. Hivi kama ingekuwa hatufi ingewezekana vipi watu kuishi hapa duniani hivi sasa? Je ni mpango wa Mungu ili kuepusha watu kufurika hapa duniani na kuhatarisha uwepo wake? Kwa mujibu wa takwimu za umoja wa mataifa zilizotolewa hivi karibuni, kuna idadi ya watu wapatao Bilioni 7 hapa duniani . Cha kushangaza Umoja huo wa mataifa unapiga kelele watu wapunguze kuzaa watoto wengi, ili kuepukana na uharibifu wa mazingira. Hivi ingekuwa hatufi, ingewezekana vipi watu bilioni 105 hapa duniani ilhali watu bilioni 7 tu, wanatishia usalama wa dunia?

  Hata hivyo kuna jambo moja ambalo Umoja wa Mataifa umeshindwa kulibaini. Kwa mujibu wa takwimu za hivi karibuni zilizofanywa katika nchi za Ufaransa na Japani, imebainika kwamba nchi hizo nikama vile hawazaani, kwani idadi ya wanaozaliwa na wanaokufa iko karibu sawa (Zero Population) na wazee wanazidi kuongezeka katika nchi hizo, lakini bado Umoja huo wa Mataifa wanahimiza watu kutozaana kwa wingi. Huko nyuma watu walizaana bila hofu na masharti, na ndio sababu idadi ya watu ilikuwa ikiongezeka kadiri miaka inavyokwenda, lakini siku hizi watu wanazaliwa kwa masharti.

  Wakati umoja wa mataifa ukipiga kelele tupunguze kuzaana, na hapo ndipo tunaposhuhudia idadi ya vifo ikiongezeka kila uchao, utasikia mara tetemeko la ardhi limeua watu 3000, mara ajali ya ndege, mara ajali ya treni, mafuriko, magonjwa ya mlipuko, vimbunga, nakadhalika nakadhalika. Na hapo tena tunasikia watu wakipiga kelele, jamaniee….. vifo vimezidi, watu wanakufa!!!???? Tunasahau kuwa ili dunia iendelee kuwepo ni lazima watu wazaane na nilazima watu wafe, huo ndio mfumo wa kuwepo dunia hii tunayoishi.
   
 2. MadameX

  MadameX JF-Expert Member

  #2
  Sep 26, 2012
  Joined: Dec 27, 2009
  Messages: 7,847
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Kweli ni kuwa zamani watu walikuwa na life expectancy kubwa, hii ni kutokana na mfumo wa maisha waliokuwa wakiishi ndo maana idadi ilizidi kwa kadri kubwa. Siku hizi lazima idadi ike breakeven possibly, maana japokuwa tunazaana kilasiku, maradhi kama HIV, cancer na mother nature forces ambazo zinabeba mabilion ya watu kutokana na mabadiliko ya dunia. Haya hayakuwepo enzi hizooo au ni machache sana.

  All in all we must have ****ed somewhere
   
 3. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #3
  Sep 26, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Kwa hiyo wewe MadameX unasimamia wapi...?
  Tupunguze kuzaa ama tuendelee kusongesha tu kwa kwenda mbele...?
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 4. MadameX

  MadameX JF-Expert Member

  #4
  Sep 26, 2012
  Joined: Dec 27, 2009
  Messages: 7,847
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Mmmh nitazaa kwa kiasi nitakachoweza kuwahudumia.......
   
 5. Watu8

  Watu8 JF-Expert Member

  #5
  Sep 26, 2012
  Joined: Feb 19, 2010
  Messages: 47,341
  Likes Received: 2,672
  Trophy Points: 280
  Kwa nchi kama ya China inayoongoza kwa idadi kubwa ya watu duniani, takwimu zinaonesha idadi ya wanawake ni kubwa kuliko wanaume hivyo ni wazi kuwa kasi ya kuzaliana nayo itakua ikiongezeka...

  pili wana sheria ya mtoto mmoja kwa familia hii yote ni kupunguza idadi ya watu...

  tatu idadi ya wazee ni kubwa kuliko rika lolote kwa kuwa watu wanachelewa kufa...

  Ukiangalia hizo takwimu kwa kiasi utaona zinakinzana, wakati wanajaribu kuzuia watu kuzaana, unakuta wale waliopo hawafi haraka pia wale wenye jukumu la kuzaa(wanawake) wanazidi kuongezeka.
  Mi nadhani tuache nature iamue tu...Mungu aliumba ili wazae waijaze nchi hivyo anajua ni wakati gani wa kupunguza na kuongeza
   
 6. L

  LADY JO Member

  #6
  Sep 26, 2012
  Joined: Sep 5, 2012
  Messages: 25
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tupunguze kuzaa ndugu! Siku hizi magonjwa mengi, mbali na hilo umaskini umekisiri! Asilimia kubwa ya watoto siku hizi wanakosa basic needs that's way watoto mitaani wanaongezeka, mateja, wezi, na nk.! Na ndio maana tunatakiwa kuzaa watoto ambao tutaweza kuwahudumia! Nchi kama hii Ya Tanzania ni lazima watu wapunguze kuzaa!
   
 7. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #7
  Sep 26, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,874
  Likes Received: 6,228
  Trophy Points: 280
  aaah hayo mambo ya wazungu tuwaachie wenyewe...sie tuzae tuongezeke tuijaze dunia....
   
 8. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #8
  Sep 26, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,966
  Likes Received: 1,858
  Trophy Points: 280
  Mtambuzi ninachoshindwa kuelewa mimi na ambacho kila siku huwa nawacriticize watu wa demography ni juu ya namna ya kupunguza kuzaa huku.
  angalia uzazi huu wa mpango umeelekezwa kwa mama tu, tuanze hivi mwanamake anategemewa aanze kuzaa akiwa na miaka 20 mwanamke huyu hadi afikie menopouse miaka 45 atatakiwa kuzaa mara zisizo pungua 8 tu, na hapa nimechukulia child spacing ya 3 yrs.

  turudi upande wa pili wa baba, maisha yanamruhusu mwanaume kuoa mke zaid ya mmoja kulinana na mila tofaut tofauti sasa baba huyu yeye awe na wake wawili tu atakuwa na watoto 16 wakati mama anao 8. sasa uzazi huu wa mpango umemlenga mama tu ama?

  ukirudi kwenye mch mama anapewa dawa za kupanga uzazi za aina tofauti katika dawa zote hizi hakuna zinazomzuia baba kuzaa wakati yeye ndo anaye oa mara nyingi kuliko mama sasa hapo uzazi upangwe na mama tu baba aachwe aendelee kuzaa?

  haya hebu jiulize zaid leo hii likitengenezwa bomu leo hii liue wanaume wote utagundua kwamba maisha bado yatasonga tu, lkn leo hii likitengenezwa bomu liue wanawake automaticaly maisha yatasimama sababu ni ipi hapo?
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 9. Bazazi

  Bazazi JF-Expert Member

  #9
  Sep 26, 2012
  Joined: Aug 18, 2008
  Messages: 2,029
  Likes Received: 561
  Trophy Points: 280
  Mtambuzi haja hapa kwa mtazamo wangu ni kuzaa kwa mpango na sio kuacha kuzaa hadi kufikia ongezeko la wangu la 0%. Kupunguza kuzaa ni muhimu sana hasa katika nchi zetu maskini kutokana na kuwa kwa sasa kila mtu na lwake hivyo tukizaa bila mpango watoto watakufa kama nzi.


  Ni hayo tu,

  Ndimi Bazazi!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 10. farkhina

  farkhina Platinum Member

  #10
  Sep 26, 2012
  Joined: Mar 14, 2012
  Messages: 12,831
  Likes Received: 775
  Trophy Points: 280
  Tuzae kama paka..

  Sent from my BlackBerry 9100 using JamiiForums
   
 11. Z

  Zero One Two JF-Expert Member

  #11
  Sep 29, 2012
  Joined: Sep 16, 2007
  Messages: 9,390
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  tuzae kadri tuwezavyo kuwamudu watoto tutakao wazaa, na sikuzaa ili mradi umezaa, matokeo yake watoto hapata shida nawe mzazi kuishi katika mazingira magumu na familia yako.
   
 12. Kaunga

  Kaunga JF-Expert Member

  #12
  Sep 29, 2012
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 12,591
  Likes Received: 797
  Trophy Points: 280
  Kuna kitu sijaelewa hao watu bil 105 waliwahi kuishi, waliishi duniani at per au ni kiasi cha watu waliozaliwa kuanzia Adam mpaka leo?

  Haya kuhusu uzazi wa mpango, kuna dhana 2, ya kwanza ni kuzaa watoto wachache na ya pili ni idadi unayoitaka ukipangilia mwenyewe (si kwa bahati mbaya).

  Kuhusu ya idadi ya watu kuongezeka haina mjadala fuatilia takwimu za Tanganyika tangu tunapata uhuru mpaka leo. Na mtoto anakuja na mahitaji yake ili aweze kuishi, nafikiri watafiti wanaweza wakatupigia hesabu anahitaji heka ngapi kwa ajili ya chakula, Maji baridi kiasi gani na mengine mengine mengi tu. Zamani ambapo huduma za afya zilikuwa hafifu kulikuwa na vifo vya watoto wengi, ndio maana ukizaa mtoto mmoja au wawili utaambiwa "shetani anatazama huyo huyo, binadamu na Mungu pia".

  Lkn sasa pamoja na HIV, malaria, njaa etc population inazidi kuongezeka; Kgm pop growth 2.8% kwa mwaka.
  Kupanga ni kichagua, tuzae tuongeze idadi ya chokoraa au tuzae watoto ambao tutawawezesha walau wawe walimu wa shule za msingi. Tuzae wengi ili hata mmoja akifariki kwa kukosa ORS (kuharisha), tutabaki na watoto 9.
   
 13. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #13
  Sep 29, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,759
  Likes Received: 82,733
  Trophy Points: 280
  Tupunguze kuzaa maana gharama za maisha ni za juu mno. Yanini kuwa na kundi la watoto kama huwezi kuwapatia lishe ya uhakika na elimu ya uhakika ili watakapokuwa wakubwa waje kusimama wenyewe kwa miguu yao miwili. Angalia tatizo la watoto wa mitaani linavyozidi kuongezeka kwa wazazi kutelekeza watoto mtaani pale wanaposhindwa kumudu gharama za maisha. Dini zetu kubwa mbili zinaongeza tatizo kwa kupinga uzazi wa majira na matumizi ya kinga mbali mbali ili kuzuia mimba zisizostahili. Angalia kama picha ya mtoto huyu jinsi inavyotilisha huruma, anajiuliza "Hivi ni kwanini mimi nilizaliwa!?"

  [​IMG]
   
 14. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #14
  Sep 29, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 303
  Trophy Points: 160
  mie bado nazaa sana tu.
   
 15. Kijakazi

  Kijakazi JF-Expert Member

  #15
  Sep 29, 2012
  Joined: Jun 26, 2007
  Messages: 3,546
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 135
  Hata hiyo sentensi peke yake ni mambo ya wazungu mbona haujawaachia umeiandika?
   
 16. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #16
  Sep 29, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Ni kiasi cha watu waliozaliwa na kufa kuanzia Adam na Eva mpaka leo hii... ndio maana unakutas ongezeko la watu wanaoishi hapa duniani kuanzia karne ya 19 linaongezeka kidogo kidogo tofauti na karnr zilizopita,,,,
   
 17. Kaunga

  Kaunga JF-Expert Member

  #17
  Sep 29, 2012
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 12,591
  Likes Received: 797
  Trophy Points: 280
  Asante kwa ufafanuzi, nilielewa vizuri kumbe. Na kiundani nilikuwa na mtazamo huo huo; na mara nyingi huwa nahisi kila mtu anapokanyaga, lzm ndani ya hatua tano au kumi kuna maiti ya mtu hata kama imekuwa mbolea.
   
 18. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #18
  Sep 29, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,759
  Likes Received: 82,733
  Trophy Points: 280
  ...Hongera zako...unao wangapi hadi hivi sasa!?

   
 19. nyumba kubwa

  nyumba kubwa JF-Expert Member

  #19
  Sep 29, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 10,279
  Likes Received: 1,720
  Trophy Points: 280
  Juzi kati nilikuwa naangalia CCN na picha nilopata ni opposite hasa ikija kwa kizazi kipya cha Wachina.

  Watoto wa kike ni wachache mno kwa kuwa couples ziko tayari kutoa mimba pindi wanapojua mimba ni ya mtoto wa kike na fact kuwa wanatakiwa kuwa na mtoto mmoja tu.

  Hii imeanza kuwaumiza kichwa wachina...kuwa wanaume wengi watakosa wake siku za usoni...ukizingatia si watu wa kujichanganya na mataifa mengine.

  Huko china watu wanafikia kutupa watoto wa kike ili wapate chance ya kuzaa tena wapate mtoto wa kiume.

  Na kama nilifuatilia vizuri wanafikiria kurekebisha hiyo one child policy kuruhusu angalau watoto wawili.

  Inachekesha sana...nasikia ukizaa watoto zaidi ya mmoja unatozwa faini kubwa sana. Kuna couple mpaka ilibidi wafilisike kulipia fine ya kuwa na mabinti wawili...lakini wanasema hawa regret kwani ni raha kuwa na watoto wawili ambao kwa sasa ni wanafunzi wa chuo kikuu.

   
Loading...