Eti nimfanyaje huyu?

Eti nimfanyaje huyu?

zandar

Member
Joined
May 27, 2013
Posts
99
Reaction score
18
Wadau nina mpenzi wangu ambae anasoma chuo kiukweli katumia pesa zangu sana tu mpaka akafikia kunizalia mtoto, sasa pesa zimekata na nyumba niliyopanga nikarudisha nikarudi home kujipanga upya nikiwa nae, kapata pesa akanambia kapanga nyumba kwaiyo nipeleke vitu tuka ishi wote tena.

Chakushangaza ile namaliza kuingiza vitu ndani tunatoka kwenda kula ananambia pale ni kwake na vile vitu nisahau vitakuwa vya mtoto ila nikitaka kumuona mtoto niende muda wowote ila siyo kwetu tena ni kwake na mtoto wadau nimfanyaje huyu kabla sijafanya unyama.

Naomba mawazo yenu kwanza.
 
Hahaaa..mkuu zandar kwanza pole sana.

Ungeangalia kwanza ukaribu wenu, maelewano na mapenzi kati yenu. Swala la kupeleka vitu halafu unahamia bila mipango yoyote kama Ndoa nadhani ni kutafuta mteremko wa maisha.

Halafu wewe ni mwanaume, sioni kama ni busara kwa maamuzi ulochukua ya kuhamia kwa mwanamke bila malengo madhubuti. Inaonekana wewe uliwahi kumsumbua sana na hapo anafanya malipizi tu, kwa binaadam yoyote hawezi kukurupuka na kukufanyia hivo.

Hapo kuna mawili labda ulimtelekeza na mtotot wake, sasa unaona maisha yake yamenyooka ndio unajirejesha. Cha kufanya kua mpole tu, uamuzi wowote wa kukurupuka utakutia matatizoni.
 
Last edited by a moderator:
Hasara roho' Pesa makaratasi! Pesa na vitu hutafutwa na haukuzaliwa navyo' umetafuta tu na ukavipata hivyo anza upya. Na kuanza upya sio ujinga.

Usilumbane nae mwachie' jipange upya! Chukulia kama yalikuwa mapito na changamoto katika maisha. Maana haujakatwa mikono wala haujachukuliwa akili. Hivyo wewe bado ni tajiri tu.
 
Utafikiri ulikua kichwani mwangu wakati unaandika
 
Mtoto kama ni wako kweli mwachie tu mkuu, Vitu kwani bei gani jamaa kugombana na mzazi mwenzio.
 
Muachie tu hivyo vitu. Mwanaume umeumbwa kutafuta. Watu walitoa magari na takataka nyingine wakaingizwa mjini itakuwa household items. Achana nae, tena furahia tu kwa kuwa mwanao atakaa pazuri. Mungu atakurudishia maradufu wala sio issue.
 
hasara roho' pesa makaratasi! Pesa na vitu hutafutwa na haukuzaliwa navyo' umetafuta tu na ukavipata hivyo anza upya. Na kuanza upya sio ujinga.

Usilumbane nae mwachie' jipange upya! Chukulia kama yalikuwa mapito na changamoto katika maisha. Maana haujakatwa mikono wala haujachukuliwa akili. Hivyo wewe bado ni tajiri tu.

naam mkuu ajipange upya tu la msing ni kua ana access na mwanae shukuru mungu kama mwanaume jipange upya na maisha yako kaka what goes around comes around very early so na kama mwanaume hana haja ya kuweka kinyongo na mwanamke mkuu......................
 
Wewe nae ! vitu ndiyo nini kesho utapata vitu vingine vipya, just forgeti utafute maisha kwingine!
 
Wadau nina mpenzi wangu ambae anasoma chuo kiukweli katumia pesa zangu sana tu mpaka akafikia kunizalia mtoto, sasa pesa zimekata na nyumba niliyopanga nikarudisha nikarudi home kujipanga upya nikiwa nae, kapata pesa akanambia kapanga nyumba kwaiyo nipeleke vitu tuka ishi wote tena.

Chakushangaza ile namaliza kuingiza vitu ndani tunatoka kwenda kula ananambia pale ni kwake na vile vitu nisahau vitakuwa vya mtoto ila nikitaka kumuona mtoto niende muda wowote ila siyo kwetu tena ni kwake na mtoto wadau nimfanyaje huyu kabla sijafanya unyama.

Naomba mawazo yenu kwanza.
Huyo mdada yuko sahihi pale ni kwake na amekuwa muungwana kwa kukueleza mtoto uwe unaenda kumsalimia, mwanaume utategemeaje nyumba ya mkeo.
 
Swala jengne kwan hvyo vitu si anakaa navyo mzaz mwenzio naona ni kwa ajil ya mwanao mwisho wa siku nahis kama una waswas wa kwamba anaeza kuja mwanaume mwenzio akawa anatumia vitu vyako
 
Wadau nina mpenzi wangu ambae anasoma chuo kiukweli katumia pesa zangu sana tu mpaka akafikia kunizalia mtoto, sasa pesa zimekata na nyumba niliyopanga nikarudisha nikarudi home kujipanga upya nikiwa nae, kapata pesa akanambia kapanga nyumba kwaiyo nipeleke vitu tuka ishi wote tena.

Chakushangaza ile namaliza kuingiza vitu ndani tunatoka kwenda kula ananambia pale ni kwake na vile vitu nisahau vitakuwa vya mtoto ila nikitaka kumuona mtoto niende muda wowote ila siyo kwetu tena ni kwake na mtoto wadau nimfanyaje huyu kabla sijafanya unyama.

Naomba mawazo yenu kwanza.

Fanya kwamba vile vitu umempa mwanao. Anza moja na upate funzo hapo. Kweli mwanaume unahamia kwa mwanamke? Je una uhakika hajapangishiwa na kidume mwingine hapo?
 
Umeweza kumlea mwanao kwa kiasi gani?
Mna mahusiano yaliyo katika hali gani?
 
khaaaa!! kwanza furniture zinakawaida ya kupitwa na wakati,, so we acha tu endelea na mipango mingine ya maisha yako
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom