Eti 'Mpe wa Nyumbani Yule'.....

Eti 'Mpe wa Nyumbani Yule'.....

Nyani Ngabu

Platinum Member
Joined
May 15, 2006
Posts
97,115
Reaction score
136,844
Hiyo ni kauli ya dada mmoja hivi jirani yangu niliyemsikia akiongea kwenye simu!

Na huyo wa 'nyumbani' si mwingine bali ni yule mgombea urais kupitia CCM.

Huyu mdada anatokea huko kanda ya ziwa. Pia, jana niliongea na mtu wangu wa karibu aliyeko pande za Simiyu huko na akanambia kuwa mwelekeo wa watu wengi huko ni kumpigia kura mgombea wa CCM kwa kutumia hiyo sababu ya wa 'nyumbani'.

Sasa mimi sielewi kabisa.

Hivi ina maana rais akiwa ni wa 'nyumbani' ndo shida za watu wa 'nyumbani' zitaisha au?

Kama hazitaisha, kuna nini kingine katika kumpigia kura huyo mtu wa 'nyumbani'?
 
Watashangaa sana pale ambapo tutapata kura nyingi huko Kanda ya Ziwa na hata Chato na kuwaacha wakijiuliza inakuwaje hata kwao kashindwa
 
NN karibu Msoga. Ten years ago hapakuwa palivyo leo. That set the prrcedence of favouring nyumbani for all the might and wannabes.
 
Ni ujinga kabisa, mambo ya ukabila na ukanda ni vya kukemewa kbs
 
NN karibu Msoga. Ten years ago hapakuwa palivyo leo. That set the precedence of favouring nyumbani for all the mighty and wannabes.
 
Mbaya zaidi ni pale mgombea mwenyewe wa Urais wa Tanzania anapowaambia waumini wamuombee kwa Mungu ili aweze kuwa Rais wa Tanzania kwa sababu dhehebu lake halijatoa Rais wa Tanzania.

Sasa unajiuliza, hivi huyu Mungu anawaumba binadamu kwa kuangalia madhehebu?

Huyu Mungu anaweza kuruhusu na kukubaliana na fikra za kibaguzi kwa watoto wake wote.

Ni Mungu gani huyu anayetoa baraka katika misingi ya kuligawa Taifa lake.

Kwani hao ambao wanaomba Mungu awape Rais kutoka dhehebu lao wamebaguliwa au watapata nini zaidi ya madhehebu mengine.
 
mnatafuta kuneutralize... swala ni mgombea urais kuomba kura kanisan kisa yeye mlutheran.. eti kwa vile hajatokea mlutheran teh teh... dah kwel tumuogope kama ukoma
 
Ukawa wanapoteana sasa, CCM ongeza mapigo na kuchanganya formation tofautitofauti kuanzia 4-4-2, 4-3-3, 3-5-2 nk mpaka ukawa wasalimu amri. Mtoto akililia wembe mwache wembe umkate
 
Mbaya zaidi ni pale mgombea mwenyewe wa Urais wa Tanzania anapowaambia waumini wamuombee kwa Mungu ili aweze kuwa Rais wa Tanzania kwa sababu dhehebu lake halijatoa Rais wa Tanzania.

Sasa unajiuliza, hivi huyu Mungu anawaumba binadamu kwa kuangalia madhehebu?

Huyu Mungu anaweza kuruhusu na kukubaliana na fikra za kibaguzi kwa watoto wake wote.

Ni Mungu gani huyu anayetoa baraka katika misingi ya kuligawa Taifa lake.

Kwani hao ambao wanaomba Mungu awape Rais kutoka dhehebu lao wamebaguliwa au watapata nini zaidi ya madhehebu mengine.
Walianza na mungu, watamaliza na mungu. Huyo mungu wao atajulikana Novemba.
 
Nyie hangaikeni semeni kila muwezalo ila october ni ukawa na lowasa ndio mwanamapinduzi wa kweli utabiri wa baba wa taifa utatimia
 
Hii akili huwa tunayo sana,Wakenya waliamini sana kuwa watasaidiwa na OBAMA eti kwasababu anaasili ya KIAFRIKA..
 
Safi sana kaka. Kuna kiongozi mmoja wa Kahama (CCM) ndani ya mkutano akaanza kuwahadaa wanazengo kuwa mchagueni Msukuma mwezetu, Magufuri kwani hata ukiwa na shida ya kuonana nae akiwa mapimziko kutoka hapa tulipo hadi chato hata kwa baiskeli unaweza fika kwa Magufuri!!! Shiiiiti😕
 
Hii akili huwa tunayo sana,Wakenya waliamini sana kuwa watasaidiwa na OBAMA eti kwasababu anaasili ya KIAFRIKA..

Tena hao Wakenya ni zaidi ya wajinga!

Ni majuha kabisa.

Siku Obama aliyochaguliwa kuwa rais wa Marekani eti wenyewe (hao Wakenya) wakatangaza kuwa ni siku ya mapumziko.

Wakati huko kwao Marekani ilikuwa ni siku ya boksi kama kawaida.
 
Unashangaa mpe wa nyumbani wakati Lowassa anasema walutheri wampe kura kwa kuwa yeye ni mlutheri.

Hilo halikupi shida?
 
Back
Top Bottom