Eti kweli huyu anafaa?

Miss_Irene

JF-Expert Member
Jun 12, 2019
320
455
Kwanza kabisa nitoe pongezi za dhati kwa mheshimiwa Rais kwa kutuletea mtandao huu wa JamiiForums hakika Rais Magufuli ni mwamba (samahani nimeangalia taarifa ya habari ya ITV leo kuna daraja sijui Tanga kwa Godwin Gondwe sijui sasa kila mtu anasema pongezi ziende kwa Rais nikasema sasa imekuwa too much hata kama ni sifa imeanza kuboa aiseee!

Wacha niende kwenye mada, kuna mkaka anataka kuoa mdogo wa rafiki yangu, bado haja jitambulisha lakini. Ila tatizo rafiki yangu anadai hamuelewi elewi huyo shemeji yake mtarajiwa (ila hajawahi kumuona)

Kinieleza vitu vingi ila hiki imebidi nikishee kwenu

Kiufupi mwandiko wake haueleweki aisee nimesoma text za chats zake nikachoka mno zipo kama hivi

"uxiconde xhem 2po pa1" hii ni moja ya text yake huyu kweli anajielewa jamani anafaa kuoa mdogo wetu huyu?
 
Mwisho wa siku ni mdogo wenu ndio mwenye maamuzi ya mwisho binafs labda niulize wana umri gani?
Kwani wee ukiona mwanao au ndugu yako anapotea labda kwa mfano unamuacha tu eti yeye ndo ana maamzi? Mdogo wetu ana 21 huyo muoaji sijajua kiukweli maana hata sijamuona
 
Miss_Irene,
Hukunielewa mantiki ya kuuliza hilo swali la umri nilitaka kujua tu ndugu yenu ana umr gani hadi nyie muingilie maamuzi yake swala la kuoana likishafika ni la watu wawili binafsi kama umri unaruhusu kwa miaka 21 bado mdogo mnaweza mpa ushaur tu wa changamoto za ndoa kuingia hasa na umri wake huo akiona hawaelewi mtu anakanywa akisharudi sio akienda.
 
@Miss_Irene,Mpaka hapo huo ni wivu.
Acha mdogo wako aolewe wewe endelea kusugua benchi
 
Ndoa ni ya wawili wewe unasema hafai lakini yeye kaona anafaa na si ajabu hata miandiko inafanana.
 
hukunielewa mantiki ya kuuliza hilo swali la umri nilitaka kujua tu ndugu yenu ana umr gani had nyie muingilie maamuzi yake swala la kuoana likishafika ni la watu wawili binafsi kama umri unaruhusu kwa miaka 21 bado mdogo mnaweza mpa ushaur tu wa changamoto za ndoa kuingia hasa na umri wake huo akiona hawaelewi mtu anakanywa akisharudi sio akienda.
Sawa shost nimekuelewa
 

Similar Discussions

3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom