Sajenti
JF-Expert Member
- Apr 24, 2008
- 3,651
- 412
- Thread starter
- #41
...Lakini na wanawake kwa upande wao wanachangia katika kuiweka hii dhana ya kuwa demu akimegwa sana ni malaya na si mwanaume. Nina mifano hai kwangu mi binafsi ya wanawake ambao walijua kuwa nimemega rafiki zao na ninapo-muapproach yeye anaishia tu kukwambia lakini wewe unapenda sana wanawake....huku anainma chini na kutafuna kucha, ukimtolea macho sana na uongo mwingine kidogo unachukua mzigo!Tuliangalie hili swala kwa undani zaidi.Hii ni moja ya maswala tete ya jinsia. Moja ya ishu kubwa katika muktadha mzima wa mambo ya jinsia ( gender) ni mitizamo ya behaviours zinazoonekana ni sahihi kwa wanawake na wanaume na hili ni standard katika jamii nyingi.Watoto wa kike na wa kiume hupewa malezi yenye kuonyesha kuwa msichana/mwanamke lazima awe mwenye aibu kutenda mambo fulani hasa haya ya kujamiiana.Wavulana/wanaume wao hulelewa kuelekea kuwa viwembe kwenye mambo hayo na ni njia mojawapo ya kuonekana ni kidume kwelikweli.Kwa kweli malezi haya japo hudumisha heshima kwa wanawake, inabidi kutizamwa kwa jicho lingine hasa kwa miaka hii yenye UKIMWI.
Ulimwengu umebadilika sana na hata zile systems za kurekebisha mienendo mibaya kwenye jamii hazipo tena na hata kama zipo hazifanyi kazi. Pia kuna matatizo mapya ambayo yamejitokeza siku hizi ambayo zamani hayakuwepo.Mwanaume au mvulana mwenye kujivinjari ovyo ovyo..huweza kupata athari za kiafya na hata kifo. Ni muda muafaka kwa jamii kusisitiza heshima kwa wote... hakuna cha mvulana wala msichana.Kilicho kibaya kwa msichana ni kibaya pia kwa mvulana - ndio ukweli kwa maisha ya sasa hivi.