Eti kuna nchi ambazo hakuna mbu hapa duniani?

Wadau nilikuwa nabishana na jamaa flan et kuna nchi ULAYA na AMERCA ambazo hakuna mbu kabisa, tumebishana sana nikaona nilete ubishi huo umu jamvini ili tusaidiane kupeana faida

Sent using Jamii Forums mobile app
Uwezekano wa kuwepo ndio ni 50% Kwa 50% Ila wanautofauti sema hivi mbu wapo wenye Sumu na wasio na Sumu mfano "Ivilikinge wapo wa mchana wakati limewaka Jua ukipita msituni unawapata na wanang'ata"Ila hawana madhara

Siyo nchi za mbali...kipindi flani nilienda kuishi masaki...swali la kwanza mbona hakuna net wakaniambia hakuna mbu. Dah niliona aibu sana...kuwa nshazoea shida.
Lakini naamini siyo maeneo yote ya masaki na siyo misimu yote ktk mwaka

Mambo yasiwe mengi, mengi yasiwe mambo
 
Ungesema hakuna Malaria sawa.

Maana kuna sehemu mbu wapo lakini malaria wanasikia kwenye taarifa ya habari kuwa "nchi fulani watu wamekufa kwa malaria ya kung'atwa na mbu"
 
Kiufupi,mbu haishi sehemu za baridi,mfano america na ulaya,kote hakuna mbu.mfano dhahiri ni mikoa ya baridi hapa bongo like,arusha,iringa,mbeya kidogo,kilimanjaro etc

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Baadhi ya maeneo ya mbeya, njombe, iringa, Kilimanjaro na Arusha Amna mbu wala nzi Achana na huko mbali
 
kwetu kibosho sijawahi kuona mbu....... ila mabogini na chekereni kuna mbu wakubwa kwa maana kunalimwa mpunga..... sasa siku ya kwanza nimetoka kwetu kibosha nikaenda mabogini usiku nikauliza mwenyeji wangu hawa ni nzi gani wanazunguka usiku?? Jamaa alinicheka sana ndiye akaniambia ni mbu.
 
Mbu ni mdudu anayeishi katika hali ya joto. Kwa maana hiyo anatambulika zaidi kama mdudu wa kitropik (Tropical insect) Anapatikana zaidi kati ya tropics za cancer kwa upande kaskazini kushuka kusini mpaka unapoifikia tropic ya Capricon. Kwa maana hiyo basi mbu huyu anapatikana katika bara la Africa ,Amerika ya kusini na kusini mwa bara la Asia katika nchi kama India, Bangladesh, Sri Lanka na Indonesia. Vilevile anapatikana katika visiwa vilivyopo katika bahari ya Pacific vilivyopo ndani ya tropik hizo nilizotaja. Mbu huyuhuyu anaeneza magonjwa tofauti kulingana na sehemu anayopatikana. Mfano mzuri ni huku kwetu anaeneza malaria lakini ukienda kusini mwa Asia anaeneza ugonjwa wa Dengue. Katika safari zangu za bara la Ulaya niliwahi kumuona mbu mara moja tu nchini Uholanzi. Na alikuwa ni mkubwa kuliko hawa wa huku kwetu. Ukubwa wake unaweza kukaribiana na ule wa nzi. Watu wa uholanzi wanamuita MUG. Na haambukizi ugonjwa wa aina yoyote. Nadhani mtoa swali utakuwa umejifunza kitu kwa jibu langu..
 
Wadau nilikuwa nabishana na jamaa flan et kuna nchi ULAYA na AMERCA ambazo hakuna mbu kabisa, tumebishana sana nikaona nilete ubishi huo umu jamvini ili tusaidiane kupeana faida

Sent using Jamii Forums mobile app
Yes Cuba wametokomeza woote, hata serekali yetu iliwaleta watengeneze kile kiwanda cha kuua viluilui vya mbu pale kibaha ila mpaka leo sijui kama kimeshaanza kuzalisha.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uwezekano wa kuwepo ndio ni 50% Kwa 50% Ila wanautofauti sema hivi mbu wapo wenye Sumu na wasio na Sumu mfano "Ivilikinge wapo wa mchana wakati limewaka Jua ukipita msituni unawapata na wanang'ata"Ila hawana madhara

Sent using Jamii Forums mobile app
Weeee hapo tuta kamatana uongo kule ni nyumbani hakunaga huyo mdudu, poli LA wapi uliona maana mie nimechunga vindama na mbuzi kwenye Yale mabonde, sasa we niambie ulimuona wapi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom