Eti Kikwete acharuka! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Eti Kikwete acharuka!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Mar 19, 2011.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Mar 19, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,587
  Likes Received: 82,209
  Trophy Points: 280
  Kikwete acharuka, amtaka Ngeleja awe makini
  Imeandikwa na Oscar Mbuza; Tarehe: 18th March 2011 @

  RAIS Jakaya Kikwete amemtaka Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja kuwa makini na utatuzi wa suala hilo ili kuiepusha nchi kuingia katika kashfa kama iliyosababishwa na Mkataba wa Richmond.

  Katika hatua nyingine, Rais Kikwete ameagiza kuwekwa pembeni kwa ushabiki wa kisiasa katika utekelezaji wa miradi ya uzalishaji umeme ili kuweza kufikia malengo yaliyowekwa na serikali ya kuzalisha zaidi ya megawati 1,130 za umeme ifikapo mwaka 2013.

  Rais Kikwete aliyasema hayo alipokuwa akizungumza na maofisa wa Idara na Mashirika yaliyo chini ya Wizara ya Nishati na Madini katika ziara yake ya kikazi ya siku moja kwa wizara hiyo jana.

  "Katika suala hili la uzalishaji wa umeme wa dharura, naomba tujifunze kutokana na historia. Nakumbuka suala la Richmond lilitokana na suala kama hili la uzalishaji wa umeme wa dharura.

  "Nililisema hili pale katika kikao cha Baraza la Mawaziri, shughuli hizi zote za uzalishaji wa umeme wa dharura zianzie na kuishia palepale Tanesco. Bodi ya Tanesco isimamie mchakato mzima bila kuingiliwa na wizara, naomba tusirudi tena kule," alisema Rais Kikwete.

  Kabla, Waziri Ngeleja alisema Wizara yake inachukua mikakati mbalimbali ya muda mrefu, muda wa kati na mikakati ya dharura katika kukabiliana na matatizo ya umeme nchini.

  Kuhusu mikakati ya dharura inayochukuliwa sasa ni kuagizwa kwa majenereta ya kufua umeme yanayotumia mafuta mazito yenye uwezo wa kuzalisha megawati 260 ambapo jana ilikuwa mwisho wa kupokea nyaraka za zabuni kwa ajili ya uagizwaji wake.

  "Mheshimiwa Rais, ni imani yetu kwamba katika wiki ya pili au ya tatu ya Mwezi Aprili, mwaka huu, majenereta haya yatakuwa yamewasili na lengo letu ni kuona kuwa umeme unaanza kuzalishwa ifikapo mwezi wa saba," alisema Ngeleja.

  Waziri alisema pamoja na mpango huo wa dharura ni matumaini ya Wizara hiyo kuona kuwa kunakuwa na uzalishaji wa megawati 1,130 za umeme zitakazoingizwa kwenye gridi ya taifa ifikapo mwaka 2013 kutokana na kukamilika na kuanza kazi kwa miradi mbalimbali ya uzalishaji wa umeme.

  Aliitaja baadhi ya miradi hiyo kuwa ni ule wa Kiwira (Mbeya) utakaozalisha megawati 200, Mnazi Bay (Mtwara) megawati 300, Kinyerezi (Dar es Salaam) utakaozalisha megawati 240 na Mwanza megawati 60.

  Waziri Ngeleja alitaja mafanikio mbalimbali yaliyofikiwa katika miradi ya umeme inayosimamiwa na Wakala wa Umeme Vijijini (REA) yenye miradi 41 sasa, miradi ya Shirika la Changamoto za Milenia (MCC), miradi ya Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB) na miradi ya uzalishaji umeme kupitia majenereta na mitambo inayosimamiwa na Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco).

  Akizungumzia miradi hiyo, Rais Kikwete alisema itaweza kukamilika kama ilivyopangwa kama watendaji ndani ya wizara hiyo watapeleka nguvu na fikra zao katika utekelezaji wa miradi na si maneno yasiyokuwa na nia ya dhati na ya kisiasa.
  "Lengo langu ni kuona tunaondokana kabisa na umeme wa maji.Tukiweza kupata umeme wa Mtwara na Kiwira tu utaweza kabisa kutufanya tuachane na umeme wa Mtera na Kidatu. Umeme wa maji uwe umeme wa ziada na si tegemeo kama ilivyo sasa.

  "Mradi wa Kiwira haukuweza kukamilika kutokana na siasa kuingia ndani yake, (siasa au kulikuwa na wizi uliofanywa na Vingunge mafisadi?) lakini sasa mradi umerejeshwa serikalini na kuna hatua zinaendelea kuchukuliwa ili mradi uanze uzalishaji upya, hili likitekelezwa tutakuwa mbali," alisema.

  Rais pia alieleza kuridhishwa kwa kiwango kikubwa na mikakati inayochukuliwa na Taneso chini ya Mkurugenzi Mtendaji, Mhandisi William Mhando na Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (Ewura) chini ya Mkurugenzi Mkuu, Haruna Masebu katika kuongeza miradi ya uzalishaji wa umeme na usambazaji.

  Alisema ili kufikia lengo la Wizara ya Nishati na Madini la kuona umeme unawafikia asilimia 30 ya Watanzania nchi nzima kutoka asilimia 14 za sasa ifikapo mwaka 2015, jitihada za makusudi zinatakiwa kuchukuliwa na vyombo husika hasa REA, Ewura na Tanesco ili kuhakikisha miradi yote iliyoainishwa inatekelezwa.

  Kampuni ya Richmond ilipewa zabuni na serikali kupitia Wizara ya Nishati na Madini, ili kuzalisha umeme wa dharura baada ya nchi kukumbwa na nakisi kubwa ya umeme mwaka 2006 kutokana na kukauka kwa maji katika Bwawa la Mtera, kazi ambayo kampuni hiyo ilishindwa kuifanya.

  Hatua hiyo ilisababisha Bunge kuunda Kamati Teule ili kuchunguza mazingira ya mkataba huo baina ya serikali na Richmond chini ya Mbunge wa Kyela, Dk. Harrison Mwakyembe, iliyobaini kuwa kampuni hiyo ilikuwa hewa na haikuwa na uwezo wa kuzalisha umeme kama ilivyodai kwa serikali.
  Kutokana na kitendo hicho Kamati hiyo ilipendekeza kujiuzulu kwa viongozi wa serikali waliohusika na mkataba huo wa Richmond kwa kuiingiza nchi katika hasara, hatua iliyomfanya aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa, Waziri wa Nishati na Madini Nazir Karamagi na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk. Ibrahim Msabaha, kujiuzulu Februari 2008 na kumlazimisha Rais Kikwete kuvunja Baraza la Mawaziri.
   
 2. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #2
  Mar 19, 2011
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  RAIS Jakaya Kikwete amemtaka Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja kuwa makini na utatuzi wa suala la matatizo ya umeme ili kuiepusha nchi kuingia katika kashfa kama iliyosababishwa na Mkataba wa Richmond.

  Katika hatua nyingine, Rais Kikwete ameagiza kuwekwa pembeni kwa ushabiki wa kisiasa katika utekelezaji wa miradi ya uzalishaji umeme ili kuweza kufikia malengo yaliyowekwa na serikali ya kuzalisha zaidi ya megawati 1,130 za umeme ifikapo mwaka 2013.

  Rais Kikwete aliyasema hayo alipokuwa akizungumza na maofisa wa Idara na Mashirika yaliyo chini ya Wizara ya Nishati na Madini katika ziara yake ya kikazi ya siku moja kwa wizara hiyo jana.

  HabariLeo | Kikwete acharuka, amtaka Ngeleja awe makini
   
 3. Pakawa

  Pakawa JF-Expert Member

  #3
  Mar 19, 2011
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,733
  Likes Received: 3,160
  Trophy Points: 280
  Mchezo wa kuigiza hakuna jipya hapa. Alikuwa wapi siku zote kuwafokea watumishi wake???? mpaka mabolozi wamtoe usingizini ndio atoe tamko?? Mawaziri wako mkuu ni vilaza hawana faida yoyote kwa taifa hili. Nchi itaaje gizani miezi yote hii halafu wewe unakaa kimya. Too late too little
   
 4. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #4
  Mar 19, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  aanze yeye kuwa makini kwa kumuwajibisha Ngeleja
   
 5. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #5
  Mar 19, 2011
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Mtu anauchapa tena mbele yake ataweza kumwajibisha kweli?

  [​IMG]
   
 6. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #6
  Mar 19, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,103
  Likes Received: 22,144
  Trophy Points: 280
  Tanzania haijaanza kukaa kiza kipindi cha JK, nakumbuka alipoingia madarakani alirithi kiza kikubwa kutoka kwa??? Utajaza mwenyewe. At least JMK anafanya jitihada za kweli za kukiondoa kiza. Wa kabla yake, wooooote, walifanya nini?
   
 7. Shedafa

  Shedafa JF-Expert Member

  #7
  Mar 19, 2011
  Joined: May 21, 2008
  Messages: 802
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Kweli mapenzi upofu na ukipenda chongo utaita kengeza, yetu macho!.
   
 8. m

  mambomengi JF-Expert Member

  #8
  Mar 19, 2011
  Joined: May 16, 2009
  Messages: 829
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  Umesema vema kabisa, Jitihada zake zimesaidia kulipa gharama ya ufadhili aliopewa kuingia Ikulu............Hicho ndicho unachofuatilia na Matatizo ya Umeme yanazidi kuongezeka. Kumbuka yeye ni Rais na aliomba ridhaa ya wananchi wamchague ili kuleta maendeleo ya nchi na wala sio blabla, usanii na ujambazi wa mali za umma. Si haba ni wewe ummoja wa wanaofisaidi malihasili ya nchi yako kwa faida ya tumbo lako na familia yako.
  Mwisho unahitaji kwenda Loliondo kupata Kikombe kimoja kutwa mara tatu toka kwa babu.
   
 9. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #9
  Mar 19, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  ... kelele!!!
   
 10. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #10
  Mar 19, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  hawa jamaa ni marafiki wa karibu,so sijawahi ona rafiki akimkemea rafikie kwa swala la ulaji,ukizingatia urafiki ndio uliofanya Ngereja kuteuliwa hapo alipo
  hehehehe,naungana na mwana jf kuwa ni mchezo wa kuigiza tuuuu
   
 11. Mzee Wa Rubisi

  Mzee Wa Rubisi JF-Expert Member

  #11
  Mar 19, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 1,754
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Mkuu omuonei huruma kiongozi wako unayemwabudu. Kihama kinakuja kama hakuwa makini akaacha masiala,kwa sasa hakuna ndio mzee,unaongea jaamaa wanaguna.
   
 12. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #12
  Mar 19, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  hawa ndiyo viongozi tulio watuma kwenda kutuwakilisha, iko siku tutawasubilia uwanja wandege sikwania ya kuwapokea...
   
 13. Dumelambegu

  Dumelambegu JF-Expert Member

  #13
  Mar 19, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 1,052
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Tumechoka kusikia upuuzi wa aina hii!
   
 14. K

  Kijallo JF-Expert Member

  #14
  Mar 19, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 409
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  ni mrad gani ulioanza kipindi cha Boss wako na ukazinduliwa?kila mradi aliozindua boss wako Jk,ilianza kipindi cha ????unamjua mwenyewe!miaka mitano ya Jk ni awamu ya uzinduaji,hilo la umeme ni maneno tu,hakuna utekelezaji.
   
 15. dudus

  dudus JF-Expert Member

  #15
  Mar 19, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 7,764
  Likes Received: 6,084
  Trophy Points: 280
  Si huyu huyu aliyewahi kusema "mwacheni mzee apumzike?" Kama kwa hoja yako uzembe wa kuliingiza taifa kizani ulianza kabla ya uongozi wake hakutakiwa kumwacha apumzike, ilikuwa ni wajibu wake kumhoji huyo mzee. Vinginevyo, kufumbia macho uzembe wa mtu mzembe ilhali ukijua ni mzembe basi wewe ni mzembe zaidi. Vinginevyo, kama kiongozi mkuu wa dola hujui uzembe unaofanywa na wasaidizi wako au waliokutangulia, then it is even worse.
   
 16. Lukansola

  Lukansola JF-Expert Member

  #16
  Mar 19, 2011
  Joined: Sep 5, 2010
  Messages: 5,456
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Ndivyo alivyodanganywa na wasaidizi wake, kwamba aanze kuongeaonga tu maana naina ni kama ametoka usingizini hivi, mambo anayoyasema leo alitakiwa kuyasema siku nyingi sana, infact kama agekwa kiongozi makini yasingetokea kabisa, maana watendaji wake wasinguthubutu kufanya upuuzi huku wakiujua msimamo wa boss wao. mimi nilidhani angemfukuza kazi. mnakumbuka wakati wa kampeni JK aliwapigia kampeni laivu Mramba, Chenge na Rostam huku akisema RA ameenea kama mtandao wa vodacom, mimi sina imani naye.
   
 17. J

  JITA New Member

  #17
  Mar 19, 2011
  Joined: Dec 7, 2010
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tumewatumaa au wamejituma ili wapate per diem zao?
   
 18. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #18
  Mar 19, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,179
  Likes Received: 895
  Trophy Points: 280
  CRAP (ya JK)
   
 19. P

  Proud Patriot JF-Expert Member

  #19
  Mar 19, 2011
  Joined: Oct 13, 2010
  Messages: 220
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  WTF? Did i read backwards or summ'? majerenereta yataingia ''kati ya wiki ya pili au ya tatu ya mwezi aprili'' na umeme kuzalishwa mwezi wa saba! So mgao mpaka july? THIS CAN ONLY HAPPEN IN THE UNITED REPUBLIC OF ALF LELA U LELA
   
 20. Mipangomingi

  Mipangomingi JF-Expert Member

  #20
  Mar 19, 2011
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 2,719
  Likes Received: 980
  Trophy Points: 280
  Kwani lazma uchangie? Issue iko hivi we majimshindo, jk anamtaka ngeleja awe makini, hii maana yake kwa sasa ngeleja siyo makini! But mamlaka ya ngeleja ni jk,ndo kusema kama mchaguliwa si makini bac pia mchaguaji naye si makini! Otherside,kama yy jk anadhani makini bac amtafute mtu makini amuweke pale nishati sio ngeleja ambaye ameshamuona kuwa si makini!
   
Loading...