Eti hujitongozesha kwa Mabosi! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Eti hujitongozesha kwa Mabosi!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mtambuzi, Aug 1, 2011.

 1. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #1
  Aug 1, 2011
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Kuna dhana kwamba wanawake walioajiriwa wanakabiliwa na mazingira ambayo yanawalazimisha kuingia kwenye vitendo vya kutoka nje ya ndoa zao, ukilinganisha na wanawake ambao hawajaajiriwa hususani mama wa nyumbani jambo ambalo katika maisha ya kawaida bila utafiti linaonekana kama vile ni kinyume yaani akina mama walio majumbani ndio ambao hutoka nje zaidi.

  Niliwahi kuwahoji wanawake kadhaa jijini Dar, mwanamke mmoja kati ya watano alikiri kwamba yuko tayari kujitongozesha kwa bosi ili kujaribu kulinda nafasi yake kazini au kupandishwa cheo. Nilifanya mahojiano hayo ili kujua idadi wanaume wanaotumia nafasi zao kazini kuwadhalilisha wanawake kijinsia.

  Lakini bila shaka suala la mapenzi kwa wanawake walioajiriwa lina nguvu na kwa hiyo limekuwa likifanyiwa tafiti katika sehemu mbalimbali duniani. Tofauti na tafiti ambazo zimefanywa hivi karibuni zinaonyesha kwamba mwanamke mmoja kati ya kumi walioajiriwa huwa anaonyesha tabia za kimapenzi au kujitongozesha kwa bosi wake.

  Tafiti hizi zinaonyesha kuwa yule mmoja kati ya kumi ambaye hujitongozesha kwa bosi huishia kutembea naye au hata kuolewa naye kama hana mume na pengine kuvunja ndoa yake. Inaelezwa pia kuwa mmoja kati ya wanawake kumi wanaojitongozesha kwa mabosi huwa anapandishwa cheo. Hii ina maana kwamba wanawake wanaopandishwa vyeo kwenye maeneo ya kazi huenda mmoja kati ya kila kumi hupandishwa kwa sababu za kimapenzi hata hivyo siyo lazima iwe hivyo.

  Tafiti hizo hata hivyo hazikulenga katika kuonyesha kwamba wanawake ni dhaifu bali huenda zimelenga katika kuonyesha kwamba idadi ya wanawake wanaojitongozesha kwa mabosi ni ndogo kuliko inavyotazamwa au kuaminika na pia kuonyesha kwamba bado wanawake walioajiriwa wako kwenye nafasi kubwa zaidi kushiriki mapenzi kuliko wale walioko majumbani. Ni juu ya wanawake ambao wanadhani ni halali kuuza thamani zao kwa ajili ya kazi kubadili mwenendo huo..
   
 2. Masaki

  Masaki JF-Expert Member

  #2
  Aug 1, 2011
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,465
  Likes Received: 163
  Trophy Points: 160
  Ngoja Wabeijing waje hapa. Mbona utajibeba leo....!!
   
 3. ABEDNEGO

  ABEDNEGO Senior Member

  #3
  Aug 1, 2011
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 109
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Tafiti zako hazina data! Zilifanyika katika mazingira gani? Ughaibuni ni tofauti
   
 4. Yasmin

  Yasmin JF-Expert Member

  #4
  Aug 1, 2011
  Joined: Jul 28, 2011
  Messages: 242
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  <br />
  <br />
  unamaanisha wanawake ni gold digger ama vipi
   
 5. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #5
  Aug 1, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  Hiii topic ni very deep
   
 6. Rashdind

  Rashdind Senior Member

  #6
  Aug 1, 2011
  Joined: Jul 19, 2011
  Messages: 195
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  We acha tafit za uchochoron sio za kuleta uku bwana.
   
 7. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #7
  Aug 1, 2011
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,113
  Likes Received: 3,035
  Trophy Points: 280
  deep sana
   
 8. Smile

  Smile JF-Expert Member

  #8
  Aug 1, 2011
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 15,427
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  hv unajua procedure za kupandishwa cheo? sasa sijui utatembea na mabosi wangapi maana icho cheo kitakuwa cha kichina watu wajanja siku hz?
   
 9. FiQ

  FiQ JF-Expert Member

  #9
  Aug 1, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 479
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  hamna Bebii ukikubali kutoa mambo cheo lazima upate, hasa kwenye taasisi na mashirika, lakin kwa hawa wa uswazi mfano walimu hata wakitoa penzi kwa head master imekula kwao mana bosi hana uwezo wa kugawa vyeo i mean cheo kinachopanda sambamba na mshahara.
   
 10. Azimio Jipya

  Azimio Jipya JF-Expert Member

  #10
  Aug 1, 2011
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 3,370
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Justifications pls!!
   
 11. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #11
  Aug 1, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,014
  Likes Received: 417,269
  Trophy Points: 280
  in comparison to what??????????????
   
 12. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #12
  Aug 1, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,014
  Likes Received: 417,269
  Trophy Points: 280
  ndani ya ccm upandishwaji wa vyeo kwa wanawake kunategemea sana kama anatoa rushwa ya ngono..........hata Jk alikwishasema yakuwa ili ule lazima uliwe..................................kwa hiyo inside ccm ratio is approximately one to one............................kati ya mtoa ngono na yule wa halali
   
 13. Gaga

  Gaga JF-Expert Member

  #13
  Aug 1, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 4,565
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  mhhh kwa kweli hii ni deep,ila kila mwanamke ana hulka yake mwingine hata apewe nn hayuko tayri kutembea na bosi wake
   
 14. Elia

  Elia JF-Expert Member

  #14
  Aug 2, 2011
  Joined: Dec 30, 2009
  Messages: 3,442
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Mmmmmh, kweli ipo deep! hata vyuoni wapo.
   
 15. M

  Mjenda Chilo JF-Expert Member

  #15
  Aug 2, 2011
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 1,425
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 145
  Hujaiweka vizuri, kujitongozesha au kutongoza ni jambo la kawaida sana, iwe kwenye daladala, kazini, shule au popote ndo wazazi wetu walivyokutana mpaka tukazaliwa. ngoja niinogeshe point yako, ila watoto najua hawatanielewa.

  Wanawake au kwa maneno mengine, wake za watu walioolewa kutembea na mabosi au niite wafanyakazi wenzao imekuwa ni tatizo kubwa ambalo limeharibu familia nyingi sana, kama hujui uliza utaambiwa.

  my take: Hii ni tabia ya malaya, hata kama jirani yake au mtu wa karibu atakuwa ni mbuzi au ng'ombe dume basi atatembea nae. mi nachukulia huyo atakuwa kama kunguru mwingine wa zanzibar yani hafugiki, ombi kwa wanaume wenzangu, ukigundua na ukawa na uhakika dont hestate, PIGA CHINI.
   
 16. nyumba kubwa

  nyumba kubwa JF-Expert Member

  #16
  Aug 2, 2011
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 10,278
  Likes Received: 1,716
  Trophy Points: 280
  That goes both ways. Hao wafanyakazi wenzie na hao mabosi anaotembea nao ni waseja? Au serengeti?

   
 17. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #17
  Aug 2, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180
  Mtambuzi analysis yako is really good and unfortunately true in most cases&#8230;.

  Ila tu nataka nikurekebishe kua huu utafiti umelengesha saana nafasi ya huyo mwanamke katika hio relationship (in the sense ya kutongoza).. naona kama iko biased&#8230; Mara nyingi ni kua Maboss ndio wanamtindo wa kutongoza katika issue nzima inayohusu wanawake waloolewa&#8230; Na saa ingine wala hata sio sababu za kutaka kuhonga au kumpa kitu fulani&#8230; Inakua tu tokana na ukweli kua tokana na ukaribu wao wa mara kwa mara wanaingia katika issue zima ya kuvutiwa kwa kila mmoja na kujikuta katika dimbwi la mapenzi&#8230; Na siku zoote Boss ana mwanamke wake anampenda, nafasi kitoka nzuri na Yule mwanamke ataweza ku cover basi ujue hio nafasi inevitably ya Mpenzi wake huyo&#8230;

  Katika issue zima ya kujitongezesha kwa wanawake kwa ma Boss, mara nyingi saana hutokea kwa wadada ambao hawajaolewa&#8230; huyu kweli mara nyingi hujitongozesha ingawa sio woote tokana na sababu tu kua anajua she can reach places akiwa na Boss na kuchukulia advantage&#8230;

  However note that idadi ya wanawake wanaotembea na bosses zao ni nyingi mno lakini ni wanawake wachache saana huweza fika mbali kisa tu she is sleeping with the Boss&#8230;. If the lady has brains na ana focus yaweza msaidia, but mwingine kweli ni mzuri na ni mrembo with no brains attached &#8211; huyu hum cost saana&#8230; (mtanisamehe wadada &#8211; just being real na nimelenga wale wachache); Na mara nyingi kwa mke wa mtu anaetembea na Boss sio nasisitiza kwamba sio tu kwa nia ya kuokoa kazi au kupanda cheo&#8230; sa ingine ni mafilingi tu!
   
 18. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #18
  Aug 2, 2011
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,672
  Trophy Points: 280
  <br />
  <br />
  Reality!!!!!!!!!
   
 19. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #19
  Aug 2, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Nimeupenda huu utafiti, true in most cases.
   
 20. Kaunga

  Kaunga JF-Expert Member

  #20
  Aug 2, 2011
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 12,590
  Likes Received: 797
  Trophy Points: 280
  Thanks AshaDii; kwa uchambuzi mzuri!
  Nilitaka kuhighlight some of the things ulizosema, guys mwanamke naye anapenda hii ni haki yake pia kama ilivuokupendwa! Boss pia ni binadamu first so naye anapendeka; kuna added value as a leader anazipata kutokana na kuwa na nafasi ya kuziexpress tokana na kuwa na jukwaa 'uboss' mf kuonesha authority, may be kujali, kuwa problem solver etc! Kama siyu bully sana, huwa admired by many both men n women!

  Sasa tukirudi kwa wanawake, it is true wengi wetu admiration na love tunachanganya sana; na hujikuta tukionesha au kupenda kuwa karibu na huyo mtu! Very few kama ADii alivyosema hasa wale wazuri bila brains intention Yao ni kubebwa, na mara nyingi wao hata boss asiwe na quality nzuri wao haijalishi watagawa tu! I have a boss ambaye hutaka kufinua every skirt, lkn kuna watu katudhindwa na tunachukiwa kishenzi!

  So kusummarize hayo juu, a woman has a right to love too, na anaweza kufall kwa driver, boss, chai boy etc! Mazingira ya kazi hufanya watu kuwa karibu na kujuana na that might lead into admiration n affairs or ndoa!
   
Loading...