Eti dar watu hawashibi?

Eti dar watu hawashibi?

herimimi

Member
Joined
Aug 4, 2011
Posts
62
Reaction score
10
Bibi mmoja toka kanda ya ziwa,kabila nalihifadhi,alikuwa amekuja kumtembelea mtoto wake hapa dar. Alikaa kama miezi sita hivi na mwanawe. Maisha yao yalikuwa mazuri tu kwani walikuwa wanakula na kunywa kama kawaida. Siku moja bibi akamwambia mjukuu wake, mimi nimechoka maisha ya dar nataka kurudi kwangu angalau nikapate choo! Mjukuu akashangaa, kwani bibi hupati choo? Akasema kule kwetu mtu unapata choo kwa siku mara 2 au 3, hapa kwenu mara 1 baada ya siku tena kwa kulazimisha! Hee mjukuu kabaki anashangaa.wataalamu wa lishe mpo?
 
choo kilikuwepo, tatizo hakuwa anaenda kama akiwa kwake!
 
Sasa kama mtu anapewa kawali kwenye kisosi atapataje choo?mwenzenu alizoea kugonga sinia zima na maji lita 2,wacha aende zake akajinafasi kwake.
 
Back
Top Bottom