Jioni ya leo tar 20 May 2013 nilibahatika kutazama kikao cha bunge la jioni. Hii ilitokana na kuahirishwa Spika Makinda kuahirisha kikao cha asubuhi baada ya Mbunge wa ccm Godfey Zambi kuomba muongozo kwa spika kutokana na alichodai kua hotuba ya Kambi rasmi ya upinza Bungeni iliyokua ikisomwa na Waziri kivuli Joseph Mbilinyi ilikua ni ya uchochezi.
Baada ya bunge kuahirishwa asubuhi,....jioni nilikua na hamu sana kujua mwisho wa Igizo hilo la Spika na Godfrey Zambi utaishia wapi na utaishaje!
Nyote tulishuhudia jinsi sakata lile lilivyoisha kwa Sugu kusoma hotuba yake yote japo bado Zambi aliomba mwongozo lakini Spika alimkatalia na kusema kuwa Hotuba hiyo ya Kambi ya Upinzani ukurasa wa 1-14 haitakua Rekoded.
Jambo la kushangaza kama sio kuuzunisha,akichangia hotuba hiyo ya Wizara ya Habari Vijana Utamaduni na Michezo, Mbunge mmoja Viti maalum Ccm(Jina limenitoka) alisema kwamba Vijana 60% Tanzania Matumaini yao yapo Ccm na kwamba yale walioyasikia muda mfupi uliopita kutoka kwa "Wasanii" Ni Sanaa! Nadhani alimaanisha hotuba ya Mh Joseph Mbilinyi(Sugu). Na wasidanganywe na waigizaji kwani Mugizaji anaweza kuigiza analia na wewe ukalia kiukweli.
Serikali ya CCM kwa miaka yote wamekua na wimbo wao wa kusema Vijana ni Taifa la kesho na sio la leo. Mh huyu anavyodai kuwa Mategemeo ya Vijana yapo Ccm je ni kwa yepi ambayo ccm inaweza kujivunia kuwa imewatendea vijana wa nchi hii? Kauli ya mheshimiwa huyu ni ya uongo na ya Kisanii! Vijana tuamke na tuikatae Ccm kwa kuwa hawana jipya wala hawana Nia na Mipango madhubuti ya kutukomboa na hali ngumu ya maisha zaidi sana wanataka kutuhadaa.