Sam Gidori
Senior Member
- Sep 7, 2020
- 165
- 414
Serikali ya Ethiopia imetangaza hali ya hatari katika jimbo la Kaskazini la Tigaray baada ya Waziri Mkuu wa taifa hilo, Abiy Ahmed kulaumu Serikali ya majimbo inayoongozwa na upinzani kushambulia vikosi vya Jeshi vya serikali.
Taarifa ya Ofisi ya Waziri Mkuu inasema kuwa matukio ya vurugu yanayotekelezwa na Serikali ya Majimbo ya Tigaray inavunja Katiba ya nchi hiyo na kuhatarisha usalama.
Kauli hii ya Abiy inaashiria kuanza kwa shughuli za kijeshi katika eneo hilo la kaskazini, kwa mujibu wa msemaji wake, Billene Seyoum, alipozungumza na Shirika la Habari la Reuters.
Katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter, Abiy aliandika: "Majeshi yetu ya ulinzi yameagizwa kufanya operesheni ya kuliokoa taifa. Mstari wa mwisho umevukwa. Nguvu itatumika kuwalinda watu wetu na taifa letu."
Serikali ya Jimbo la Tigaray ilifanya uchaguzi wake mwezi Septemba, uchaguzi uliohesabiwa kama 'haramu' na Serikali Kuu, huku pande zote mbili zikishutumiana kupanga njama za mashambulizi ya kijeshi dhidi ya mwingine.
Chanzo: Al Jazeera