ESTIM Construction ni kampuni ya nchi gani?

Mkuu hizo gharama unazitoa wapi. Pia estim ni contractor wa pili baada ya wa kwanza kufukuzwa.


Du....kweli eewe ndio hujui kitu.
Mchina hakutia mguu mradi wa Msata Bagamoyo.
Kazi ilikuwa estim mwanzo mwisho, tena kwa gharama za kutisha Tshs 2bn kwa kilometa!
Ulizia Tanroads upate facts.
Hapa si chit chat.
 
Kwa kweli nami nawawakubali wamejenga mitaa ya makumbusho Barbara zimetulia. Njoo Sasa hawa delmonte na can...wamejenga Barbara ya mbweni isharudiwa Mara mbili wapi, Makonda alikuja na mkwala wa kuzifungia akafeli, sijui alipewa Mambo ya fedha akanyamaza ama vipi
 
Ndio wameshusha ile kitu moroccco square.
Kitu kimesimama hatari
 
Wewe ndio Eng. mzawa ee? Au nyie ndio maEng wa mkoa?
Wajinga kabisa.

Tanlalila nyiiiiingi. Kazi ziro.

Huyu jamaa alichokiongea kina ukweli kwa mwananchi wa kawaida regardless na elimu zenu sijui madaraja chini sijui earth road,gravel road sijui double.hayo mtajua nyie.

Kwanza tubie kwa nini mliruhusu kupitisha BRT pale jangwani bila daraja?
Jibu hilo swali.
Unavyojifanya kumpinga mleta mada unatupigia tu makelele kwa sababu hata sisi tunaona
 
Umesema alikuwepo mchina , tupe jina.
Ya TAKOPA tunayakumbuka fika.
Gharama ulizo refer ni pamoja na madaraja matatu pale mto Ruvu?
 
Kwa uzoefu wako kama mhandisi mzawa unadhani ile kazi iliyofanyika pale kwenye lile bonde ni ya kitoto?
Umesema alikuwepo mchina , tupe jina.
Ya TAKOPA tunayakumbuka fika.
Gharama ulizo refer ni pamoja na madaraja matatu pale mto Ruvu?
 
Estim wako vizuri sana.... na kinacho nifurahisha hawa jamaa wana vitendea kazi maana hata kama mtu si mtaalam unaona wazi hapa kuna muelekeo mzuri kabisa.
 
Taratibu muzee bado tuko Eid pili.
 
Ni kampuni inayomilikiwa na mtanzania mwenye asili ya Uhindini (Uraia wa kusajiliwa)

Hivyo kuiwezesha kusajiliwa kama kampuni ya kizawa

Ni kampuni daraja la kwanza (1) kwenye majengo na uhandisi wa miundombinu jamii.
Uraia wa kusajiliwa ndiyo wa aina gani mkuu? Hapa nimetoka kapa mkuu😀
 
Wanachonikera hawa jamaa wanaojenga barabara ya Kimara ni kutokuwa na utaratibu wa kuweka njia mbadala ili kusiwe na msongamano. tunajua kwamba eneo hilo kuna nyumba nyingi zimebomolewa ili kupisha ujenzi wa barabara na kwa hiyo kuna nafasi kubwa sana ya kuweka njia mbadala. kuna viwanja viwili vya mpira hapo katika upana wa barabara. Sasa badala ya kujenga service road za uhakika ili kusiwe na msongamano, tumeshuhudia misururu mirefu ya magari hivi karibuni kutokana na style wanayotumia kujenga ambayo siyo rafiki kwa barabara yenye watumiaji wengi kama ilivyo morogoro road. yaani kwa hilo hawa jamaa MIMI NAWALAANI KABISA WAKAFILIE MBALI
 
Picha ya huko kimara hadi kibaha wanapojenga hio barabara ipo wapi? Na ya hayo majengo?
Kwani upo kipori mkubwa nenda mbezi mwisho kuelekea kibamba utaona picha zitakudanganya
 
Barabara yote ya zamani bado ipo labda sema kuna eneo ambalo rafiki yangu siku moja amekaa karibia saa 1 ambalo ni mbezi darajani ikitokea kibanda cha mkaa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…