Aliyekuwa mwanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Esther Matiko Jumapili Juni 29, 2025 ametangaza nia ya kuwania nafasi ya Ubunge Jimbo la Tarime Mjini kupitia chama tawala, Chama Cha Mapinduzi (CCM)
Akizungumza na wanahabari, Matiko kando ya kuwashukuru Watanzania kwa kumuungano mkono katika safari yake ya kisiasa, amebainisha kuwa maamuzi ya kuhamia CCM na kuwania nafasi hiyo hayajatokana na jazba ama kutafuta maslahi binafsi na hajadhamiria kuwakatisha tamaa Watanzania wanaomuunga mkono
Amesema amefikia hatua hiyo kutokana na tafakari yake, hali ya Tarime Mjini na matarajio makubwa ya wananchi, akibainisha kuwa kupitia CCM anaamini kuwa ndoto hizo zitatimia na kutafsiriwa kwa vitendo, akiahidi kuwa sehemu na suluhisho la maendeleo ya Tarime Mkoani Mara
Akiwahakikishia kuwa safari yake ya sasa ni ya matumaini, Matiko amebainisha kuwa Ilani ya CCM ya mwaka 2025/30 ni miongoni mwa mengine yaliyomfurahisha, akisema Ilani hiyo imetoa kipaumbele kikubwa katika huduma za kijamii nchini, huku pia akionesha kuvutiwa na dhamira njema ya Rais Samia na maendeleo makubwa aliyoyafanya ndani ya miaka yake minne ya awali kama Rais wa Tanzania
Soma pia: Esther Matiko sasa ni mwanachama wa CCM