GE2025 Esther Matiko ataja sababu za kujiunga CCM

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
1. Kwani mbunge wa sasa wa Tarime Mjini ni nani na je hagombei tena?
2. Vipi wale makada kindaki kindaki wa CCM wafia chama waliokuwa wanapambana na upinzani mchana na usiku hakuna hata mmoja anayegombea iwapo mbunge anayemaliza muda wake hagombei?
3. Je CCM ina utaratibu gani kwa makada wapya wanaotoka kwenye vyama vingine kuhusu kugombea nafasi mbali mbali kama uraisi, ubunge na udiwani? Je kuna muda maalum wa kuwa chini ya uangalizi kabla ya kupewa nafasi ya uongozi na kama upo ni muda gani?

Ni mtizamo tu.
 
Ukweli mchungu, na ndio shida ilipo Africa, watu wote wanataka kupiga domo na sio kufanya kazi.

Ukiangalia taasisi zote ambazo watu wake wanaishi vizuri kwa kulipana mishahara minono na posho, they are not productive.

Siasa ina maslahi makubwa kwa kuzalisha absolutely nothing.
 
Ujinga na uupuzi mtupu... wamtose kama condom, ndiko anako stahili- period! kama inavyovuja kila mwezi. samahanini kwa kutimia maneno makali...
 
Esta matiko na Esta bulaya wote wamerud Ccm?! Hua wananichanganya hawa matapeli wa siasa.
 
Siwapendi CCM ila mkimpiga chini huyu nitafurahi sana.
unatakiwa ukomae kisiasa na uache mihemko, mtu akihama chama ni haki yake kabisa yeye ni mwana siasa na sio mwana chadema
 
Aliyekuwa mwanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Esther Matiko Jumapili Juni 29, 2025 ametangaza nia ya kuwania nafasi ya Ubunge Jimbo la Tarime Mjini kupitia chama tawala, Chama Cha Mapinduzi (CCM)

Akizungumza na wanahabari, Matiko kando ya kuwashukuru Watanzania kwa kumuungano mkono katika safari yake ya kisiasa, amebainisha kuwa maamuzi ya kuhamia CCM na kuwania nafasi hiyo hayajatokana na jazba ama kutafuta maslahi binafsi na hajadhamiria kuwakatisha tamaa Watanzania wanaomuunga mkono

Amesema amefikia hatua hiyo kutokana na tafakari yake, hali ya Tarime Mjini na matarajio makubwa ya wananchi, akibainisha kuwa kupitia CCM anaamini kuwa ndoto hizo zitatimia na kutafsiriwa kwa vitendo, akiahidi kuwa sehemu na suluhisho la maendeleo ya Tarime Mkoani Mara

Akiwahakikishia kuwa safari yake ya sasa ni ya matumaini, Matiko amebainisha kuwa Ilani ya CCM ya mwaka 2025/30 ni miongoni mwa mengine yaliyomfurahisha, akisema Ilani hiyo imetoa kipaumbele kikubwa katika huduma za kijamii nchini, huku pia akionesha kuvutiwa na dhamira njema ya Rais Samia na maendeleo makubwa aliyoyafanya ndani ya miaka yake minne ya awali kama Rais wa Tanzania

Soma pia: Esther Matiko sasa ni mwanachama wa CCM

Hizo ni mbwembwe tu hakuna jipya...huyu kashanogewa na mchezo wa kuvuna mamilioni ya Kodi za watanzania bila jasho.Alizokula zinamtosha...
 
Ukweli mchungu, na ndio shida ilipo Africa, watu wote wanataka kupiga domo na sio kufanya kazi.

Ukiangalia taasisi zote ambazo watu wake wanaishi vizuri kwa kulipana mishahara minono na posho, they are not productive.
Kwa afrika siasa ni eneo la kuvuna bila kupanda, kula bila jasho...
 
Esta matiko na Esta bulaya wote wamerud Ccm?! Hua wananichanganya hawa matapeli wa siasa.
Washarudi kwenda kuendelea kuvuna Kodi za watanzania Bure, ningekuwa mie ndo mpiga kura mbunge yeyote aliyekaa bungeni kuanzia miaka kumi ni kupingwa chini, wale na wengine
 
Esta matiko na Esta bulaya wote wamerud Ccm?! Hua wananichanganya hawa matapeli wa siasa.
Kwa sababu wanaitegemea siasa kuendesha maisha yao. Pesa waliyovuna huko muda wote bado wanashindwa kujiajiri na kung'ang'ania kazi ya kwenda kuhimiza wengine wajiajiri.
 
Esther Matiko aliyekaa ndani kwa sababu alikuwa mpinzani. Aliyepigwa kwa sababu ya kuwa mpinzani. Aliyekuwa Mwenyekiti wake akiwa pamoja na yeye na Esther mwenzake walihukumiwa kifungo mpaka walipolipiwa faini na wananchi. Mwenyekiti wake huyo huyo alikaa mahabusu kwa miezi zaidi ya saba. Mwenyekiti wa chama hicho kwa sasa yuko rumande kwenye shauri ambalo akipatikana na hatia anaweza kunyongwa. Leo akiwa na macho makavu anasema chama chake kipya kina historia ya kuunganisha wananchi! Kinachosikitisha zaidi ni kuwa kuna uwezekano mkubwa atarudi bungeni kujiunga na wenzake wapiga meza. Anasikitisha sana.

Amandla....
 
Aliyekuwa mwanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Esther Matiko Jumapili Juni 29, 2025 ametangaza nia ya kuwania nafasi ya Ubunge Jimbo la Tarime Mjini kupitia chama tawala, Chama Cha Mapinduzi (CCM)

Akizungumza na wanahabari, Matiko kando ya kuwashukuru Watanzania kwa kumuungano mkono katika safari yake ya kisiasa, amebainisha kuwa maamuzi ya kuhamia CCM na kuwania nafasi hiyo hayajatokana na jazba ama kutafuta maslahi binafsi na hajadhamiria kuwakatisha tamaa Watanzania wanaomuunga mkono

Amesema amefikia hatua hiyo kutokana na tafakari yake, hali ya Tarime Mjini na matarajio makubwa ya wananchi, akibainisha kuwa kupitia CCM anaamini kuwa ndoto hizo zitatimia na kutafsiriwa kwa vitendo, akiahidi kuwa sehemu na suluhisho la maendeleo ya Tarime Mkoani Mara

Akiwahakikishia kuwa safari yake ya sasa ni ya matumaini, Matiko amebainisha kuwa Ilani ya CCM ya mwaka 2025/30 ni miongoni mwa mengine yaliyomfurahisha, akisema Ilani hiyo imetoa kipaumbele kikubwa katika huduma za kijamii nchini, huku pia akionesha kuvutiwa na dhamira njema ya Rais Samia na maendeleo makubwa aliyoyafanya ndani ya miaka yake minne ya awali kama Rais wa Tanzania

Soma pia: Esther Matiko sasa ni mwanachama wa CCM

Masahihisho: Hakuwa Mwanachama wa Chadema, Alishatimuliwa mithili ya nyau aliyekunywa maziwa ya mtoto
 
Kwamba Toka uhuru tarime inaongozwa na chama gani?
 
Back
Top Bottom