Esther Bulaya VS Esther Wassira

Nani utampa kura yako ubunge Bunda kati ya Steven Wasira (CCM) na Esther Wasira (Chadema) ?


  • Total voters
    112
Status
Not open for further replies.
Ester Bulaya anaonekana anatumia sana "hoja ya nguvu" katika ushawishi wakati Ester Wasira anatumia "nguvu ya hoja".
Jana Ester Wasira nilimchek akijenga hoja, ni mzuri katika kushawishi, anajiamini, anajua nini anakisema peke yake bila kusimamia miguu ya chama. Bulaya anatumia sana miguu ya chama kusimama.
 
Esther Wassira kwa kweli sio mzuri wa kujenga hoja tu ila hata sura anayo. Sikuwepo kwenye jukwaa la mwalimu lakini na nilimwona kwenye TV jana akanivutia sana sana learned counsel, nadhani kama vile natamani kumfahamu zaidi

For sure wewe utakuwa 'gamba' tuu
Kama unachagua kiongozi kwa kuangalia sura kwenye karne hii 'umekwisha'
 
tofauti ya wassira na bulaya ni kwamba wasira yupo chama chenye kupigania wanyonge wakati bulaya yupo chama cha majambazi, hakuna conflict kwani mchuano ni cdm na ccm, bulayo angelijua mapema angejiondoa mapema magamba na kujijenga akiwa cdm, lakini tayari cdm kuna jembe ester wasira sasa kilichobaki ni m4c kupelekwa bunda halafu mambo ni mia mia
 
Mimi bado sijafanikiwa kumona Esther Wassira ila Bulaya nimemuona mara nyingi bungeni.Nilichokiona kwake sip mjengaji hoja ila mbambiaji hoja.Uchangiaji wake mara nyingi ni wa cheap popularity analenga kitu bado anawakati ajifunze kwa watu kama Mnyika.But namushauri Wassira tumuone wkt wa M4C itakapokua Mara apande jukwani.
 
Esther Bulaya, Profile yake Gonga hapa (Muandishi wa Habari = Uhuru na Mzalendo!!!!!!!!!)

Parliament of Tanzania

Esther Wassira ni Wakili wa Kujitegemea.

Hebu acheni kufananisha hawa watu, hawalingani kabisaaa
 
Mi namshauri Esther Wassira ajipange. Nataka Mzee Wassira apumzishwe 2015. Huyo Esther Bulaya hata kama mzuri kiasi gani, yupo kwenye wrong platform kwa sasa.
Mkuu kimwonekano Esther Wassira yuko vizuri zaidi na anamvuto wa hali ya juu!!!
Esther Bulaya kimwonekano ni wa kawaida sana na hana mvuto wowote.
 
Huyu Esther Wassira ndiye yule mwanabongoflava aliyewika miaka ya mwanzoni mwa 2000 au majina tu yamefanana?(Wengine hatukuuona huo mdahalo)
Japokuwa huyo wa bongoflavour simkumbuki vizuri bado sioni mfanano wowote kimaumbile wala Kiupeo kati yao.
 
Mazindu mimi sikubaliani na hoja,acha E.W agombee na baba yake ili huyo mzee aaibishwe mbele ya wanabunda.W.kama ataona vipi atangaze nia ya kung'atuka bungeni
 
Avanti umetumia kigezo cha jana katika jukwaa la mwalimu au umeshawahi kumsikiliza mara za kutosha kiasi cha kufika kusema sio mzuri wa kujenga hoja mkuu?? kama ni cha jana peke yake, basi mpe nafasi ya kumsikiliza zaidi ndio uhitimishe kwa usemi wako wa blue

Ni vizuri mtu ukasoma kwa kutulia na kituo kwa kituo la sivyo unaweza kubadili maana ya mwenzako kabisaaaaaa!
 
Kuna haja ya kuanza kuangalia hvi vitu nje ya ubunge tu wajameni.
Naamini kutoka jana inbox ya E. Wasira imejaa washauri wa kumtaka ajipange kwa kugombea jimboni na "kuchukua" jimbo.
Siasa ni zaidi ya ubunge.
Ester Wasira atakuwa rasilimali makini ya chama na nchi kama atapata washauri watakao muelekeza vema kuhusu kutumikia siasa safi na sio kumjaza ndoto za ubunge!
Anahitaji kuwa mentored na mfumo wa chama kwanza, azielewe falsafa za chama, mambo ya ubunge ni matokeo.

Kuhusu huyo mwingine sitasema kitu sababu nilishaacha kuwazungumzia wanasiasa wa CCM!

Mkuu,
Umeongea kitu cha maana sana. Ubunge sio kila kitu...atumike zaidi kichama ktk kushawishi na kuchochea hoja
changamshi kwa vijana.

Yaani jana wakati tunaangalia hotuba yake nilikuwa na mgeni wangu nyumbani ambaye ni Mchungaji, kwa kweli
alidatishwa mpaka ikabidi usiku niitafute hotuba hapa JF na kumprintia pastor (10 pages) na leo amesafiri roho
yake ipo kwatu!!!

Kumlinganisha na E. Bulaya sio sahihi hasa ukizingatia hata ule ufafanuzi ulioutoa kwa vyombo vya habari kuhusu
matamko ya babake mdogo...duh I thought aliandikiwa ila jana ndo nimejua kuwa this girl is something else!
Hongera Dr. Slaa (na CDM) kwa kupata jembe, na kweli alistahili kukabidhiwa kadi na Katibu Mkuu!!!
 
kwanza esther wassira kujiunga chadema tayari kesha mzd mwenzake kwa kila ki2...ameonyesha ni jnc gan yupo makn
 
Sidhani kama uko sahihi. sio wajita wote mmojawapo muikizu. Na humu ndani makabila ya nn. kinachotakiwa uwezo wa mtu kuiongoza BUNDA regardless anatoka chama gani
Hamna muikizu hata mmoja kati yao kina Ester ni machotara
 
Mkuu kimwonekano Esther Wassira yuko vizuri zaidi na anamvuto wa hali ya juu!!!
Esther Bulaya kimwonekano ni wa kawaida sana na hana mvuto wowote.

Mkuu nachokiona pia ni kuwa kwa Ms Bulaya ni kwamba wengi walikuwa wakimlinganisha zaidi na Mzee Wassira ndio maana akaonekana ni nyota (wameangalia nani afadhali). Lakini kwa hili la Ms Wassira ni level nyingine kabisa. Maana licha ya umahiri wake wa kuzungumza, pia hayuko kwenye wrong platform ya ccm. Mkuu, ushawahi kumsikia Ms Bulaya akizungumza? Picture her addressing ule umati pale Nkurumah kama alivyofanya Ms Wassira.
 
Nimemsikiliza jana kupitia ITV Esther Wassira, ni kweli kabisa kwamba anajenga hoja, ana haiba ya kumiliki jukwaa na hata anaonesha anachokiongea anakimaanisha toka moyoni (Kumbuka kwamba wakati akiongea, ndio wakati huo huo Kikwete alikuwa akiongea kwenye TBC akiwa Shinyanga). Mwanzoni hapa kwangu watu walikuwa wana-prefer tuwe tunabadili badidi channel Tbc to ITV, kusikia jamaa huko Shinyanga anasema nini, lakini ilifika mahali (automatically tu) tukabaki ITV tu kumsikiliza E. Wassira). Nataka kusemaje: ana ushawishi wa hali ya juu!

Kwa kumlinganisha na Bulaya, mara nyingi nimemwangalia jinsi aongeavyo bungeni,huwezi kumlinganisha na Esther Wassira katika hii 'haiba ya jukwaani/kisiasa...unless mtu aje atuthibitishie kuwa nae anao ugonjwa wa wabunge wa CCM wa kutomaanisha wanachokiongea, na hata kutoishi uhalisia.
 
Mi naona ni vigum kumlinganinisha Esther Wasirra na Esther Bulaya kwani, watanzania wengi wamemsikia Esther Wasira kwa mara ya kwanza jana.Na hatujui consistency yake itakuwaje,na si rahisi kudraw conclusion yake kwa kumsikia mara moja tu!!Labda tumpe muda,lakin kwa upande mwingine Esther Bulaya tunamfahamu vizuri
 
Mi naona U CHADEMA addicted unafanya kazi tu hapa. Mtu kasikika mara moja, inatosha kumlinganisha na mtu aliyemsumbua WASSIRA siku nyingi hivyo?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom