Esther Bulaya VS Esther Wassira

Nani utampa kura yako ubunge Bunda kati ya Steven Wasira (CCM) na Esther Wasira (Chadema) ?


  • Total voters
    112
Status
Not open for further replies.
Labda mkuu Mchambuzi , atuwekee uchambuzi wao kwa hoja, naona kama ipo kishabiki, mtu badala ya hoja, kwa jana I vote for E,Wassira.
Hoja zao muhimu tumeshawahi kuzisikiliza kama sio kuzisoma. kwa mfano
*Esther Bulaya(Ameongea mara nyingi bungeni(Hansard za bunge), Kampeni za uchaguzi Igunga na Arumeru mashariki nk)

*Esther Wassira(Tamko lake la kujiunga CHADEMA, ufafanuzi juu ya mzozo ulioibuka kuhusiana na undugu na Steven Wassira, Hotoba yake kwenye kongamano la Kumbukumbu ya Nyerere.)

****Links zao zote zimo humu JF unaweza ukatafuta ukasoma na kisha ukachangia mwenyewe.
 
Last edited by a moderator:
[EMAIL=" Concrete" Concrete[/EMAIL],
Tumeanza kuona umuhimu wa midahalo, kwa wenzetu nchi zilizoendelea ndio sehemu pekee ya kuchambua pumba na mchele, binafsi namchukia Buyala toka campaign za uchaguz mdogo Igunga. unaikumbuka hii...

Recently the MP for Sumbawanga Urban, Mr Aeshi Hillally and Esther Bulaya (CCM-special seats) were allegedly ambushed at a rest house popular with CHADEMA supporters at Mwanzuki Road with the aim of torching CCM's campaign vehicle.

Chaos ensued as bullets were fired soon after CHADEMA security men were tipped-off of the situation and reacted.
Eye witnesses told reporters that the two MPs decided to run away to save their lives but their vehicles were already stoned by suspected CHADEMA security men.

Addressing press conferences at The CCM Campaign Manager, Mr Mwigulu Mchemba, said Ms Bulaya and Mr Hillary
were attacked by CHADEMA supporters while driving back to their guest house while CUF through Mr Lissu and the CHADEMA campaign Manager, Mr Mwita Waitara said the accused actually wanted to sabotage their opponent's campaign efforts.
 
Last edited by a moderator:
Mimi naona Ester Wasira ni zaidi. Mleta uzi hebu tuwekee na kura ya maoni tuangalie nani zaidi
 
ESTER wasira kwa kweli ni jembe la uhakika,kama MDEE vile, anajiamini ,anajenga hoja,anajua cha msingi sasahivi ajisogeze karibu kwa wananchi ambao ndio watakao mpigia kura.dada anaweza kwa kweli.
 
ITV wapambanisheni hawa wawili, katika mada fulani watu waone, Esta wasira ni noma, nimependa sana uwakilishi wake jana, sijui alikuwa wapi. What a brilliant young lady, it was so astonishing and strong incomparable presentation. Bunda ni ya kwake kama akiamua.
 
Mimi naona Ester Wasira ni zaidi. Mleta uzi hebu tuwekee na kura ya maoni tuangalie nani zaidi
Mkuu mimi sina utaalamu, ila nawaomba Moderator kama wanaweza kufanya hivyo waunganishe na kura ya maoni hapa hapa.
 
Wale wenye nafasi ya kuonana naye ana kwa ana (huyo Esther Wassira) wamshauri ili aanze maandalizi, hata ikiwezekane ashiriki kwenye M4C na kupewa nafasi ya kushambulia jukwaa ili aweze kujulikana zaidi. Mwenzake Bulaya licha kujulikana kutokana na nafasi yake ya Ubunge, pia alishaanza kujitangaza mapema huko Bunda kwa kufadhiri timu za mpira. Dr. Mkumbo tafadhari mshauri Esther (Wassira) namna ya kujitangaza zaidi kwa Wana-Bunda! Tunapenda kumwona mjengoni mwaka 2015!
 
Masikini mzee wa watu steven wasira wanammaliza watoto wake atakoma kuwakana.
ila hilo zee muda wake umeisha alikuwa mkuu wa wilaya miaka 30 iliopita
 
Kuna haja ya kuanza kuangalia hvi vitu nje ya ubunge tu wajameni.
Naamini kutoka jana inbox ya E. Wasira imejaa washauri wa kumtaka ajipange kwa kugombea jimboni na "kuchukua" jimbo.
Siasa ni zaidi ya ubunge.
Ester Wasira atakuwa rasilimali makini ya chama na nchi kama atapata washauri watakao muelekeza vema kuhusu kutumikia siasa safi na sio kumjaza ndoto za ubunge!
Anahitaji kuwa mentored na mfumo wa chama kwanza, azielewe falsafa za chama, mambo ya ubunge ni matokeo.

Kuhusu huyo mwingine sitasema kitu sababu nilishaacha kuwazungumzia wanasiasa wa CCM!
 
Upeo wa akili huamua busara na weledi wa mtu kuchambua hoja. Siasa ni fani na wala sio kipaji.
Esther Wassira ni moja ya wanawake wenye kaliba ya aina yake. Uwezo wake wa kuchanganya taaluma aliyonayo na nia ya kuleta ukombozi wa kweli ndio kiini vha weledi wa hoja zake.
Siku zote huwa naamini ni wakati sasa wa kuwaachia wanataaluma nafasi ya kuliweka taifa letu katika ramani.
 
Bulaya sio mjenga hoja, ana jazba, arrogant. Wassira ana kila attribute (sijui kwa bed), ila si vibaya nikijua! I wl make a follow up!
 
mnachekesha... hivi bunda ni nyama ya yowe inagawia hata kwa mpita njia... ukitaka kuijua Bunda muulizeni Cyprian Musiba
 
*Esther Bulaya ni mbunge wa kike, kijana kwa tiketi ya CCM viti maalum, watu wengi wamepata kumzungumzia uwezo wake wa kisiasa humu JF mara kadhaa. Ameonekana Bungeni na mara kadhaa kwenye majukwaa ya kisiasa akijenga hoja.

*Esther Wassira alionekana kwa mara ya kwanza kwenye ulingo wa kisiasa siku akichukua kadi ya CHADEMA, watu wengi walitaka kumfahamu uwezo wake wa kisiasa(kujenga hoja na kuamsha ushawishi), na kupitia hotuba aliyoitoa kwenye kongamano la kumbukumbu ya mwalimu Nyerere pale Nkurumah kila mtu sasa anaweza kumzungumzia.

*Sababu za kutaka kuwalinganisha kisiasa.
1/Mfanano wao (Wote ni wanasiasa, vijana, wanawake, wanatoka Bunda, wameshawahi kuwa na mzozo wa kisiasa na Steven Wassira, wote wanaitwa Esther!!)

2/Wanatoka vyama viwili vinavyopinzana.

3/Watu wengi wanataka kuona mmoja wao akirithi kiti cha ubunge wa Steven Wassira kule Bunda 2015.

***Wadau wa JF mnaweza kuchangia kwa kujenga hoja za ulinganifu wao kisiasa.

1.Esther Bulaya anaonekana ni mnafiki wakati ambapo Esther Wasira anaonekana anakiamini kile anachozungumza. 2.Esther Bulaya anazidiwa na mafisadi wakati ambapo Esther Wasira ni mwiba wa mafisadi. 3.EB NI MVIVU WA KUFIKIRI WAKATI EW NI GREAT THINKER.
 
Tatizo kwangu mtu akiwa ndani ya CCM ya SASA napata kigugumizi kidogo, anatafuta nini huko, ndio maana respect yangu iko kwa Ester Wasira.
 
Nukuu kutoka kwa mwana JF fulani wakati akijaribu kunielezea kuhusu Esther Bulaya.

''Esther Bulaya ni
1/MNAFIKI(kama walivyo wana CCM wengi),

2/MZUSHI(kama alivyotengeneza tukio kule Igunga)

3/MWOGA(kushindwa kwake kusema na kusimamia kile anachokiamini ndani ya bunge)

4/ANAJAZBA(Mara kadhaa ameonekana Bungeni na kwenye kampeni katika mood mbaya sana)

5/MZITO SANA KUJIELEZA(Inahitaji kumsikiliza kwa makini sana na kwa muda mrefu ili upate kumwelewa kwa ufasaha)'' mwisho wa kunukuu.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom