Esther Bulaya aanza kupigwa vita

Esther Bulaya aanza kupigwa vita

THINKINGBEING

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2010
Posts
2,779
Reaction score
1,304
Mkuu wa wilaya ya Bunda amepiga marufuku michuano ya kombe la mpira wa miguu iliyodhaminiwa na Esther Bulaya ITV imeripoti.Chama cha mpira wa miguu wilayani Bunda kimeiambia ITV kimepokea barua ya kusimamisha michuano hiyo kutoka kwa mkuu wa wilaya bila sababu zozote.Akihojiwa na ITV mkuu huyo wa wilaya alisema kwa mkato viongozi wa CCM hawaruhusiwi kusimamia michuano kama hiyo.
Esther Bulaya amekuwa akipigwa vita na viongozi wa chama chake CCM na hivi karibuni amekuwa mwiba kwa chama hicho kutokana na msimamo wake wa kudai serikali 3 kinyume na msimamo wa chama chake.Pia mbunge huyo ametuhumiwa mara kadhaa kuwa anatumiwa na CHADEMA.
 
...Katika kile kinachooneka kama ni kupigwa vita kwa mbunge Ester Bulaya na Mbunge wa sasa wa Bunda Wassira, mashindano yake yamepigwa marufuku wilayani bunda na mkuu wa wilaya ndugu Joshua Marumbe. Akiongea na simu na ITV mkuu wa wilaya Marumbe amesema, mashindano ya mpira wa miguu yanapaswa kusimamiwa na TFF na sio makada wa CCM. Akasema, sasa kuna vurugu ya kila mtu kutaka kuanzisha mashindano kwa maslahi binafsi na sio kwa maslahi ya wananchi.

My Take:

Hii ni dalili nzuri sana ya ukombozi wa Taifa hili, nawaombea heri Esther na Wassira, naomba ikibidi hata wapigane kabisa. Naliona anguko la Wasira 2015.
 
Ukombozi upi unaouzumgumzia.
 
Mimi mwenyewe nimeona na kusikia ITV nikajua hapa lazima Wasira kapenyeza mkono wake! Nadhani Esther Bulaya analitaka jimbo hilo! Akaze buti kwani ninavyojua wananchi wameshajua kwamba wanasiasa wameingilia ili kumnyanyasa Esther Bulaya kwa kukwamisha mashindano yake! Yetu macho!
 
Kwani Ester Bulaya ni mzaliwa/mkazi wa Bunda?
 
1399056417351.jpg
Viongozi wake si hawa Wagonjwa walioaminisha watu ushirikina?
Wenyewe kutwa kusaka tiba zisizo na tbs unategea nn
1399056634718.jpg
Kijana ndo huyu anaangalia mama zake wakimwaga radhi
1399056793983.jpg
Ukiwa ccm utachekwa na visivyocheka.
 
bulaya hoja yake binafsi bungeni imewaudhi intarahamwe so asome nyakati arudi kwa cdm apambane asingoje kumwagwa kura za maoni ndipo akimbie
 
Sasa Wassira kipima joto kama hicho tayari pumzi zimemwishia, anaanza kutumia mashine! Halafu eti anajigamba anaweza kupambana na CHADEMA! Eti naye anafikiria kuwa rais! What a disgrace to our presidency institution jamani!

Bila dola CCM hawawezi kufanya siasa ya ushindani na wakashinda mahali popote. Bila shaka wanazidi kujiumbua.

Waziri mzima ametolewa jasho...no wonder alirudi CCM baada ya Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere kufariki. Watu wasio na uwezo na waso wasafi kama yeye wasingefikiria kugombea ubunge achilia mbali kuwa eti waziri na eti kufikiria kuwania urais! Shame on CCM!
 
Bulaya anawakilisha wapiga kura na si chama,Hao ndio wanao hitajika kwa kipindi hiki kuelekea 2015.
 
ndesamburo wa chadema ndio alikuwa mwanasiasa aliyesimama frontline kumtetea babu wa loliondo. Mpaka alitoa magari yake na helkopta ipeleke watu wakapate kikombe.

Mkuu picha ziko 3 si unajua mambo ni 3 siku hizi.
Ndesa alijitolea baada ya viongozi wakuu kuhakiki dawa hiyo lkn hakuinywa.
Vp huyo kijana na mama zake ndo heshima ya ccm?
 
ndesamburo wa chadema ndio alikuwa mwanasiasa aliyesimama frontline kumtetea babu wa loliondo. Mpaka alitoa magari yake na helkopta ipeleke watu wakapate kikombe.

...hii ndo hoja yako kuhusu bulaya..!st**pid,no wonder kwenye bunge la katiba mnatema mataputapu mliyokaririshwa bila kuwa na hoja...
 
Mkuu wa wilaya ya Bunda amepiga marufuku michuano ya kombe la mpira wa miguu iliyodhaminiwa na Esther Bulaya ITV imeripoti.Chama cha mpira wa miguu wilayani Bunda kimeiambia ITV kimepokea barua ya kusimamisha michuano hiyo kutoka kwa mkuu wa wilaya bila sababu zozote.Akihojiwa na ITV mkuu huyo wa wilaya alisema kwa mkato viongozi wa CCM hawaruhusiwi kusimamia michuano kama hiyo.
Esther Bulaya amekuwa akipigwa vita na viongozi wa chama chake CCM na hivi karibuni amekuwa mwiba kwa chama hicho kutokana na msimamo wake wa kudai serikali 3 kinyume na msimamo wa chama chake.Pia mbunge huyo ametuhumiwa mara kadhaa kuwa anatumiwa na CHADEMA.

Chezea Tyson weye!Wassira muuaji
 
Back
Top Bottom