DOKEZO Ester Noah Mwanyilu, Mwanafunzi wa kidato cha tano shule ya Pandahill Mbeya amepotea

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Sio kweli, shule inatoa ushirikiano mkubwa sana...Ukiangalia platforms zote za shule zinatoa taarifa juu ya upotevu wa mwanafunzi huyu. Kuanzia waalimu, viongozi na wafanyakazi wengine wasiokua walimu wanatoa taarifa.

Mpaka wanafunzi walioruhusiwa na wazazi wao kuwa na simu nyumbani huku wanasambaza taarifa hizi. Kwenye groups nyingi za Whatsapp wamesambaza pia hiyo taarifa..Kwa Polisi sijui Bado. Pengine labda mzazi anahitaji mtoto apatikane Kwa haraka, ndo inapelekea yeye kusema hivo..Well mengine Mungu anajua zaidi.
Huyo mwalimu anayeweka maisha magumu kwa wanafunzi hapo shuleni ndo kushikwa mpaka aseme mtoto yuko wapi.,
 
Walimu wa nidhamu hutwishwa mizigo mizito sana pale mambo yaendapo mrama!
Huenda mwalimu Jimmy hana kosa lolote dhidi ya Esther.
Cha maana hapa tuungane kumwombea Esther awe salama huko aliko. Kama anaweza soma hapa , Esther tafadhali rejea nyumbani au shuleni huna kesi ya kujibu.
 
kuna vi ticha vis…enge sana vikimtaka mtoto wa kike asipokubali kuliwa ataishi maisha magumu sana shuleni hayo nilishayashuhidia sana.

sijui dawa ya hii kitu ni nini aise
 
Mtoto Ester Mwanyilu kodato cha Tano shule ya secondari Pandahili ametoweka kwa zaidi ya mwezi sasa.
IMG-20230622-WA0027.jpg

IMG-20230622-WA0028.jpg
IMG-20230622-WA0026.jpg


Mama wa mtoto akapaza sauti,


Hatimaye waziri mkuu akaagiza msako.. ni kivumbi na jasho Azo mata Azo kita mtoto apatikane.
IMG-20230622-WA0045.jpg

Enyi walimu mlio zoea vya kuchinja vya kunyonga mtaviweza?
Tukutane hapa kama jamii kumtafuta mtoto Ester...
 
Nchi hii iko na mambo ya ajabu sana .. mwalimu katajwa kwa barua aliyoandika huyo mwanafunzi lakini bado serikali imekula buyu.

walimu sidhani kama mtakuja kuwa na maisha mazuri kiukweli kama hali itaendelea kuwa hivi.

ualimu umekuwa kama genge la wahuni daah inauma.
itoshe basi.
Screenshot_20230623-000324_YouTube.jpg
nziu
 
Walimu wa nidhamu hutwishwa mizigo mizito sana pale mambo yaendapo mrama!
Huenda mwalimu Jimmy hana kosa lolote dhidi ya Esther.
Cha maana hapa tuungane kumwombea Esther awe salama huko aliko. Kama anaweza soma hapa , Esther tafadhali rejea nyumbani au shuleni huna kesi ya kujibu.

Na changamoto ya malezi inaanzia nyumbani
Tunalea watoto kama mayai
Tunawadekeza sana
Walimu wanapata wakati mgumu. Anyway tuendelee tu kumuombea mtoto apatikane
 
Hatutaki mkataba wa DP world. Yunataka bandari zetu.

Nchi nzima inazungumzia mwanafunzi kupotea...kwani ni mara ya kwanza kwenye nchi hii?

Watanzania nawasanua amukeni. Daini bandari!
 
Kwa kweli inasikitisha mno, Mwanafunzi

Naomba wana JF muisikilize audio hii kwa umakini pia vyombo vya serkali vinavyohusika vichukue hatua.

==========
Siamini kuwa shule imemficha, mtoto amepitia mawazo ya kujitafuta PCB kashindwa kuhimili mikiki saizi anawatesa wazazi tu.

Hizi shule ni uvumilivu, unapokwama kuna mahali pako ambapo unaweza wasilisha changamoto zako ukapata msaada wa kimawazo kabla ya kufanya maamuzi.

Niko hapa kusubiri report ya mwisho njue kosa liko wapi.
Tumhoji Jimmy kwanza
 
Back
Top Bottom